Hivi ndivyo unavyoweza kuwa Mwanaume wa hadhi/daraja la juu"high - Value man"

Hivi ndivyo unavyoweza kuwa Mwanaume wa hadhi/daraja la juu"high - Value man"

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,059
Reaction score
79,405
HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUWA MWANAUME WA HADHI/DARAJA LA JUU"HIGH - VALUE MAN"

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Baada ya Uzi huu Mambo ambayo yatakufanya uwe A Broke Man (Mwanaume aliyefeli)
Ambao niliandika mambo yatakayokufanya uwe mwanaume aliyefeli sasa nimekuandikia Uzi mwingine wa kukufanya uwe mwanaume mwenye hadhi/daraja la juu ambapo kwa kikwere tunasema High-Value Man.

1. Jitambue ili uweze kujiheshimu.
Kujiheshimu huweza kubeba pia maana ya kujitambua.
Ili uwe mwanaume wa daraja la juu lazima ujiheshimu.
Ujijue na kujitambue wewe ni Nani.
Ujue nini unatakiwa kufanya kwa wakati gani.
Uwajue watu wanaokuzunguka na kuwaweka katika makundi yao wanayostahili.
Ujue mazingira yako.

2. Thamini Muda wako( Kuwa mwanaume mwenye mipango na malengo)
Tumia muda wako kwenye vitu vyenye tija kama
a) Kujikuza na kujiimarisha kiuchumi na KAZI au taaluma yako.
b) Kujenga Mahusiano bora yenye tija. Kama mahusiano ya kifamilia, kibiashara au kikazi, na mahusiano na Mungu wako
c) Kujifunza vitu vipya. Hapa Njia Bora za kujifunza Kusoma vitabu au makala au maandiko yenye tija kama kina Taikon Master, jifunze zaidi na zaidi taaluma au kile unachokifanya kwa kusoma kozi iwe mtandaoni au chuoni kabisa, tembea na safiri maeneo mengine ya dunia. Hudhuria kwenye maonyesho, makongamano na mikutano yenye tija.
d) Uwe na Muda mzuri wa Kupumzika.
Hakikisha kwa siku angalau uwe umelala masaa yasiyopungua Saba au nane. Kulala ni afya na itakusaidia kadiri unavyokuwa mtu mzima hasa uzeeni.
e) uwe na Muda wa kuongea na nafsi na Mungu wako.
Hii inaitwa kujitathmini, kutafakari na kuiangalia hatma yako.

3. Vaa mavazi yanayokupa mwonekano wenye utukufu na heshima.
Kumbuka watu watakuzingatia na kuku-judge kwa mwonekano wako.
Watakutafsiri kwa vile unavyoonekana.
Vaa nguo Safi na nzuri. Zinazokukaa vizuri. Sio masulupwete au mabwangwa. Au zinazokubana Sana
Mavazi ni utambulisho.
Yanaweza kukupandisha au kukushusha.
Vaa kulingana na wakati, umri, mazingira na matukio.

4. Jifunze Ujuzi wa Kuwasiliana (Communication Skills)
Mwanaume wa daraja la juu lazima uwe na uwezo wa kuwasiliana kwa kiwango cha kuridhisha.
Uijue lugha vilivyo. Ujue kusoma kwa ufasaha, kuandika kwa ufasaha, kusikiliza kwa Makini, na Kuzungumza.
Makosa ya matamshi hayatarajiwi kwa High Value man. Sijui kuchanganya herufi sijui R na L, F na V, S na th n.k. hupaswi kuwa miongoni mwa wanaofanya hivyo.
Ndio maana unatakiwa ujifunze. Usiwe mtu wa kusema nimeathiriwa kanakwamba huwezi kuondoa hizo athari.

Kwenye mawasiliano kuna semnatiki yaani kujua maana iliyopo kwenye maneno.
Lazima uwe na uwezo wa kuelewa kinachosemwa au kilichoandikwa, au mchoro au picha kwa upesi.

Lazima ujue kupangilia maneno wakati unazungumza. Na lazima yawe na mantiki.

5. Usiwe mwanaume wa Kukimbizana au kushobokea wanawake (Don't Chase Women).
Moja ya dalili kuwa were ni mwanaume wa kawaida au uliyefeli ni kukimbizana na wanawake.
Wanaume wa daraja la juu hawakimbizani na wanawake. Hukimbizana na malengo na kutimiza ndoto zao.

Ukiona unasema wanawake wanaringa au wanadharau ujue bado unakazi kubwa ya kufanya. Wanawake huwaringia wanaume wa daraja la chini ambao huwakimbilia na kuwashobokea.

Jitafute, kuwa mtu wa kukimbizana na ndoto zako. Wanawake wazuri watajileta wenyewe.
Ukiwashobokea na kukimbizana na wanawake utakosa vyote. Utakosa wanawake na hutatimiza ndoto zako.

Usitumie pesa kutaka mwanamke akupende. Hiyo ni dalili wewe huna hadhi wala sio daraja la juu. Ni dalili pia hauna lolote.
Mwanamke anatakiwa yeye ndio ajione anabahati ya kuwa na mwanaume mwenye hadhi kubwa kama wewe.

6. Tengeneza mtandao na watu wenye nguvu.
Lakini ili mtandao huu uwe thabiti lazima nawe uwe na hadhi na daraja linalolingana au kukaribia.
Epuka mahusiano yoyote ambayo ni sumu kwako au wahusika Wana bad and negative energy.
Watu wenye negative na bad attitude hao ni toxic Relationship.

7. Kuwa Mwanaume mwenye Maamuzi na Msimamo thabiti lakini wenye Tija.
Hii itamaanisha usiwe mwepesi wa kutoa maamuzi bila kuyatafakari Kwa Kina.
Mtu mwenye Maamuzi na Msimamo hujulikana pia kama mtu anayetimiza kile anachokisema.

Ndio maana mwanaume hupaswi kuwa Roporopo au muongeaji Sana hasa ukijijua akili yako hainyumbuliki kwa upesi. Yaani Slow learner.
Ila kama unajua ni active learner kuwa muongeaji kwako sio tatizo

8. Usiwe Mtu unayetabirika
Usiruhusu mtu au watu wakujue kwa haraka. Usiruhusu watu kukadiria hatua zako zinazofuata.
Kwa lugha nyepesi uwe msiri, usiwe mtu wa kutoa mipango na mikakati yako.

Jifunze kuwa mbele ya mawazo ya watu hasahasa adui zako.

9. Linda Reputation (Brand) Yako.
Kujijenga na kufanya watu wakuelewe na kukuamini inachukua Muda mrefu.
Fikiria wakati unaanza watu walivyokuwa wachache wanaokuamini na kukuelewa kile unachokifanya.
Labda ni biashara au huduma fulani. Leo umekuwa mkubwa unawatu wengi. Jina lako limekuwa na nguvu. Alafu MTU mmoja atake kuliharibu na kulichafua kwa usiku mmoja.

Linda brand yako.
Brand inalindwa Kwa mambo yafuatayo;
a) Uaminifu
b) consistency (sijui no uthabiti au umadhubuti) lakini maana yake ni kutokubadilika badilika na ikibadilika basi inazidi kuwa bora zaidi. Sio Leo umeanza kupata vimilioni moja au mbili unaanza kushusha ubora wa huduma kwa wateja au ubora wa bidhaa.

10. Lazima uisaidie Jamii yako.
Mwanaume wa daraja la juu lazima atengeneze mazingira ya kusaidia na kushika mkono wale ambao anaona wanahitaji kushikwa mkono kwa maslahi ya Jamii na taifa.
Kutoa misaada na huduma za kijamii ni Moja ya vipaombele vya High Value Man.

11. Lazima aache Mwanafunzi wa kumrithi.
Iwe ni mtoto wake au mtu mwingine atakayeona anafaa. High Value Man hatakubali afe Bola kuacha MTU nyuma yake wa kushika Mikoba yake.
Lazima amuandae mtu mwingine wa kumpokea kijiti.
Amfundishe na kumrithisha mambo ya msingi ili yeye akiondoka nyuma yake yupo kijana wa kuendeleza gurudumu.

Nimechoka! Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Shukrani kwa uzi mkali, uzi unafaa utolewe copies upigwe lamination kikao kijacho kila mwanaume apate nakala yake.
 
Back
Top Bottom