Ponjoro La Kizimkazi
Member
- Jul 1, 2025
- 26
- 41
Wakuu habari za siku mingi? Ni miaka kadhaa sasa imepita tangu niwepo JF kama member. Mara nyingi nimekuwa nikiitumia kusoma nyuzi za wadau tu bila kuweza kuchangia. Na kwa vile sio msikilizaji sana wa radio, wala kusoma magazeti au kuangalia TV (sipendi censored and fake news), JF imekuwa ni chanzo changu cha habari namba moja ambapo wahabarishaji ni members wenyewe (uncensored content directly from the source).
Sasa tangu mwaka huu uanze mambo yamekuwa mengi kutokana na vuguvugu la uchaguzi. Kilichonifanya hasa nirudi tena JF na kuacha mapumziko yangu ya msingi kule Kizimkazi (Uponjoroni), ni kile kiroja cha juzi kutoka kwa yule wakili wa serikali. Yule bwana mpaka sasa naendelea kumtathmini na bado sijafikia conclusion kuhusu yeye. Siku nitakayofanikiwa nitapandisha uzi kumhusu.
Naomba niende moja kwa moja, kwenye lengo la uzi huu. Leo niliona uzi kuhusu kushambuliwa tena mara ya pili kwa mwanamtandao mmoja aitwae Japhet Matarra alias Eng Matarra akiwa wodini ambako alikuwa akitibiwa baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana. Soma hapa. Sidhani kama Matarra ni mwanachama halali wa CHADEMA, ila nafahamu yuko oriented towards CHADEMA na amekuwa critic mkubwa wa serikali kule X (zamani Twitter).
Nimemtumia Matarra kama mfano wa matukio ya karibuni ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miaka isiyopungua 10 against upinzani na hasa hasa CHADEMA. Ni juzi tu Mdude Nyagali alitoweshwa. Soka pia. Dioniz na makada wengineo wengi tu wa CHADEMA. Sasa imekuwa ni jambo la kawaida tu kusikia mwana-CHADEMA ametoweka na maisha yanaendelea. Hapa tulipofikia ni muda sasa tukubali ukweli, kuwa kinachoendelea sasa ni UHALIFU DHIDI YA BINADAMU (pure crimes against humanity) na huku wahanga wakubwa wakiwa ni CHADEMA. Mauaji dhidi ya wayahudi yalipewa jina (HOLOCAUST). Labda idadi sio kubwa kama ile, lakini ukiwa unawatarget watu wale wale lazima ipo namna.
Sijui kama CHADEMA wanazo taarifa kamili, juu ya majina ya wafuasi wao wote ambao waliteswa, kutekwa, kupotezwa na kuuliwa tangu uhalifu huu uanze. Hili jambo limekuwa la muda mrefu sana na mali bila daftari hupotea bila habari.
Ni muda sasa CHADEMA wafungue website ya kudocument uhalifu wote unaoendelea dhidi yao. Picha na taarifa za kila anayefanyiwa na wanaohusika kufanya uhalifu huo ziwekwe huko. Isiishie tu kupost na hashtags. Uhalifu huu uwekwe wazi na siku moja criminals wote wawajibishwe. Oldest website ambayo mpaka leo bado iko online ni ya mwaka 1986, kwa hiyo unaweza kuona nguvu ya mtandao. Na pia kuna Wayback Machine ambayo huarchive websites zote. Kwahiyo taarifa hizi ziwekwe kwenye mtandao ili kuhakikisha haya hayasahauliki. Tuiambie na kuikumbusha dunia na vizazi vyote vijavyo.
Najua ni ngumu kwa initiative hii kuanzishwa kwa waliopo nchini, ila naamini kuna diaspora wengi wa CHADEMA wanaoweza kusaidia kutafuta developers wa kutengeneza na kuhost website hiyo nje ya nchi. Gharama hii ni ndogo sana na chama kinaweza. Mangekimambi is just one individual na ameweza kuwa na a big online platform, CHADEMA inaweza.
Unaweza kutumia google search yangu kwa kubofya hapa kuona baadhi ya ma-Nazi maarufu yaliyokamatwa baada ya vita vya pili vya dunia kutokana na uhalifu wa kivita na kibidanamu na mambo yote ya ovyo waliyowatendea watu ambao waliwaona hawafai.
Tuweke kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
Regards,
Ponjoro La Kizimkazi.