Hivi, nani anatakiwa kuchinja nyama?

Watanzania hatuja hamia digital ki fikra bado tupo analogy.Modern abattoir zinatumia mashine wala hilo swala la dini halipo.Tujiangalie tutazame mbali zaidi hili swala lisitufikishe mbali kiasi tukasahau maswala ya muhimu kwa mustakabal wa taifa letu.
 
MImi nauliza hivi, nyie watu wa ukoo wa kuchinja, kama nina mbuzi wangu, nikamuona Ustaadh Fanyafanya ambaye ndio imamu wa msikiti wa jirani anakatiza na kanzu yake na videvu kama beberu, nikamuita aje achinje huyo mbuzi, akikataa nikashitaki wapi?
 
Hii ishu ina migogo baadhi ya maeneo na watu wanataka kuanza kugoma kununua nyama. Niliwahi kutana nayo na kwenye maoni ya katiba mpya. Kisheria na kijamii nani wanaruhusiwa kuchinja mifugo machinjioni? Tumezoea mashehe ndo wanachinja, je wachungaji/wainjilisti na mapadre/makatekista wanaruhusiwa kuchinja? Kama ndio kwa nini haikuwekwa zamu? Kama hapana kwa nini iwe hivyo? Kuna ndugu zangu wauza nyama na wengine ni walokole wamenifuata na kuniuliza kuhusu hilo, ukichukulia nina kaelimu ka kukariri wakajua najua kila kitu. Naomba wanasheria, wanajamii, mabwana mifugo na wengine wenye ujuzi wa hili jambo mnijuze ili nisitoe ufafanuzi wa kimgogoro.

Sio kuchinja nyama, ni kuchinja mnyama.
 
Mgogoro kuhusu haki ya kuchinja kwenye mabucha limeshindikana kwa sababu kuna baadhi ya watu wameona hawatendewi haki. Watu hawa walikuwa wamewapa wenzao haki ya kuchinja kwa ajili tu ya ustaarabu; lakini baada ya kuona 'ustaarabu' wao unageuzwa na kufanywa ni sheria ndipo walipoamua kuidai haki yao.
Nashauri yafuatayo: kwa kuwa nchi yetu siyo ya kidini bali watu wake wana dini zao;
na kwa kuwa watu hawabaguliwi kwa dini (imani) zao;
kwa hiyo basi, wote wapewe haki ya kuchinja kwenye hayo machinjio na wauze nyama kwenye mabucha yao.
Kwa wale wenye mashaka ya kula vilivyochinjwa na wenye imani tofauti na yao - nashauri mabucha yao yaandikwe 'HALAL' ili kiwe ni kitambulisho cha wapi wanunue na wapi wasinunue. Huko ughaibuni, wale wanaohofia kula visivyochinjwa kwa imani yao huenda kwenye mabucha yaliyoandikwa 'HALA' na hakuna ugomvi wowote. Pia wale ambao ni wa imani tofauti ambao hawaoni kikwazo kula kilichochinjwa na wa imani nyingine huamua kununua watakapo.

Kwa hiyo, serikali itoe haki kwa wananchi wote kuchinja kwenye machinjio nchini na kuuza nyama mabuchani. Wale wanaotaka kula vilivyochinjwa kwa imani yao, mabucha yao waandike 'HALAL'.
 
Binafsi naamini akinja mwenye imani ya kiislam nakula na akinja mkristo nakula. LAKINI ISIWE SHERIA KWAMBA LAZIMA ACHINJE MWISLAAM!
 
Mimi nadhani suruhisho hapa ni kuruhusu woote wachinje na waweke label, hii imechinjwa na Islam au hii imechinjwa na mkristo! Kwakuwa kwa mkristo pia anakatazwa kula nyama iliyotolewa sadaka! Yaani kwenye Biblia wamekataza kula nyama iliyotolewa sadaka na Damu! Kihalali nyama ikichinjwa na muislam mkristo anaye fuata neno kikamilifu anastahili asile! Mambo ya imani ni magumu!
 
Mi nadhani ifike mahali achinje yeyote Kwann kila mtu Ana Imani yake wengine Huku wrap again na wanna kila bila complication minimum Imani ziheshimiwe tu
 
mtu yeyote achinje tu kwani hakuna popote panapotamka juu ya kuchinja katika sheria zetu za nchi na hata ktk katiba. Halafu mi nashangaa sana hvi huu udini umeaza lini wa kubaguana na kufanya masuala ya dini fulani kuwa sheria?
 
Mgogoro kuhusu haki ya kuchinja kwenye mabucha limeshindikana kwa sababu kuna baadhi ya watu wameona hawatendewi haki. Watu hawa walikuwa wamewapa wenzao haki ya kuchinja kwa ajili tu ya ustaarabu; lakini baada ya kuona 'ustaarabu' wao unageuzwa na kufanywa ni sheria ndipo walipoamua kuidai haki yao.
Nashauri yafuatayo: kwa kuwa nchi yetu siyo ya kidini bali watu wake wana dini zao;
na kwa kuwa watu hawabaguliwi kwa dini (imani) zao;
kwa hiyo basi, wote wapewe haki ya kuchinja kwenye hayo machinjio na wauze nyama kwenye mabucha yao.
Kwa wale wenye mashaka ya kula vilivyochinjwa na wenye imani tofauti na yao - nashauri mabucha yao yaandikwe 'HALAL' ili kiwe ni kitambulisho cha wapi wanunue na wapi wasinunue. Huko ughaibuni, wale wanaohofia kula visivyochinjwa kwa imani yao huenda kwenye mabucha yaliyoandikwa 'HALA' na hakuna ugomvi wowote. Pia wale ambao ni wa imani tofauti ambao hawaoni kikwazo kula kilichochinjwa na wa imani nyingine huamua kununua watakapo.

Kwa hiyo, serikali itoe haki kwa wananchi wote kuchinja kwenye machinjio nchini na kuuza nyama mabuchani. Wale wanaotaka kula vilivyochinjwa kwa imani yao, mabucha yao waandike 'HALAL'.
Ushauri wako unafaa katika hili la kuchinja
vp na la weekend (siku za mapumziko)
kuwa za mfumo kristo???
 
Watu wanashindana kuutokomeza uislamu,kwanza walianza huko nje a,ambapo baadhi ya nchi zilipiga marufuku uvaaji wa hijabu mashuleni na mwisho wa siku hata baadhi ya maeneo nyeti ya serikali hizi si ruhusa kwa yeyote kuvaa mavazi yanayonfunika mwili mzima na kubakiza macho tu.

Kama mjuavyo kwa nchi yetu nayo kuwa miongoni mwa nchi zinazopokea mamboleo kila kukicha tukianzia masula ya ushoga ambapo hili kidogo serikali walilipinga.Suala la uchinjaji nalo pia limeonekana kuanza kushabikiwa na baadhi ya watu bila ya kufahamu mletaji wa mjadala huo alikuwa na maana gani?

Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo nchi inavyo-katwa katwa kwa ajenda za kipuuzi na kuwasahaurisha wananchi yale ambayo tulitegemea yangekuwa ni maisha bora.Suala si nani anafaa kuchinja suala ni nani mlaji wa nyama kila siku kuanzia mishikaki barabarani,kuku kwenye mahotel na vibandani,supu na nyama choma kwenye mabaa mijini.

Huko tuendako usije shangaa hata hotel na migahawa itakuwa ni maalum kwa watu wa imani fulani kama ilivyo kwa migahawa ya kichina,kijerumani,kifaransa n.k

Kiukweli Mason in Mason out each & everything is under control may you proceed with the mission.Always you brought new things which are very complicated to judge or decide the way forward.I appriciate your intelligency toward empty minded person,may God bless all including those who are struggling to destroy others and give those empty minded person your glory at least to view the sunset.
 
To be honest tamaduni na vitendo vyake maranyingi zimekuwa zikiweka sheria ambayo kwa namna moja au nyingine tunaheshimu utamaduni kiujumla bila kujalisha imani ila ktk kulinda amani sasa hili la kuchinja mm binafc naona ni tamaduni amabayo imezoeleka na imetijenga kwakulinda amani pacpo utegemezi wa fikra za kidin sasa linapokuja swala la mwisilamu kusema wao wanastahili au mkristo kusema kuwa wao wanastahili tujue lengo ni uvurugaji wa amani kwa kitu kisicho na tija
Sasa mm wito wangu ni kwamba utamaduni uleule uendelee the so called religious politics ziwekwe kando km walishafanya hivyo miaka miailiopita nani leo kafa au mungu wake kamwambia ni haramu!!? Tumeshazoea hivyo na tayri ni tamaduni ktk nchi hii na kwa namna hiyo amani ilidumu
sasa tusilete siasa tuache ujinga wa kuiga tufikirie mambo ya kujenga amani na mwisho kuiletea maendeleo tanzania.
I beg to submit
 
Yeyote mwenye kisu anaweza kuchinja. Mi mbona mke wangu anachinja kuku, bata na hata mbuzi kama siko nyumbani. Visingizio vingine hivi ni vya kujiletea wenyewe kutokana na uroho wetu. Eti jirani akikuchinjia sharti umpelekee shingo,si upuuzi huu? Mi nimempa ruhusa mke wangu kuchinja kile akitakacho. In short, anybody mwenye kushika kisu anaruhusa ya kuchinja, hii haina miiko. Ulaya mashine ndizo zinazochinja mbona utamu wa nyama ni ule ule?
kweli kabisa
 
hili nalo jipu muda ukifika litatumbuliwa!; ushauri wangu > hawa ndugu zetu ktk Adam wana roho ya kuchinja chinja! acheni wachinje ilaha nyama ikifika nyumbani itakaseni kwa jina la Yesu...kwa ajili ya Upendo kama una kuku wako IMA nguruwe muite akuchinjie kisha mzawadie kichwa ya kuku, shjngo, stand aende na yeye akafaidi na family!; huo kwa msaada huo na wewe utabarikiwa! Sema Amen!
 
Back
Top Bottom