tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,539
- 21,567
Mara tu Rais Magufuli alipoapishwa kuwa rais wa tano wa Tanzania alianza kutembelea ofisi na taasisi mbalimbali za serikali kwa mtindo wa kushtukiza huku akiwasimamisha kazi baadhi ya watendaji na kutoa maagizo kadhaa kwa watendaji hao. Aidha, Rais alipomuapisha Waziri Mkuu, kiongozi huyo mpya naye akaiga mtindo wa bosi wake?.kila kukicha yu kiguu na njia akivizia taasisi na mashirika kadhaa ya serikali kwa mtindo wa KUSHTUKIZA. Mawaziri, makatibu, wakuu wa mikoa na wilaya nao hawajaachwa nyuma kwa kushtukiza. Hii sasa imekuwa ndiyo staili mpya ya uongozi?.kwamba ili uonekane unafanya kazi sharti ushtukize watu na kuwakurupua kwa lengo la kutafuta kiki na uhalali wa nafasi unayoshika!
Sio nia yangu kupinga aina hii ya utendaji kwa kuwa kila kiongozi ana mbinu zake za kujitngaza kwa wananchi, ila natoa angalizo kwamba sheria na tataratibu za kiuongozi na usimamizi wa mambo ya serikali sharti zifuatwe. Hatuwezi kuendesha nchi kienyeji kana kwamba sheria hazipo. Kabla sijaenda mbele naomba turejee nyuma hadi kwenye meli ya wachina. Meli ile ilikamatwa kwa kukurupuka lakini mwisho wa siku serikali ilishindwa kesi na kulazimika kulipa mamilioni ya shilingi za walipa kodi kama fidia ya samaki waliopotea na meli iliyoharibika baada ya kuegeshwa baharini kwa muda mrefu.
Tutumie uzoefu huu kama mwalimu kwa lengo la kuepuka kuja kuiingiza nchi katika kesi zisizokuwa na msingi na hivyo kupoteza fedha za watanzania. Hawa watumishi wa umma wanaosimamishwa kazi ovyo bila kufuata taratibu, kanuni na sheria za utumishi watakuja kuisababishia serikali hasara ambayo kila mtanzania atabaki kinywa wazi. Kusema hivi sio kwamba nawatetea mafisadi bali nasisitiza kwamba sheria na taratibu za utumishi sharti zifuatwe katika kumsimamisha au kumuachisha mtumishi wa umma kazi. Nasema haya nikiwa na kumbukumbu kwamba serikali hushinwa 99% ya kesi kutokana na kuchukua maamuzi ya kukurupuka.
Naomba turejee kwenye dira ya uongozi na utawala bora pasipo kumuonea mtu wala kumtetea muovu au fisadi yeyote anayetaka kuliangamiza taifa. Hivi mnadhani ni kwanini fisadi Chenge na mafisadi wenzake hawakamtwi na kufikishwa mahakamani kwa ufisadi wao wanaoufanya kila kukicha? Tatizo ni ukosefu wa USHAHIDI usioacha shaka. Unaweza ukaona kabisa mtu fulani ni fisadi lililokubuhu lakini ukakosa ushahidi wa kumfikisha mahakamani au ukampeleka mahakamani na akashinda kesi misa ya kwanza. Hii ndio sababu watu kama Zombe na Prof Mahalu walishinda kesi zao saa 1 asubuhi licha ya kwamba tuhuma zao zilikuwa wazi kabisa.
Hivyo ndugu zangu, tuache kuchukua maamuzi ya kukurupuka tusije kuiingiza nchi katika hasara inayoweza kuepukika. Sheria na taratibu lazima zifuatwe kabla ya kuchukua maamuzi kishabiki, huku ukishangiliwa na wananchi ambao wengi wao ni mbumbumbu na wasiojua sheria.
:yield: