Hivi mnajuaje hili?

Umesoma mada na ukaelewa?
Yawezekana nimeelewa tofauti na ulivyomaanisha. Ila nimesoma na mwisho nikaona umeuliza maswali matatu
1.Sasa kwenye suala la mahusiano watu wamekuwa wakidai kujua kuwa wenza wao wanawapenda,hii inakuwaje?
Unakuwaje na uhakika kwenye hili?

2.Naombeni mniambie huwa mnasema tu au mnakuwa mnajua kabisa kuwa mko sawa?
Au huwa mnaamini tu?

3.Nauliza maana hao hao wanaodai kuwa wanajuwa kuwa wanapendwa huja hapa na malalamiko kedekede kuwa wamesalitiwa au wametendwa,hii siielewi kabisa,hebu nisaidieni tafadhali!

Nilikuwa najaribu kujibu hilo swali la kwanza tu. Samahani kama nimekosea, nimtazamo wangu tu.kwamba uhakika unakuja kwa kuwa vigezo wanavyotumia kupima upendo kwao vimetimizwa. na vigezo kila mtu anavyake.
 

Soma mada yote uelewe!
 
chukulia mfano wako wa mvua NAJUA MVUA INANYESHA ina maana unaiona ndo maana unapata uhakika si ndio
na unaposema ninajua mpenzi wangu ananipenda
kuna uhakika pia kwa sababu uhakika sio lazima uletwe na vitu vinavyoonekana kwa macho tu bali uhakika unaweza kuletwa na hisia na ishara uzionazo
ninajua mpenzi wangu ananipenda wewe mtu wa tatu huwezi kuuona huo upendo bali anaependwa ndo anaeuona ndo maana anapata uhakika na ujasiri wa kusema ninajua mpenzi wangu ananipenda
 
Mkuu mada zako huwa zimetulia sana, hubahatishi
 
Ulichoki quote umekisoma ukakielewa au hauna uwezo wa kuelewa?

Ni wapi nimesema kujua ni kuelewa?
Sija-quote popote isipokuwa nafafanua zaidi ya ulichokiandika kwa mtazamo wangu...usitegemee kuwa sahihi kwa kila ukielewacho.

Unajua maana ya kujua wewe au unaandika tu vitu usivyovijua?
Swali halina msingi wa mada kuu,i drop it.

Dogo kujua kuna maana ya kuwa na uhakika na unaweza kutoa uthibitisho
Kuwa na heshima,maana ya "Dogo" ni mbaya kwa tafsiri niitumiayo mimi na jamii inizungukayo.

Uthibitisho haupingiki lakini ushahidi unapingika
Vyote vyaweza kupingika yategemea na mazingira husika. Uthibitisho wa jambo uhitaji ushahidi timilifu,na ushahidi (evidence) ndiyo huthibitisha jambo.Hivyo ushahidi timilifu(wa kujitosheleza) huaminika katika kuthibitisha jambo.

Lakini unapokwenda mahakamani na kutoa uthibitisho huwezi kupingwa
Mfano unaposema umemuona Juma anaiba na ukatoa Tape ya kuonesha Juma akiiba huo ni uthibitisho na haupingiki
Si kweli. Hata uthibitisho pia waweza kupingwa kwa uthibitisho kinzani. Siku hizi kuna tape za kutengeza kutokana na maendeleo makubwa ya ICT...naweza kutoa tape kuonesha Juma alikuwa sehemu nyingine na mashahidi wakashuhudia hivyo...hapo nitakuwa napinga uthibitisho wako wa awali...kwahiyo kuna mazingira kwamba uthibitisho unapingika pia.

Sasa nakuuliza unaweza kutoa uthibitisho kuwa unapendwa?
ndiyo naweza kutoa. Karibu kwangu, ili uthibitishe mimi na mke wangu tunapendana.Nakualika na kukukaribisha nyumbani (seriously...ni-pm)

Rudia kusoma mada dogo!
Kuniita dogo ni sawa na kunitusi,hupaswi tafadhali.
 
 

umenena vyema sana... mapenz hayana General formula... na hata kama ipo there must be an exception and variations ndy maana bnadam tupo tofaut so as when it come to lov affairs... huyu apenda awe treated hivi na yule vile. period!
 
Mapenzi imani tu na ni mchezo mzuri na mpaya pia ,
 
mi nahisi kitu cha kwanza ili mada hii ifike tamata inabidi tukubaliane indicators za mtu kupendwa,na ikiwa indicstors hizo mhusika (anayependwa) ameonyeshwa na mpenziwe basi ana haki ya kusema fulani ananipenda na ikiwa indicators hizo zimeonyeshwa na zimezidi hapo mhusika(anayependwa) ana haki ya kusema napendwa sana na fulan,kwa mjuibu wangu hizo ni indicator ni kumjali,kumhurumia,kumthamini menzako,kutamani kuwa naye muda wote(pembeni yake)),hutaki kumuona amekasirika aua hana furaha,na mwisho wa na hisia za kimapenzi juu yake

naamini wanaoleta mada hapa huwa wanaona baadhi ya dalili hizi kutoka kwa wapenzi wao thats y husema wanapendwa najua pia mtu ana uwezo wa kufake badhi ya indicators hizi na mtu akifake mhusika(apendwaye ) akimuamini basi hilo halitakuwa kosa lake

#teamrafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…