barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,865
Hili la Vietnam na Halotel si la kuacha kimya kimya bila kujadili na kuweka tahadhari kwa vyombo vya usalama na uweledi wa ofisi ya Mashauriano ya kigeni chini ya kitengo cha "Chief of Protocol".
Tuliwahi kulijadili hapa,japo kuna watu walitubeza na kutukashifu,lakini lengo lilikuwa kukuza mjadala na kuwakumbusha watu majukumu yao.Unaweza kupitia hapa ili kujikumbusha Alichokifanya Rais wakati wa kumsindikiza PM wa Ethiopia ni "aibu" kiitifaki, wahusika msaidieni
Dunia na siasa zake zimebadilika sana.Kwa sasa mataifa mengi ya dunia hayachukulii "diplomasia" kama suala la ushirikiano tu katika siasa na mambo kama hayo,sasa wana hiyo kitu wanaita "diploamasia ya uchumi na ujasusi".Nchi ipo tayari kutumia namna zozote kuwawezesha wananchi wake kiuchumi na kibiashara ili mradi tu,waupoke uchumi wa mahali pengine na kuuleta katika nchi yao.
Si ajabu kwa sasa,mataifa mengi yanatuma mabalozi na wanadiplomasia katika nchi nyingine ambao ni "majasusi wa kiuchumi" na "wajasialiamali" wanaotumia "mbinu" safi na chafu kufaidisha wafanyabiashara wa nchi zao na serikali zao.Hili la Halotel (kampuni tanzu ya Viatel ambayo ni mali ya jeshi la Vietnam) liwe fundisho kwetu kama raia na serikali kwa ujumla.
Ukitaka kujua mbinu na njia ambazo Halotel walijipenyeza na "vifaa" vyao ambavyo baadae TCRA walikuja kugundua kuwa "vimeingia" kwa njia ya panya,lazima uanze kungalia picha za siku ya ujio wa Rais wa Vietnam na ujumbe wake ambapo baadhi ya taratibu za kiitifaki na kidiplomasia zilivyokiukwa.
Ukiukwaji huu ulileta mashaka sana toka siku ya tukio na hata baada ya tukio na namna ambavyo kitengo cha protokali kilivyolala usingizi kufuatatilia "majasusi wa diplomasia ya uchumi" walivyotumia mwanya huo kuingia kwa njia za panya.Itifaki na taratibu za kidiplomasia zinapolegea,basi kuna watu wanaotumia mwanya huo kujifaidisha.
Kwanza tunapaswa kujua kuwa kuna taratibu mahususi za ukaguzi wa ndege na msafara wa kiongozi anayeingia ndani ya nchi,ili kuepuka kuingiza magendo,silaha na mambo mengine bila uangalizi wa "custom" au vyombo vya usalama.
Mambo ambayo huzingatiwa ni "Weapons and Diplomatic protection".Hapa msafara wa kiongozi anayekuja ni lazima utoe taarifa kwa nchi mwenyeji,idadi ya maafisa usalama watakaokuja na silaha za kumlinda kiongozi wao,hapa kuna ku-declare type of the weapon,serial number,Caliber of the weapan na number of rounds of ammnunation.Silaha hizi hukaguliwa na kuthibitishwa na kitengo cha usalama mara tu ya ndege ya kiongozi mgeni kutua na kabla hata ya msafara kuondoka Airport kuelekea katika ziara ndani ya nchi mwenyeji.
Jambo lingine ambalo ujio wa ugeni hupaswa kupatiwa kwa utaratibu wa kidiplomaisia ni "Radio Frequencies".Hii na kwa ajili ya maafisa usalama kupata mawimbi ya kuwasiliana wawapo katika msafara na shughuli zote wakati wakiwa katika nchi mwenyeji.Hii ni kwa ajili ya portable radio,Walkie Talkie Radio na Base Radio.Frequencies hizi kwa kawaida hutolewa ili mawasiliano yao yasiingiliane na wengine na waweze kufanikisha kazi zao za kiusalama.
Kingine ni "Importing equipment for official use".Katika kipengere hiki,kinaeleza kuwa "When an individual or delegation with a Head of state/Gvt inter the country without diplomatic status and is bringing with them a commercial equipment not covered under their personal exemption,those items should be MANIFESTED, items include vehicles,Communication media equipments,Cash,Checks of money above required amount,Medical equipments (Except Oxygen tanks,diabetic kits,wheelchairs etc).Hivi vyote lazima vikaguliwe na watu wa "Custom".
Ukiingalia picha niliyoambatanisha,utaona kuwa kitengo cha Itifaki na wote wanaohusika "walizembea" jambo dogo,ambalo wenzetu ambao wapo katika "diplomasia ya uchumi wa kijasusi" walilitumia.Ugeni ule wa Rais wa Vietnam ulikuja na ujumbe wa wafanyabiashara wengi sana ambao hawakuwa na hadhi ya "kidiplomasia" lakini sbb pengine waliusoma "udhaifu" wa itifaki yetu kabla,basi waliratibu mambo mengi kiustadi ili kupenyeza mambo yao kwa njia za mgongo wa diplomasia.
Moja ya wafanyabiashara waliokuja na Rais wa Vietnam usiku ule,walikuwa ni mabosi wa Viatel (Halotel Tanzania),ambao walipokewa na wafanyakazi wao waliopo Tanzania,ambao wengine ndio hao walioshitakiwa kwa kuingiza vifaa vya kielectronic bila "custom" wala taarifa ya TCRA.
Ujio wa magari ya HALOTEL TANZANIA,kuingia tu uwanjani kwa mgongo wa kubeba mizigo yenye hadhi ya "kidiplomasia" ulipaswa kuwastua watu wetu wa itifaki na wale wa usalama.Kwamba mabox makubwa makubwa,masanduku makubwa yenye upana wa futi nne hadi tano kushuka katika ndege na ugeni wa watu wanaokuja kukaa siku mbili katika ziara yanakuwa yamebeba nini?Hata hili watu wetu hawakustuka.
Katika vikao na "Advance Team" ya watu wa Vietnam,watu wetu wa itifaki walipaswa kujiridhisha kuwa magari yatakayotumika katika kubeba mizigo ya ugeni wa Rais,yanahakikiwa na kuhakikisha ndiyo yale yanaingia uwanjani siku ya ugeni husika.Inajulika kuwa katika ugeni kama huo,kunakuwa na "Expediting Processing and Clearence upon VIP arrival",ambapo mizigo na passport za VIP zinapelekwa harakaharaka kwa heshima ya ugeni.
"Expediting" hii ndio imekuwa inatumiwa vibaya na majasusi wa kiuchumi,pale ambapo hupenyeza mizigo na magendo yao kuingia katika nchi husika kama tu kitengo cha protocol na usalama wa nchi mwenyeji havipo makini.Kwa aina ya maitambo kama "Gateway" iliyokamatwa na TCRA kwa HALOTEL TANZANIA,ni dhahiri kuwa mahali pa kuanzia uchunguzi huu,ni siku jopo la wafanyabishara wengi wa Vietnam walipoambatana na Rais wao katika ndege moja kuingia Tanzania.
Hali hii ilipunguza umakini na wote wakapata huduma ya "Expediting" wakati wengine hawakuwa na hadhi ya kidiplomasia.Nafasi hii na kwa namna Halotel ilivyotumia magari zaidi ya sita kuingia na kubeba "mizigo" yao ya "kidiplomasia",inatukumbusha namna tunavyopaswa kuona umuhimu wa "Chief of Protocol" na vyombo vyetu kuwa makini.Na kwa sisi "wadadisi pori",tunahitimisha kwa kusema,hii ndio moja ya njia ambayo HALOTEL waliingiaza vifaa vyao vya kielectronic bila taarifa za "Custom" na TCRA.
Muda ambao ndege iliingia ilikuwa ni usiku,lakini magari ya kampuni ya simu kuingia na kutumika kubeba "mizigo" toka kwenye hold ya ndege,ilipaswa kuweka "alarm" yenye kuasharia kuwa jicho la tatu linapaswa kutumika.Yaliyotokea yametokea,tujifunze kuanzia hapa.
Ikumbukwe jambo hili la kujipenyeza na "magendo" katika misafara ya wakubwa si geni sana,hata hapa kwetu Tanzania lilipata kuwepo/lipo .Tofauti iliyopo ni kuwa,Tanzania watu wengi,wakiwemo waandishi wa habari waliokuwa wakiambatana na misafara kama hii ya Rais,Makamu au Waziri mkuu,walikuwa wakipitisha suti za Ulaya na "dona" kama punda wa wazee wa kazi(Hili hata @Pasco wa Jf aliwahi kulieleza humu kwa kifupi),wakati wenzetu wanaingiza mitaji na uchumi wa nchi zao kwa faida ya Taifa zima.
Nihitimishe kwa kusema,pongezi kwa TCRA kwa kuwagundua hawa "majasusi wa diplomasia ya uchumi",ila angalizo liwe kwa kitengo cha itifaki katika kukumbuka na kutambua wajibu na taratibu za kidiplomasia katika dunia hii yenye ushindani wa diplomasia ya uchumi.Lengo ni moja,kumsaidia Rais wetu mpendwa kufikia Tanzania ya viwanda.
#Jf [HASHTAG]#BeTheFirstToKnow[/HASHTAG]