BIG Africa
Member
- Oct 15, 2022
- 84
- 116
"LIGI yetu inaeendelea"."Ligi yetu imepiga hatua".Hizi ni baadhi ya kauli za watu ambao wamekuwa wakijitokeza na kusema hivyo.
Binafsi sidhani.Kwani maendeleo ya ligi kuu huwa yanatazamwa kwa kuangalia vigezo vipi katika timu?.Jibu ni jepesi tu.
Ni viwanja bora vya timu,malipo mazuri ya wachezaji na benchi la ufundi ambayo hutokana na uwekezaji mzuri ndani ya klabu na kadhalika.Sasa tujiulize swali.
Timu zetu zina miundombinu bora ya soka?.Jibu ni hapana.Inashangaza kuona hata timu kubwa kama Simba na Yanga na zenyewe hazina viwanja vyao vya mechi,achana na viwanja vya mazoezi.
Azam FC na Kagera Sugar tu ndiyo timu zenye viwanja vyenye hadhi ya Ligi Kuu.Uwanja wa Benjamin Mkapa sio wa Simba wala Yanga.Ni wa serikali.
Nchi hii mambo mengi sana kwenye soka bado hayajakaa sawa tofauti na watu wanavyodanganyana.
Nilichokuja kugundua ni kwamba watu wengi wanaitazama Ligi Kuu yetu kwa kuangalia timu tatu tu.Simba,Yanga,na Azam FC.Basi.Bado kuna pengo kubwa sana kati ya timu zetu ndogo na timu zetu kubwa.