Hivi Ndivyo Itakavyokua! Mengine Tumuachie Mungu...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Ndivyo Itakavyokua! Mengine Tumuachie Mungu......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gottee, Oct 11, 2010.

 1. Gottee

  Gottee Senior Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakati wanachaguana wao kwa wao walikuja na Kauli Mbiu kuwa USHINDI NI LAZIMA! Hatukuwaelewa kwa sababu tushawazoea. Kwani walishawahi kusema Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya na Tanzania Yenye Neema inawezekana. Hayo yote yamekuwa ni 'longo longo' tu. Kwa hiyo walipokuja na USHINDI NI LAZIMA tukasema hiyo ni longo longo nyingine.

  Mwanzoni kwa kutumia Mafisadi walianza kudhoofisha vyama vingine ili Mgombea wao safari hii asiwe na mpinzani katika Uchaguz Mkuu au ikishindikana awe na wagombea dhaifu. Nani hakumbuki kauli za ajabu ajabu za Zitto Kabwe kutaka kuivuruga CHADEMA? Ikaenda ikaenda ikaenda wakajua safari hii mpinzani ni Mchungaji Mtikila, yule Bwana Mdogo Mziray, yule Dakatari wa SAU. CUF waliliona hilo kuwa JK anataka kupita 'kiulaini' ndipo Profesa naye akaamua kuwania kiti cha Urais. Lipumba hakuwa tishio kwa JK ila walikerwa kwani safari hii walitaka ule USHINDI WA LAZIMA uwe ni wa asilimia 95.

  Ndipo akatokea huyu Padri wa Karatu. Mwanzoni CCM walimuona kama mtu ambaye amekurupuka, mengi yakaanza kusemwa ikiwemo kwamba amewasaliti wananchi wa wake wa Karatu. Siku zilivyoendelea nyota ya Dk Slaa ilizidi kung'ara. CCM wakaanza rafu ambazo ni za kijinga na pia ni za kitoto. Dk Slaa akaanza kusakamwa kwa maisha yake binafsi. Akatafutwa mtu ambaye anadai yule mchumba wa Dk Slaa ni mke wake wa ndoa. Mahimbo kudai kaporwa mke wake si kosa na wala si dhambi, hata mimi labda yangenikuta hayo ningeweza kudai 'kurudishiwa' mke wangu. Kilichotuacha hoi ni Mahimbo kupangiwa hoteli na kupewa 'mkoko' na CCM. Mbaya zaidi mahojiano ya Mahimbo na TBC One yalifanyika kwenye Ofisi binafsi ya Mgombea Urais wa CCM, Jakaya Kikwete inayoratibiwa na mwanae wa kuzaa, Miraji katika muendelezo wa ubia wa Urais na Familia ile ya kutoka Bagamoyo.

  Pamoja na mbinu hizo za 'maji taka' nyota ya Slaa ilizidi kung'ara. Kampeni za JK zikawa zinapwaya kulinganisha na zile za Dk Slaa pamoja na CCM kutumia nguvu ya ziada ikiwemo kuzunguka na wasanii wengi 'wanaouza sura' zao kwa sasa kwenye Runinga ikiwemo lile kundi la 'wavaa magauni' la Ze Komedi Orijino ukiachilia mbali wale wasanii wa Bongo Fleva ambapo fungu la malipo yao analo Miraj Kikwete. CCM pia wamekuwa wakikodi mabasi kukusanya watu vitongojini ili kujaza mikutano ya mgombea wao. Yote haya hayakusaidia! Huwezi amini hapa Mbeya siku ambayo JK alihutubia Uwanja wa Sokoine umati mkubwa wa watu ulijaa pale lakini alipoanza kuhutubia umati ule ulianza kutoka na wachache niliopata nafasi ya kuongea nao walisema wao walikuja kumuona 'mtoto wao' Masanja Mkandamizaji na kwa kuwa walishamuona hawakuwa na jipya la kumsikiliza Meneja Miradi wa CCM Jakaya. Pale Tunduma JK alipouliza kama wananchi watachagua CCM, kama ilivyoripotiwa na TBC kuwa walijibu, Ndiooooo! Lakini TBC wakashindwa kusema kwamba walijibu hivyo huku wakimwonyesha JK alama ya vidole viwili ambayo ni alama ya 'wavaa magwanda' wale.

  Ukweli ni kwamba CCM inajua imeshikwa pabaya. Kwa kauli Mbiu yao USHINDI NI LAZIMA medani ya ushindi imeanza kutafutwa nje ya Uwanja wa Mapambano. Kauli za hivi karibuni wananchi wenzangu si za kupuuzia. Alianza Tendwa kuidhinisha JK ame anahutubia Kampeni zake hata Usiku wa Manane na akijua hilo haliko chini ya mamlaka yake. Akaja Jenerali Shimbo na 'mkwara wake' wakaja Tume ya Uchauguzi na Takwimu zao kuwa wananchi waliojiandikisha kupiga kura wamefika milioni kumi na tisa! Mwe! Wakaja REDETI na madudu yao. Juzi wale SINOVETI wameediti taarifa yao ya mwanzo ambazo wamekuwa wakisita kuzitangaza hadi walipoamua kukopi kwa sehemu kubwa REDETI. CHADEMA walishapata ule utafiti wao SINOVETI wa mwanzo na walipoona 'uko sokoni' kwa muda mrefu wakalipua bomu. SINOVETI wakaja juu na kutishishia kuishitaki CHADEMA, wakaambiwa nendeni mahakamani. Nani aende?!

  Ndugu zanguni nataka tujiandae kulipokea hili la USHINDI NI LAZIMA la CCM. CCM imeshajua kuwa imepoteza imani na wananchi na ni kiini macho pekee ndicho kitakachoiokoa. Kwa hiyo kwa maelezo hapo juu ushindi wa CCM umeshatengenezwa na ndio maana Kiravu wa Tume ya Uchaguzi amesema matokea ya kura za Urais yatatangazwa baada ya siku moja. Kwa miundo miundo mbinu hii ya nchi yetu?

  Kwa maelezo hayo hapo juu mimi natabiri yafuatayo.

  JK atashinda kwa ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 80. Meneja wa Kampeni ya JK yule mwanajeshi mstaafu ataitisha mkutano na vyombo wa habari na kuanza kuwaponda SINOVETI na REDETI kuwa utafiti wao haukuwa wa kitaalam kwani mgombea wao ameshinda kwa majini kubwa. Kwa maana nyingine kinana wa CCM ataungana na kina Baregu wa CHADEMA kuziponda taasisi hizo a kwa maana hiyo ngoma itakuwa droo.

  Kina Slaa na Mbowe na wenzao watafunguliwa kesi ya uhaini, kwa kutaka kuleta umwagaji damu na Shimbo ataibuka kuwa shujaa wa karne, na kwenye sikukuu ya Uhuru atakabidhiwa nishani ya kutukuka kwa kuiokoa nchi yetu kwenye mauaji ya uwagaji damu.

  Zitto Kabwe atashinda ubunge wake na kwa mara ya kwanza atakapokuwa anahojiwa na waandishi wa habari, atasema uchaguzi mkuu Tanzania ulikuwa wa huru na haki. Hapo kutakuwa na mpasuko mkuu wa Chadema ikimaanisha mwaka 2015 hakitakuwa tena chama kikuu cha upinzani Tanzania Bara.

  Baada ya kuapishwa, JK ataanza kuwananga wapinzani wake, akianza na wafanyakazi akiwaambia alishasema atashinda bila Kura zao na ndivyo imekuwa. Atamsifu sana Kiongozi wa TUCTA Mgaya na kusema mwanzoni hakuwa anamuelewa lakini sasa anamuelewa vizuri na yeye Mgaya amemuelewa JK (Ile mishahara ya siri, nasikia TUCTA walipata special package)

  JK pia atasema huu ni wakati muafaka wa kuvunja makundi ndani ya CCM na hivyo wagange yajayo. Na katika kuunda serikali yake ameamua kuunda serikali ya UMOJA WA KITAIFA. Atawashukuru sana viongozi wastaafu wa Serikali zilizopita wakiwemo Mkapa, Sumaye na wengine. Atasema yeye ndiye aliyefanikisha kumuingiza 'Mzee Mkapa' (anavyopenda kumuita) kwenye ile tume ya kura za maoni za Sudan ya Kusini baada ya kufanya mazungumzo na Barack Obama na maongezi ya simu ya muda mrefu na Ban Kin Moon. Atamhakikishia Sumaye kama anataka kwenda tena Marekani kusoma PhD basi yeye au ikiwezekana Ridhiwani au hata Miraj watamlipia Karo na gharama zingine akiwa huko Marekani.

  Natabiri Serikali ya UMOJA WA KITAIFA itajumuisha Mawaziri wafuatao. EL atarudi kuwa Waziri Mkuu wa JMT. Wakati JK anatamka jina lake atasema kurudi kwenye u PM sio jambo la ajabu kwani hata Hayati Baba wa Taifa aliwahi kumrudisha Moringe Sokoine kwe u PM baada ya kumtema. Ataelezea umuhimu wa Lowassa kurudi ni kumalizia yele aliyoyaanzisha ikiwemo Richmond, Mvua za Maleshia, nk

  Pinda kwa sababu ni 'mbangaizaji' atamrudisha kule TAMISEMI akabangaize na wabangaizaji wenzake hasa Wakurugenzi wa Halmashauri na pia akamalizie lile soo lake la kuuza Uwanja wa Nyamagana.

  Kuna mwanamama atapewa Wizara nyeti kwa sababu tu ni girl friend wa yule Fisadi Mkuu wa EPA. Ndio si unajua yule fisadi yeye hataki kuchanganya Siasa na Biashara so yeye atastick kwenye biashara zake ikiwemo kufuatilia deni lake la helikopta iliyotumika kumdani swahiba wake. Na pia ile kadhia ya Dowan kwani bado ni mbichi.

  Spika wa Bunge atachaguliwa kuwa Phillip Marmo na tunachotarajia safari ni kuona Bunge la Kihistrioa ambalo kuanzia siku ya kwanza ya ufunguzi wake hadi linapovunjwa mwaka 2015 litatumia muda mwingi kumsafisha na kumsafishia njia 'Rais' wao mtarajiwa EL.

  JK atamrudisha kwenye ile Wizara ya Utamaduni, George Mkuchika ili amalize ile kazi, ikiwemo ni kulifungia na kulimaiza kabisa gazeti la Mwanahalisi, kutoa onyo ikiwemo karipio kali kwa gazeti la Raia Mwema na kutangaza tuzo kwa magazeti ya Uhuru, Habari Leo, Daily News, Mtanzania, Rai, Jambo Leo kwa kuripoti habari za Uchaguzi bila upendeleo. Sifa zingine zitamwendea Tido Muhando na kruu nzima ya TBC. Mkuchika atahitimisha kwa kusema hajutii, 'Kumuiba Tido kule BBC' ingawa serikali ya Malkia ililalamika sana.

  NDUGU ZANGU NAYASEMA HAYA KWA UCHUNGU. ILA TUJIULIZE NJIA YETU KUELEKEA MWAKA 2015 ITAKUWAJE?

  Nawasilisha.
   
 2. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Mabadiliko ni mwaka huu na sio 2015. Like it nor not, ni mwaka huu.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hiyo serikali ya mseto itatumia katiba ipi?
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Huu ndiyo mwisho wa JK na CCM yake. Wajiandae kujifunza siasa za upinzani ambazo hata hivyo hawazijui hata chembe
   
 5. S

  SUWI JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Makala nzuri sanaaaaaaa!!
   
 6. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  yawezekana ikatokea
   
 7. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Watakimbiana...Nguvu ya Umma ikishaamua ndio imeamua...Kule Tarime, raia waliwaambia wanajeshi na polisi, mtupige hadi mchoke ila ushindi wetu mtuachie hamuupati...na jeshi lilirudisha silaha alani wakaachia Ubunge ukaenda Chadema kwa kishindo....Na Urais mwaka huu ndio itavyokuwa..vinginevyo! Tutizame na kuwa macho kama kweli wananchi hawajui kinachoendelea...Ogopa sana wanaovumilia hadi tone la mwisho..wakilipuka wanaondoa na na ile sura iliyofichika na watawala hawataamini litokealo kama kweli au njozi za mchana...
  Tumuombe Mungu sana, hakuna nguvu ngingine au Majini kuzuia hali hii....ni Mungu Peke yake.
  Kumpata kiongozi mwema na mteule ni baraka halisi toka kwa Mungu, na ndio Tanzania imeipata hiyo lakini nguvu za kiza zinatumika na wanadamu kuufunika ukombozi huu....tuwe imara, DAIMA INAWEZEKANA...
   
 8. A

  Akiri JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  yapo mengine umeongea kweli, ni kweli Lowasa anaandaliwa kuwa mbadaala wa huyu jamaa kikwete.
   
 9. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama umetumwa useme! Kila kitu natabiri? wewe umekuwa nani? mabadiliko ya kweli ni mwaka huuhuu!!! Umeandika kurasa nyingi lakini umegusa point chache ambazo ni halisia na zinatoa direction kabisa hata kwa mtu Aliyefumba macho!

  Nenda kaungane na mtabiri mwenzio sheikh yahaya.....muyakatishe mashetani tamaa kwani hayo ndo hayana uwezo kabisa hata wa kupiga kura!
   
 10. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sisi tunatakiwa kuitafakari hali hii...Tuungane na tupaaze SAUTI YA PAMOJA KUWA, NCHI YETU INAKOMBOLEWA, Imepata MKOMBOZI. Hakuna wa kuziba midomo ya wanyoge na wenye haki. Hata nguvu za Mafia zilishindwa, Ukomunisti ulifikia kikomo, Marekani - Republican walitumia style hii hii ya CCM kumdhoofisha Obama kwa kusema ataiweka Marekani kwa Magaidi, yeye mwenyewe gaidi-msomali na sio Raia, ila kwa kuwa mabadiliko yalikuwa ni mkondo usiopindwa kwa njia za kifidhuli na kutisha watu...Obama aliikomboa Marekani, alikomboa kizazi chote na bila mwaka kupita, Obama ametunikiwa Nishani, na heshima ya Marekani imezidi kungara...! Ndiyo maana tunasema, hata wakitumia mbinu chafu, Umafia na kudhoofisha fikra za watanzania kwa woga, mabadiliko lazima...CHANGES ARE COMING...YES WE CAN CHANGE TANZANIA...! UTABIRI HALISIA NI KURA YAKO KWA MABADILIKO UNAYOYATAKA...sio kulia kuwa 'halikutokea, kumbe mwenyewe hukufanya litokee ( that is what we say Changes starts with youself). Tupige kura sasa KWA USHINDI na sio kuproject ya 2015, hizo ni ndoto nyingine na hilo halipo!
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mabadiliko ni mwaka huu, hiyo 2015 tutakuwa tunakamilisha tu!
   
Loading...