Hivi ndivyo Tabia ya kupenda kujisomea ilivyoboresha maisha yangu. Inawezekana hata kwako pia

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Naomba nikiri kwamba mimi ni muumini mzuri wa kupenda kujisomea na vitu bora kwenye maisha yangu vimetokana na kujisomea na kujifunza mwenyewe. Leo nataka kukuonesha jinsi tabia hii ya kujifunza na kujisomea mwenyewe ilivyoboresha maisha yangu na inavyoweza kuboresha maisha yako pia kama utaijenga kwako.

Mwaka 2011 nilijikuta katika wakati mgumu sana kwenye maisha yangu baada ya kusimamishwa chuo kikuu kwa muda usiojulikana. Baada ya kupewa barua ya kuondoka chuoni haraka, niliingia mtaani nikiwa sina mbele wala nyuma. Lakini kwa kuwa nilishazoea kujishughulisha kwa shughuli mbalimbali nilianza kujishughulisha mtaani ili maisha yaweze kuendelea.

Mwanzoni mwa mwaka 2012 niliamua kuanza kujifunza vitu vya ziada ili niweze kuongeza ufahamu wangu na fursa za kutengeneza kipato cha ziada. Kwa kuwa nilikuwa mpenzi na mtumiaji mkubwa wa kompyuta niliamua kujifunza IT(Information Technology). Nadhani unajua kozi hii inafundishwa vyuoni, tena sana sana vyuo vikuu, lakini mimi nilianza kujifunza mwenyewe kwa kutumia kompyuta yangu na mtandao wa intanet. Nilidownload vitabu vya pdf, video na material mengine muhimu kwa ajili ya kujifunza mambo haya. Baada ya miezi sita nilikuwa nimeshajifunza vitu vifuatavyo; Website designing, Graphics design na Java programing. Kwenye Graphics design nilijifunza kutumia adobe photoshop, adobe dreamweaver, adobe fireworks na adobe illustrator.

Baada ya hapo nikajifunza sales na marketing. Nilijifunza kwa kusikiliza vitabu na kusoma vitabu zaidi ya kumi vinavyohusiana na sales na pia vinavyohusiana na marketing. Kupitia ujuzi wa sales niliojifunza nilielewa ni jinsi gani ulimwengu wa biashara unavyokwenda na ni vitu gani vinawafanya watu kununua au kutonunua bidhaa.

Pia kwenye marketing nilijifunza mbinu mbalimbali za kutafuta masoko ya bidhaa au huduma yoyote, jinsi gani ya kuweza kutengeneza soko hata sehemu ambayo inaonekana haiwezi kuwa na soko. Nilijifunza kwa nini baadhi ya bidhaa zinafanikiwa sana sokoni na kwa nini bidhaa nyingine zinashindwa kuhumili mkikimkiki wa soko.

Wakati huo huo nikawa najisomea na kusikiliza vitabu vya maendeleo binafsi(personal development). Hivi viliniwezesha kubadili mtazamo wangu na kuniwezesha kujiamini na kuweza kufanya kile nachofikiria kufanya bila ya kuogopa pale wengine wanaponikatisha tamaa. Hapa nimesikiliza na kusoma zaidi ya vitabu mia moja kutoka kwa wahamasishaji maarufu kama Antony Robins, Zig Zigler, Brian Tracy, Les Brown, Earl Nightngale, Robert Kiyosaki, Donald Trumph, John Maxwell, Napoleon Hill na wengine wengi.

Pia nikajisomea na kujifunza kuhusu uongozi, kitu ambacho bado naendelea kujifunza mpaka sasa. Katika kujifunza mambo ya uongozi nimejua ya kwamba kwenye kila nyanja ya maisha wanaofanikiwa ni wale wenye tabia za uongozi. Wanaokuwa wazazi bora, wafanyabiashara bora, wanaofanikiwa kwenye ujasiriamali na hata wafanyakazi bora wote wanasifa moja ya kuwa na tabia za uongozi.

Pia nimejifunza na naendelea kujifunza uandishi wa makala bora na vitabu.

Mwaka 2012 nilikuwa nasoma vitabu vingi niwezavyo ndani ya muda wowote ninaokuwa nao, hivyo kwa mwaka ule nilisoma na kusikiliza vitabu zaidi ya 120.

Mwaka 2013 nilipanga kusoma vitabu viwili kila wiki na kwa mwaka huo nilisoma na kusikiliza vitabu zaidi ya 70.

Mwaka huu 2014 nimepanga kusoma kitabu kimoja kila wiki na ni wiki chache ambazo sikumaliza kusoma kitabu.

Tabia hii ya kujisomea imenisaidia nini?

Labda unajiuliza kwa kusoma mavitabu yote haya nimefaidika nini? Jibu ni kwamba maisha yangu nayaendesha kwa ujuzi nilioupata kutokana na kujisomea vitu hivi mbalimbali. Kuanzia katikati ya mwaka 2013 mpaka sasa na kuendelea sehemu kubwa ya kipato cha kuendesha maisha yangu na familia yangu nakipata kwa ujuzi niliojifunza kutokana na kujisomea.

Nafanya biashara za kawaida, biashara za kwenye mtandao wa intanet (Internet marketing), naendesha blog nne, natengeneza na kurekebisha blogs na website na pia nafanya shughuli nyingine mbalimbali. Yote haya sikuwahi kufundishwa na mtu yeyote, hata kuwasha kompyuta sikuwahi kufundishwa. Ni tabia yangu ya kupenda kujisomea ndiyo iliyoniwezesha kufanya yote haya.

Hata wewe unaweza kunufaika na tabia hii

Nakueleza yote haya ili kama na wewe ukipenda kuboresha maisha yako uweze kujijengea tabia ya kujisomea na kujifunza wenyewe.

Kwa kuwa hii ni tabia hivyo inahitaji kujengwa. Inawezekana unapenda sana kujisomea ila kila ukijaribu unashindwa. Au unapenda kujisomea ila unaona huna muda wa kutosha kufanya hivyo.


Mwisho wa kujiunga na kisima cha maarifa ni leo hivyo chukua hatua mapema kama hutaki kukosa nafasi hii muhimu ya kujijengea tabia ya kujisomea ambayo itakusaidia kuboresha maisha yako.

Katika ulimwengu wa sasa ambapo ajira zimekuwa ngumu kupatikana na hata kufanya ni muhimu sana kujifunza vitu vya ziada.

Nakutakia kila la kheri kwenye harakati zako za kuboresha maisha yako.

TUKO PAMOJA.

========

Recommended on JamiiForums:

1)
Utamaduni wa kujisomea, kuelewa na siasa za Tanzania
2) USHAURI: Ni vema tukajenga utamaduni wa kujisomea vitabu na kuwajengea watoto utaratibu huo
 
Hongera sana makirita. Tatizo la watanzania wengi ni wavivu,mni wavivu wa kuishughurisha miili yao na akili zao katika kupambana na harakati za maisha. Kujisomea ni moja ya mambo muhimu sana katika kuendeleza maisha ya binadamu. In 1990, nilikuwa naxoma sana novel za james hadley chase, zilinisaidia kunipa uwezo wa kutathmini viyu kwa haraka, kufahamu mbinu mbali ambazo wengine ziliathiri maisha yao. In 1995 nilikuweza kupata courage na kuweza kuandika hadithi na makala kwenye magazeti ya majira na mfanyakazi. Marehemu Nick maira (Mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi-amein), alikuwa msaada mkubwa sana kwangu. Wakati huo watu kama kina maulidi kitenge na julius samweli walikuwa ndio wapya kabisa kwenye game. Hivi karibuni, mwaka 2010 jilikuwa na hali ngumu sana katika maixha, niliporomoka ghafla kwenye maisha. Vitabu vya mtunzi mnigeria aitwae Praise George nilivyovisoma vimesaidia sana kubadili fikra zangu na maisha yangu. Sasa hivi maisha yangu yameboreka sana, kutoka na mwanga wa waandishi hao. Usomaji wa vitabu husaidia pia katika kujenga kujiamini katika mambo mengi sana na kukufanya huwe na fukra huru zaidi. Ni vigumu sana kumdanganya au kumlisha sumu mtu mwenye tabia ya kupenda kusoma vitabu. Tuko pamoja Aman. Ni add kwenye list yako.
 
Inatia moyo sana....

Pengine tatizo la msingi mbali na muda ni lugha, machapisho mengi yapo kwa lugha ngeni hivyo hupunguza hamasa ya kusoma.
 
Hongera kama unatabia ya kujisomea, kila siku hua nawapigia watu kelele the same thing...

ila ulivosema una blog nne, ni zipi hizo? kama kuna hata moja yenye ngono ngono ka blog nyingi za bongo zilivyo heshima inashuka.. sivipendi viblog vya bongo bac tu..
 
Nice thread to step in.... Nakuunga mkono 100% vitabu vina maarifa mengi kuliko tunayosikia. Tujenge tabia ya kujisomea. Hata mimi nakiri kuwa kujisomea vitabu kumebadilisha sana maisha yangu. Nawasihi na wengine kushiriki kujisomea vitabu.
 
Mkuu uko smart sana....nakushauri kitu kimoja....concetrate kwenye kitu kimoja ambacho hakina watu wengi....utatoka

Asante sana mkuu. Nalielewa hilo vizuri sana, haya niliyoeleza mengi nilianza kufanya tangu 2012 lakini kwa sasa mengi nimepunguza. Nafanya internet marketing, blogging na personal development trainings.
 
Hongera kama unatabia ya kujisomea, kila siku hua nawapigia watu kelele the same thing...

ila ulivosema una blog nne, ni zipi hizo? kama kuna hata moja yenye ngono ngono ka blog nyingi za bongo zilivyo heshima inashuka.. sivipendi viblog vya bongo bac tu..

Asante mkuu. Blog zangu zote ni za kufundisha na kuhamasisha. Siwezi kufanya hizi za kuripot habari za udaku, sio saiz yangu kabisa. Sijaweka link za blog kwa sababu JF hawapendi ninapoweka link, huwa wanazifuta.
Ila moja ya blog zangu ni www.amkamtanzania.com inaitwa AMKA MTANZANIA unaweza kuitembelea na kujifunza zaidi.
Karibu sana.
 
Kusema ukweli unastahili pongezi Makrita. Siku zote mtu mwenye bidii na asiyekata tamaa hufanikiwa hatimaye. Umesoma vitabu vingi sana, umefanya mambo mengi sana lakini kwa kusikitisha umesahau kusoma (au kutaja) hata kitabu kimoja cha dini.
Hata ungekuwa na mafanikio makubwa jinsi gani kama hujui ni kwa nini upo hapa duniani umekwisha. Kumbuka maisha ya mwanadamu hapa duniani ni mafupi mno, hufikishi miaka 80 wewe. Kama una miaka 40 sasa jua kwamba baada ya miaka michache tu ijayo utakuwa umezeeka chakali na mwili umechoka hoi. Macho hayaoni vizuri, masikio hayasikii vizuri, miguu haina nguvu na baadaye unakufa.
Anza kufanya utafiti sasa, chunguza na kujimba kama ulivyozoea kufanya na utakuwa mmoja wa watu wenye furaha sana hapa duniani.
Nakutakia utafiti mwema
 
Heshima kwako kaka. karibu pia kwenye ulimwengu wa kuandika. tukijifunza na kupata maarifa baada ya kusoma vitabu tujitahidi kuandika kwa kadri tunavyoweza ili jamii yetu inufaike na maarifa mapya uliyoyapata! Jana nilifanya hesabu za haraka haraka kujua idadi za makala nilizo andika mpaka sasa nilishtuka kwa kuwa bado idadi ni ndogo sana kulinganisha na umri wangu, makala zaidi ya 5400 kwenye fb na social network nyingine achilia mbali magazeti kama Tanzaniadaima, the late banned Mwanahalisu, jamhuri nk.

Naungana na wewe tuendeleze mapambano.
 
Kusiwe na ada lakini,

Nauli elfu kumi tu! Mbona vinywaji unanunua na ofa kibao unatoa!! Cha kumi kumchangia Makirita na hali unapata faida kubwa si kwako tu unaweza kuipitisha hata kizazi chako chote ujawapa urithi mkubwa ulionunua shilingi elfu kumi tu.
 
Heshima kwako kaka. karibu pia kwenye ulimwengu wa kuandika. tukijifunza na kupata maarifa baada ya kusoma vitabu tujitahidi kuandika kwa kadri tunavyoweza ili jamii yetu inufaike na maarifa mapya uliyoyapata! Jana nilifanya hesabu za haraka haraka kujua idadi za makala nilizo andika mpaka sasa nilishtuka kwa kuwa bado idadi ni ndogo sana kulinganisha na umri wangu, makala zaidi ya 5400 kwenye fb na social network nyingine achilia mbali magazeti kama Tanzaniadaima, the late banned Mwanahalisu, jamhuri nk.

Naungana na wewe tuendeleze mapambano.

Asante sana mkuu. Kuandika naandika sana, nimeshaandika vitabu viwili na vingine viwili bado naandika. Nimeandika makala zaidi ya 300 kwenye AMKA MTANZANIA na hivi karibuni nimeanza kupeleka makala zangu magazetini ila badi hazijachapwa.
Kwa kuwa wewe upo kwenye sekta hii kwa muda mrefu nafikiri naweza kujifunza vingi kutoka kwako na pia tukashirikiana. Naomba kama hutojali tuwasiliane kwa email amakirita@gmail.com au simu 0717396253.
Pia unaweza kutembelea AMKA MTANZANIA www.amkamtanzania.com
Asante na karibu sana.
 
Inatia moyo sana....

Pengine tatizo la msingi mbali na muda ni lugha, machapisho mengi yapo kwa lugha ngeni hivyo hupunguza hamasa ya kusoma.

Na ndo hapo umuhimu wa kujifunza kiingereza unapokuja, haihitaji kukaa darasani kujua kiingereza, haya.mambo ya kuenzi lugha ya taifa ndo yanarushisha wengi nyuma, tujifunze kiingereza, kiswahili tutake tusitake tutakijua tu, hakikwepeki. Hao wanaohamasisha kiswahili watoto wao wanasoma kiingereza. Wake-up.
 
Back
Top Bottom