Hivi, nani anatakiwa kuchinja nyama?

Yeyote anaweza chinja tu kwetu sisi wakristo hatuna shida hata kama kanyongwa sisi twala. You know what we do initially chakula ni cha mpishi baada ya mimi kupewa na kibadili na kuwa chakula cha Mungu wa Israeli, Ibrahim, Isaka, n.k. Ukiamin tu hata kama kina sumu ya kufisha hakitakudhuru. Hivyo mimi nawashauri wakristo whatever atakayechinja kikubwa ni wewe kumshirikisha Mungu wako ili akipe baraka na nguvu ili kikupe afya. Tuachane na urgument za kidini hili halitatusaidia zaidi utakuta wachinjaji wanakula bila kufuata kanuni za afya na mwisho wanakufa na hypertension. Tuwe wavumilivu kama kristo alivyovumilia mpaka kufa msalabani.

Jibu la KIROHO. Ubarikiwe sana. waacheni wanaotaka kupakaa damu wapakae sie tule nyama. Ila kabla ya kuila, itakase kwa DAMU YA YESU
 
mkuu nadhani umenielewa. Tangu kuasisiwa kwa udini na jk sasa hivi watu wamefikia kuhoji kila jambo la kijamii linalofanywa na upande mmoja kwa kwa nini na wengine hawahusishwi? Ndo maana nimeuliza wanasheria, wanajamii na watu wa mifugo. Vinginevyo ningeuliza tu kwa ni waislamu ndo wachinjaji? Au ningesema nachukia nyama inayochinjwa na waislamu!

Mkuu tunakuelewa vizuri kero yako, lakini wakati mwingine ni vema tukubali kuendelea na utamaduni ulio zoeleka, mbona tunakubaliana nao wanapo funga mahoteli/migahawa ya chakula wakati wa mfungo wa Ramadhani bila ya kujali, kwamba si raia wote ni Waislaam - mwezi mzima unajikuta nawe unafunga wakati wewe ni mkristo!

Sina shaka baadhi ya Waislaam wenye itikadi kali za kidini wakikumbuka hilo labda watajifunza namna ya kuvumilia/kuheshimu dini za watu wengine specifically WAKRISTO.
 
Wakristo walikuwa wanafuata utaratibu huu kwa namna ileile ya kuishi vizuri na wenzao waislamu si unajua tena wakristo hawana hiyana. Vile vitu ambavyo wanakula na wenzao hawakupenda kuwakwaza waliwapelekea waislamu iliwachinje na ili waweze kula wote. Lakini Nguruwe huwa wanachinja wenyewe kwani wenzetu kidinihuwa hawali.
Sasa kama mahusiano yalikuwa mazuri kiasi cha kuita jirani yako akuchinjie kuku au mbuzi ili mle pamoja imekuwaje huu udini wa kubaguana,kuchomeana nyumba za ibada na kashfa? Nani kayaleta hayo ghafla namna hii? Ndugu wanapogombana haraka sana wanamtafuta mchochezi wao na kumu eliminate.Waislam na Wakristo ni ndugu toka zamani wakiishi kwa kushirikiana (hata kuchinja kuku)hivyo ni vema sasa hivi wakamjua ni nani anayewagombanisha?kwa sababu mwanao yu mahututi na mwenye usafiri jirani yako mmegombana kwa udini jee yule aliyechochea udini huo mtamuona?
 
shida hapa nikua ukristo haufundishi njia sahii za uchinjaji bali wayahudi na waisilamu wanafundishwa
 
Hakuna sehemu kwe kolani kwamba mkristu akichinja basi mslam asile.

Mwana mpotevu kwe baibo hakuchinjiwa ng'ombe na mslam.
 
Hakuna sehemu kwe kolani kwamba mkristu akichinja basi mslam asile.

Mwana mpotevu kwe baibo hakuchinjiwa ng'ombe na mslam.
kwao ni haramu kula mnyama aliyechinjwa na mkristo...cha kushangaza wakristo wenyewe hawana tatizo kula mnyama aliyechinjwa kwa kuelekezwa kibla...kuna kitu cha kujifunza hapa...
 
uislamu ni dini yenye utaratibu kwa kila jambo. Hivyo kwa dini ambazo hazina utaratibu, mtatusamehe. Simply hatuli nyama zilizo chinjwa na wasio kua waislamu kwa sababu kwetu nyama hizo ni vibudu kwa kua zimechinjwa bila kuomba idhini ya muumba.
 
Tunakula nyati, anachinjwa? Ili uweze kumchinja inabidi umpige risasi ndipo uwahi kumchinja na wakati mwingine unamkuta amekufa. Nguruwe inabidi umpoteze fahamu ili uweze kumchinja. Chakula kikiandaliwa na mwislamu kuna taratibu inabidi zifuatwe za uchinjaji na mtu yeyote anakula. Mkristo anapochinja kuna utaratibu anaufuata na mtu yeyote anaruhusiwa kula, ila mkristo kabla ya kula kitu anatakiwa abariki chakula pale najisi yeyote inatoka hata kwa mwislam akibariki anakuwa hana tatizo, ila tatizo ni mafundisho ya viongozi wa dini wanashindwa kutoa elimu ya kutosha kwa waumini wao na baadhi yao ni tatizo wanahubiri chuki na bora viongozi wetu wa dini wakawa na elimu za dini na zakijamii kuliko kuwa na kiongozi shule ndogo anaongoza watu wenye uelewa mkubwa halafu anafanya mambo ya kuwagawa wa Tz.
 
Kama shida ya Waislamu ni kuchinja tu basi tutawapelekea na KITIMOTO wawe wanatuchinjia.
 
Tunakula nyati, anachinjwa? Ili uweze kumchinja inabidi umpige risasi ndipo uwahi kumchinja na wakati mwingine unamkuta amekufa. Nguruwe inabidi umpoteze fahamu ili uweze kumchinja. Chakula kikiandaliwa na mwislamu kuna taratibu inabidi zifuatwe za uchinjaji na mtu yeyote anakula. Mkristo anapochinja kuna utaratibu anaufuata na mtu yeyote anaruhusiwa kula, ila mkristo kabla ya kula kitu anatakiwa abariki chakula pale najisi yeyote inatoka hata kwa mwislam akibariki anakuwa hana tatizo, ila tatizo ni mafundisho ya viongozi wa dini wanashindwa kutoa elimu ya kutosha kwa waumini wao na baadhi yao ni tatizo wanahubiri chuki na bora viongozi wetu wa dini wakawa na elimu za dini na zakijamii kuliko kuwa na kiongozi shule ndogo anaongoza watu wenye uelewa mkubwa halafu anafanya mambo ya kuwagawa wa Tz.

Wacha utani wewe!!

Unaweza kumuwahi nyati kabla hafa umchinje!!! hujitaki!!??
 
kuchinja mnyama ambaye ni halali ktk uislam ni sehemu ya ibada, hivyo jambo hili huwezi kulitenganisha na dini yao. kwa wakristo tendo la kuchinja pia nao ni ibada huwezi kulitenganisha na dini pia. marastafari kuchinja hakutakiwi kabisa kwa mujibu wa imani yao. sasa ktk makundi haya matatu. MUISLAM akichinja mkristo na baadhi ya rastafarian watakula, ila MKRISTO akichinja muislam hatakula . hivyo jamii yetu imeishi kwa kuvumiliana , kuheshimiana kwa miaka mingi. bila kuweka choyo ndani yake. jamii yetu imempa kisu MUISLAM ili achinje tule wote.[ haikatazwi wewe kuchinja japo si muislam, ila kama muislam akiwa ni miongoni mwa walaji wako mjulishe] kiserikali kwenye hafla zote . kwenye machinjio kisu kapewa muislam.
 
Samahani kidogo wadau, hivi KITIMOTO anachinjwa au anauawa?
Anachinjwa Mkuu au nyundo akianguka na kulegea kisu kinamalizia! Na kule kwetu huwa kazi hiyo tunawapa ndugu zetu ktk Adam kwa sababu wanapenda kuchicha, na ili Tusiwakwaze, na ni kama nguruwe wa shughuli tuwe pamoja! Manake huwa swali lao la kwanza kabla ya kula, "Kachinja nani?"
 
uislamu ni dini yenye utaratibu kwa kila jambo. Hivyo kwa dini ambazo hazina utaratibu, mtatusamehe. Simply hatuli nyama zilizo chinjwa na wasio kua waislamu kwa sababu kwetu nyama hizo ni vibudu kwa kua zimechinjwa bila kuomba idhini ya muumba.
Wacha zako hizo za kuleta!Toa ushahidi wa ayat ndani ya Qurani inayo zuia Mkristo asichinje!Si useme tu kuwa mna uchu wa nyama kwa sana!
 
....usungilo....Si kweli kuwa kwa waislamu anayeruhusiwa kuchinja ni shehe tu. Ninachofahamu kila muislamu mwanaume anayefahamu utaratibu wa kuchinjia kuchinja. Nikweli kuchinja kunaambatana na maombi/sala kwa ajili ya yule mnyama anayechinjwa. Katika uislamu kuna hata exception kuwa inapotokea kwenye mazingira ambayo hakuna muislamu mwanaume anayejua taratibu za kuchinja lakini kuna mwanamke anayefahamu taratibu za kuchinja basi anaweza kufanya hivyo. Hili ni suala la kiimani zaidi kwani mapokeo yanasema hivyo. Ulichouliza kinaweza ku-apply kweli kwenye jamii isiyokuwa na waislamu ambako bado watu wanachinja kwa utaratibu waliojiwekea. So kutegemea padri, askofu au mchungaji kuchinja mnyama kisha hiyo nyama akiliwa na waumini wa dini nyingine kwa mtazamo wangu nadhani itakuwa ngumu na hasa kwa nchi kama Tz ambayo nijuavyo si ya kidini kama zilivyo zingine ambazo hata katiba inaeleza wazi kuwa nchi husika inafata imani ya dini fulani.

Na je, mapokeo yanasemaje kuhusu kuchinja binadamu? Sala ni ile ile?
 
Wanyama wengi wanachinjwa kwa Machine siku hizi .... Labda kama ni swala la ajira hapa kwetu / ujasilia mali .....
 
Back
Top Bottom