Nijuavyo mimi lengo la simu ni mawasiano,Inakuaje kwamba namba ya simu ionekane ni kitu cha siri sana kiasi kwamba watu wengi hukataa kuweka wazi au kupewa mtu mwengine bila ridhaa yake?
Kwani tatizo ni nini?
upigiwe! simu au utumiwe text na watu usio wajua wakutishie maisha ndipo utakao elewa.
Jiulize ni vyema kila mtu ajue unapoishi??
Mkuu Makamee , salama kwanza? umenyimwa namba nini mkuu?? hahaaa, natania tu ....
Sio kitu cha siri ila ni kitu BINAFSI......Tofautisha BINAFSI na SIRI. Ukiifanya namba yako ya simu iwe ya PUBLIC utajuta. watu wana tabia tofaut, wengine hawana malengo mazuri na wengine ni wasumbufu wasio na chembe ya ustaarabu. Ndio maana huwezi kutoa namba hovyo hovyo kwa mtu yoyote tu....
Hebu km si siri weka number yako haapa
Nijibu maswali yafuatayo:
hapo mtaani kwako unapoishi
je una namba ya balozi wako? Ya jirani yako? Ya mchungaji/shehe wako? Doctor yoyote? Ya fundi yoyote?
NAMBA ya simu si kitu kinachotakiwa kiwe siri matumizi mabaya ndio tatizo.