Hivi nchi hii ni Plastiki pekee ndo zinaharibu Mazingira?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,493
8,728
Hawa NEMC naona wanakomaa mno na mifuko ya plastiki, kwani mazingira nchi hii yanaharibiwa na mifuko ya plastiki pekee?

Vipi ukataji miti hovyo? Vipi yale Makundi ya mifugo yanayo hama hama?

Yaani sehmu ya wao kutokea ni kwenye Mifuko ya plastiki tu, kwingine hapana.
 
Kuna kundi la wafugaji, nisingependa kutaja kabila lao.. Hawa wanaongoza kwa uharibifu wa mazingira.. Utadhani wana ugomvi na miti.. Wakifika mahali ni mwezi tu panageuka jangwa. Cha ajabu hili tatizo halizungumziwi kabisa.

Na vi ng'ombe vyenyewe wanafuga vimekomaa komaa tu, huwezi jua ni ndama au ng'ombe mkubwa.
 
Sure
Kwenye plastic huenda ndo kuna rushwa ya chapchap. Halafu ukigusa makundi ya mifugo yanayo hamahama, inaweza kukupotezea kazi haraka sana. NEMC wako makini sana, wanajua wanachofanya.
 
Kuna kundi la wafugaji, nisingependa kutaja kabila lao.. Hawa wanaongoza kwa uharibifu wa mazingira.. Utadhani wana ugomvi na miti.. Wakifika mahali ni mwezi tu panageuka jangwa. Cha ajabu hili tatizo halizungumziwi kabisa.

Na vi ng'ombe vyenyewe wanafuga vimekomaa komaa tu, huwezi jua ni ndama au ng'ombe mkubwa.
Sukuma waah!
 
Wanaona kwenye plastic ndiko rahisi kupiga hela au kulinda viwanda vya vifungashio vya vigogo
 
Back
Top Bottom