Hivi Ndivyo Ilivyokua Kigoma Kaskazini 2010

KACK

Senior Member
Joined
Mar 28, 2015
Posts
129
Reaction score
107
Katika Uchaguzi Uliopita Mwaka 2010 Jimbo La Kigoma Kaskazini Kulikua Na Wagombea Ubunge Watatu Toka Vyama Vya CUF, CCM Na CDM. Kila Mgombea Alikua Na Mbwembwe Zake Katika Kampeni Za Kumuwezesha Apite Katika Kinyang’anyiro Hicho.

Ndugu Omary M Nkwarulo Ambaye Alishindwa Katika Kura Za Maoni Na Ndg Robinson Lembo Ndani Ya CCM Alihamia Chama Cha Wananchi CUF, Huyu Jamaa Alitumia Kauli Mbiu Isemayo NIPE NIKUPE Akimanisha Mpigie Kura Akupe Pesa.

Hakuogopa Kutoa Rushwa, Alifanya Unyama Huo Hadharani Na Baya Zaidi Alitoa Pesa, Sabuni Na Vitu Vingine Kwa Watu Huku Akiwaandika Majina Yao Na Bidhaa Walizochukua Au Kiasi Cha Pesa Zoezi Hili Liliambatana Na Kiapo Kwa Mpokea Rushwa Kuahidi Kumpigia Kura Na Kukubali Kuwajibika Endapo Hatompigia Kura.

Wananchi Wengi Waliogopa Kupokea Rushwa Kutoka Kwa Huyu Jamaa.

Baada Ya Kutoa Hutoba Yake Alikua Anatoa Wasaa Wa Mda Wa Maswali, Hata Hivyo Wasikilizaji Hawakutakiwa Kuuliza Maswali Bali Yeye Aliwauliza Wananchi Maswali Kama Wamemuelewa Na Wako Tayari Kupokea Pesa Na Kujengewa Nyumba Bora.

Baada Ya Uchaguzi Ndg Nkwarulo Alipata Kura 4,839 Sawa Na 10.06% Na Kuwa Wa Mwisho Kwa Wingi Wa Kura. Siku Ya Pili Baada Ya Kutangazwa Matokea Huyu Bwana Alianza Kuwatafuta Wote Aliowapatia Pesa Na Alifanikiwa Kurudisha Baadhi Ya Pesa Zake.

Ndugu Robinson F. Lembo Yeye Alipitia CCM. Huyu Ni Mwajiliwa Serikalini Kwa Mda Mrefu. Huyu Jamaa Hakua Na Hoja Zinazoeleweka Zaidi Ya Kuwatangazia Wananchi Uwezo Wake Wa Kuongea Lugha Nyingi Na Kutembelea Zaidi Ya Nchi 36 Ambazo Kimsingi Sera Hizi Hazikua Na Faida Yoyote Kwa Wananchi.

Alitumia Mda Mfupi Kuongea Mbele Ya Hadhara Na Kuwaachia Makampeni Manager Na Viongozi Wengine Wa CCM Wilaya Kuongea. Alitumia Mda Mwingi Kumshambulia ZZK Personally.

Asingeweza Kusimama Jukwaani Kabla Ya Kunywa Pombe Na Hakuwa Na Uwezo Wowote Wa Kuwasoma Wananchi Wanataka Nini Badala Yake Alianza Kuwakoleza Kwa Pesa (Rushwa).

Aligawa Pesa Nyingi Sana Kwa Sharti La Kupigiwa Kura Bila Vitisho Kama Mwenzake Wa CUF, Vijana Walizishambulia Sana.
Hata Hivyo Wananchi Wengi Walikua Tayari Wanajua Sehemu Ya Kula Na Kupiga Kura.

Mwisho Wa Siku Ndg Lembo Aliambulia Kura 18,352 Sawa Na Asilimia 38.15. Baada Ya Kushindwa Uchaguzi Aliondoka Kijijini Kwao Na Kurudi Dar Baada Ya Siku Mbili Tu, Baada Ya Kukaa Hapo Kwa Kipindi Cha Miaka 3 Akijiandaa Na Uchaguzi.

Ndugu Zito Z Kabwe, Akiwa Anatetea Kiti Chake Cha Ubunge Alikua Na Hoja Nzuri Kwa WanaKigoma Kaskazini, Hata Hivyo Alijichanganya Sana Na Kujiingiza Katika Masuala Ya Rushwa Baada Ya Kushauliwa Na Baadhi Ya Watu Waliomtonya Kuwa Awe Makini Na Tabia Yake Ya Kutowajali Wapiga Kura Kwa Chochote Kwani Wenzake Wanaotoa Rushwa Wanaweza Kumshinda.

‘Mwambieni Lembo Nitamfilisi, Akitoa 1000 Mi Nitatoa 2000, Akitoa 2000 Mi 4000, Nitamfilisi Na Yule Si Size Yangu’ Maneno Haya Aliyasema Zito Baada Ya Kugawa Rushwa Ya Shilingi 1000 Kwa Vijana Kadhaa Jimboni Humo Akilipiza Rushwa Ya Shilingi Mia Tano Ya Bwana Lembo Aliyokua Ameitoa Siku Chache Kabla.

Zito Alikataa Kabisa Kujihusisha Na Utatuzi Wa Migogoro Ya Mipaka Ya Ardhi Katika Baadhi Ya Vijiji Jimboni Kwake Akihofia Kukosa Kura Kutoka Kwa Wananchi Watakaoona Wameonewa Na Maamuzi Ambayo Yangezingatia Haki.

Mwisho Wa Siku Aliibuka Mshindi Kwa Kupata Kura 23,366 Sawa Na Asilimia 48.5.

Baada Ya Uchaguzi Aliondoka Jimboni Na Alirudi Baada Ya Kushindwa Mahakamani Katika Kesi Yake Dhidi Ya CDM Kwa Kisingizio Kuwa NG’OMBE AKIJERUHIWA MALISHONI HUKIMBILIA ZIZINI Bila Kujali Kuwa Ng’ombe Huyohuyo Aliondoka Bila Ruhusa Na Kukaa Malishoni Kwa Miaka Mingi Bila Kuwa Na Dalili Ya Kurudi Zizini Kabla Ya Jeraha.

Suala Kubwa Lililosababisha Kura Zake Kupungua Zikilinganishwa Na Asilimia Ya Kipindi Cha Kwanza Ni Udini Ambao Uliasisiwa Na Wagombea Wote Wa Ubunge Akiwemo ZZK.

Hata Hivyo Zitto Kabwe Leo Hii Ni Mzalendo Baada Ya Kung’atuka Katika Nafasi Ya Ubunge Mwaka Huu Na Ametangaza Nia Ya Kusambaza Uzalendo Kwa Kupitia Kiti Cha Ubunge Jimbo La Kigoma Mjini Akibadilishana Jimbo Na Peter Serukamba Atakayerudi Kigoma Kaskazini.

Atapitia Chama Cha Kijamaa Cha ACT Na Alitoa Mtazamo Wake Wa Kuboresha Ujamaa Ili Kutofautiana Kidogo Na Ujamaa Wa Baba Wa Taifa J.K Nyerere Ambaye Aliwafilisi Watu Kwa Tabia Zao Za Kuhujumu Uchumi Wa Nchi Ukilinganishwa Na Ujamaa Wa ACT Unaoasisiwa Na Kiongozi Mkuu Wa Chama Hicho Aliyetishia Kumfilisi Mgombea Mwenzake Kwa Ushindani Wa Kutoa Pesa Za Rushwa Kwa Wapiga Kura Wao.

By: Shuhuda Aliyekuwepo.
 
Nasikia harufu mbaya CHUKI/ unafiki dhidi ya ZITTO . Kuna pia wale wengine wanaozurura Huku kanda ya ziwa wakijiita kuwa wao ni wabunge wa KITAIFA wakijenga CHAMA, wao unawaweka kundi gani mkuu
 
Kama umesema Wanazurura Kanda Ya Ziwa mi nitawaweka kundi gani tofauti na Wazururaji? Cha Msingi toa taarifa polisi wakamatwe.
 
Mleta mada umetiririka, wala haichoshi kusoma nimeshtuka tu nimefika mwisho, big up kamanda nimekupata vya kutosha.
 
Nasikia harufu mbaya CHUKI/ unafiki dhidi ya ZITTO . Kuna pia wale wengine wanaozurura Huku kanda ya ziwa wakijiita kuwa wao ni wabunge wa KITAIFA wakijenga CHAMA, wao unawaweka kundi gani mkuu

huwezi kusikia harufu hata siku moja kwa sababu haina sauti.
 
Atang'okaje wakati hana nafasi yoyote hapo?

mkuu kack asante kwa habari hii
habari yako si mpya sana haya yote yalikuwa yakifahamika isipokuwa wagombea walikuwa zaidi hayo isipokuwa walipata kura chache issue pekee ambayo tulikuwa hatuijui ni hiyo ya zzk kujiusisha na rushwa. Ebu tupe hali halisi ya jimbo la kighoma kaskazini kisiasa ikoje?? kuna bwana mmoja nafikiri ni mwalim kutoka chadema je ataweza kulikomboa jimbo hilo?? kwanini unasema zitto hana nafasi kighoma mjini wakati mgombea wake aliomchomeka mwaka 2010 alikosa ubunge kwa kura chache na wengine wanaamini alishinda isipokua aliibiwa ?
 
Kwa nini aende Kigoma Mjini wakati Kaskazini kaishindwa??
 
mkuu kack asante kwa habari hii
habari yako si mpya sana haya yote yalikuwa yakifahamika isipokuwa wagombea walikuwa zaidi hayo isipokuwa walipata kura chache issue pekee ambayo tulikuwa hatuijui ni hiyo ya zzk kujiusisha na rushwa. Ebu tupe hali halisi ya jimbo la kighoma kaskazini kisiasa ikoje?? kuna bwana mmoja nafikiri ni mwalim kutoka chadema je ataweza kulikomboa jimbo hilo?? kwanini unasema zitto hana nafasi kighoma mjini wakati mgombea wake aliomchomeka mwaka 2010 alikosa ubunge kwa kura chache na wengine wanaamini alishinda isipokua aliibiwa ?

Kigoma Kaskazini CDM ina nguvu kuliko CCM, ACT haipo kabisa japokua kuna Dr. Mmoja anataka kujitosa kupitia ACT, Wananchi wengi hawajapendezwa na kitendo cha Peter Serukamba kugombea huko + populality ya CDM - Ushindi. Pia watia nia CDM wana uwezo mkubwa Wa kujenga hoja.

Kigoma mjini CCM wana nafasi kubwa kuliko vyama vingine. ACT inashabikiwa na Vijana na Wazee wachache kwenye vijiwe vya kahawa baasi!! hawa ndo waongeaji kama K.a.s.u.ku kuanzia asubuhi mpaka jioni.

UKAWA watakuwa wa pili kwa kura.
 
Back
Top Bottom