Hivi nape amekuwa msemaji wa ccm na chadema?????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nape amekuwa msemaji wa ccm na chadema??????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jolebatawi, Oct 30, 2012.

 1. Jolebatawi

  Jolebatawi JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Napenda kuyafuatilia matamko mbalimbali ya kisiasa yanayotolewa na ndugu NAPE NNAUYE,,Nashangazwa sana na mtindo wake wa kutoa matamko mbalimbali siku hizi na kwenye hayo matamko ni lazima amtupie kijembe katibu mkuu wa chadema DR SLAA.Kwa mfano jana alipokuwa anaelezea tathmini ya uchaguzi mdogo wa madiwani ulioisha kwa kusema kuwa namshauri babu yangu Dr slaa kuachana na siasa na vijembe vingine vingi baada ya ccm kuibuka na kata 22,chadema kutoka kata 2 za awali hadi kuchukua kata 5, TLP kata 1 na CUF kata 1.
  Kimsingi namshauri NAPE atambue kuwa japo hizo kata wamezipata lakini kiukweli ni kwamba ccm kwa sasa kina hali mbaya kisiasa na inapumulia mashine,,pili NAPE atambue kuwa kazi yake ni uenezi ndani ya ccm,,na kama hivyo ndivyo chama chake kilichoshindwa kutokomeza rushwa ndani ya chama na serikal pamoja na kushindwa kusimamia maazimio waliyoyaanzisha ya kuvuana magamba anapata wapi ujasiri wa kupoteza muda kujipima ubavu wake kwa DR SLAA ambaye ni kiongozi machachari na mwenye misimamo isiyoyumba?
  Mwisho namnatahadharisha NAPE kwamba hana ubavu hata kidogo wa kushindana na DR SLAA,na anavyofanya hivyo ni sawa na mtu mzima anayejivua nguo na kubaki uchi na kuzidi kuipaisha chadema kwa sababu itaonekana kuwa DR SLAA anamnyima usingizi NAPE!!
  MAONI YENU NI MUHIM WADAU ILI TUMSHAURI HUYU BWANA MDOGO ANAYEJIFUNZA SIASA ZA NCHI HII!!!*

   
Loading...