MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,255
- 8,027
Kwa hatua ulipofikia upinzani kukamata majiji yote makuu ispokua jiji moja tu nchini hii ni dalili tosha tu kwamba chama tawala ndio kinaondoka hivyo, nadharia inasema kwamba mapinduzi yeyote huanzia kwenye miji mikubwa penye mirundikano ya watu wengi na kusambaa vijijini.
Najaribu kuangalia mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu jinsi serikali chini ya CCM ilivyowadhibiti wapinzani kufanya mikutano kwa kuzuia viwanja vya wazi vilivyokua chini ya mamlaka zao, natolea mfano wa viwanja vya Jangwani jinsi UKAWA walivyokua wakizungushwa, na istoshe kulikua na ukiritimba mkubwa kwenye ubandikaji wa mabango ya wagombea wa UKAWA tofauti na CCM. Lakini mfano leo jiji la DSM liko chini ya UKAWA na madiwani wao walio wengi chini ya mameya wao ndio wenye mamlaka ya matumizi ya viwanja vya wazi na maeneo ya kuweka mabango, sasa hapa CCM walizoea kujimegea leo hii watapitia wapi?
Kazi waliyobakia nayo UKAWA ni kumalizia kule vijijini na kurudisha lile jiji moja tu walilolipoteza mwaka jana, ni kujipanga kuonesha utofauti wao na wanaCCM ambao walikua wakiendesha majiji hayo tokea Uhuru mpaka sasa hakuna kipya, mapya yanatakiwa kiletwa na vikosi vya kazi vya Upinzani.
Ni wazi kua watawala wa sasa wanajaribu kutumia mbinu lukuki kuwaachia wapinzani vyanzo kiduchu vya mapato ili washindwee kujiendesha wakose cha kuwaambia wananchi lakini bado ukweli utabaki pale pale kua upinzani ukishaingia ndani ya jiji ni ngumu kuondoka na duniani kote ndivyo ilivyo. Chama tawala kushikilia jiji ni ngumu kutokana na uelewa wa watu na mwingiliano wa makabila mbali mbali kutoka sehemu mbali mbali kwa maana ya wagombea kupata uungwaji mkono na pande zote tofauti na sehemu ambayo unakuta kuna mrundikano wa kabila moja na kati ya wagombea wote moja anatoka ndani ya kabila hilo hali inayosababisha aungwe mkono na kabila lake hata kama hana uwezo.
Tunaambiwa siasa ni mpaka 2020 lakini kumdhibiti mpinzani ambaye ana majiji yote kwa 99% ni ngumu sana, kwanza hayo majiji yote na halmashauri kuna viongozi kama wabunge,madiwani au mameya na wenyeviti wa halmashauri ambao kwa hakika hukutana kwa pamoja na kupanga mikakati zaidi ya kuiondoa CCM madarakani.Tukumbuke kua hakuna anayependa kuachia nafasi yake ya uongozi kirahisi, hivyo nao hujipanga zaidi kuendelea kuikabili CCM.