Hivi nani ni Daktari Mkuu wa Dr. Kikwete?

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
1,881
2,000
Natambua kwamba awali daktari mkuu (Chief Physician to the President) wa Kikwete alikuwa mwana UWT Dr. Peter Mfisi, huku Dr. Mohamed Janabi (ambaye alipata uprofesa ulioleta maswali kadhaa, kupitia chuo fulani cha Marekani) akiwa kama daktari msaidizi. Lakini ghafla bin vuu Dr. Janabi akaonekana kushika usukani, huku Mfisi kama akiwekwa kando. Prof. Janabi akaanza kujitambulisha kama daktari mkuu wa Rais. Na sasa Dr. Janabi (Wewe muite Prof.) amepewa ukurugenzi wa JKCI.

Nauliza kitu gani kilitokea kwa Dr. Mfisi? Mimi sio daktari lakini nasikia Prof. sio mzuri sana sawasawa na uprofesa wake, ila ni mtu wa lobbying kwa saana na mpenzi wa kupiga picha.

Kuna thread ya Dr. Mfisi akitoa taarifa ya ugonjwa wa Dr. Kikwete (akisaidiwa na Dr. Janabi)
Taarifa ya daktari wa rais

Lakini pia kuna press release ya ikulu ya Dr. Janabi akitambulishwa amekuwa Professor!!!
Daktari wa rais Kikwete apanda cheo
_MG_2860.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom