Hizo ni takwimu za kupika ili mwana wa mfalme asilaumiweKuna muujiza gani ambao mkoa wa Dar ulitumia hadi kuandikisha wananchi zaidi ya asilimia 108 ya watu waliotakiwa kujiandikisha, katika uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba mwaka huu??
Tukumbuke pia tulipewa taarifa na Waziri wa Tamisemi, kabla zoezi hilo halijaongezewa muda wa siku 3 wa kujiandikisha, kuwa mkoa huo katika siku 10 walizopewa za awali kujiandikisha, wenyewe ndiyo ulishika mkia, kwa kuandikisha wakazi wake asilimia 8 pekee!
Sasa ninachojiuliza mkoa huo ulitumia miujiza gani kuandikisha wananchi wake zaidi ya asilimia 108, kwa siku 3 pekee zilizoongezwa kwa uandikishaji??
Tumeona namna ambavyo.uandikishaji huo ulivyodorora sana hata katika siku 3 za nyongeza za uandikishaji huo,ambapo makarani walikuwa wakiuchapa usingizi, katika vituo vya uandikishaji wakiwasubiri hao wananchi wa kuwaandikisha
Tulishuhudia wakuu wa wilaya wakihamasisha kwa kuongea na vipaza Sauti, viwamja vitupu kabisa katika maeneo mbalimbali ya hii hilo
Tunamuomba Rais Magufuli auchungize mkoa huo kwa kuwa tunaamini kabisa, takwimu tulizopewa na Mheshimiwa Jafo ni za kupika za wazi kabisa na tunasmini pia walioandikishwa ili kuweza kuvunja rekodi, ni wale wasiostshili kujiandikisha, kama vile watoto wa shule za msingi za mkoa huo, ambao ni dhahiri hawajafika umri wa kujiandikiisha,, ambao ni miaka 18
Ikumbukwe pia zoezi hilo "lilisusiwa" na wakazi wake wengi sana, kwa kile ambacho wakazi hao wamekieleza kuwa zoezi zima la upigaji kura hapa nchini Tanzania hivi sasa kuwa kama kichekesho!
Kwa kuwa wanajua kuwa watawala wetu "wanalazimisha" ushindi wa kishindo kwa chama cha CCM, hata katika maeneo yale ambayo hawakushinda kabisa!
Tuendelee kiwasihi watawala wetu kuwa wasiwageuze watanzania wote kuwa ni wajinga na wapumbavu ambao hawajui kinachoendelea nchini kwetu hivi sasa,
Ni muhimu sana kuwa kura inayopigwa na mwananchi kwenye sanduku la kura iheshimiwe na kusiwe na uchakachuaji wa kura hizo hata kidogo
Kwa kupewa uhakikisho huo pekee, ndiyo kutaweza kuwarejeshea Imani ya kujiandikisha na hatimaye kuwapigia kura wale viongozi watakaowaona wanafaa katika maeneo husika