Hivi mkoa wa Dar uliwezaje kuvuka lengo na kuandikisha wananchi wengi zaidi ya asilimia 108 ya waliotakiwa kujiandikisha?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,486
30,166
Kuna muujiza gani ambao mkoa wa Dar ulitumia hadi kuandikisha wananchi zaidi ya asilimia 108 ya watu waliotakiwa kujiandikisha, katika uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba mwaka huu??

Tukumbuke pia tulipewa taarifa na Waziri wa Tamisemi, kabla zoezi hilo halijaongezewa muda wa siku 3 wa kujiandikisha, kuwa mkoa huo katika siku 10 walizopewa za awali kujiandikisha, wenyewe ndiyo ulishika mkia, kwa kuandikisha wakazi wake asilimia 8 pekee!

Sasa ninachojiuliza mkoa huo ulitumia miujiza gani kuandikisha wananchi wake zaidi ya asilimia 108, kwa siku 3 pekee zilizoongezwa kwa uandikishaji??

Tumeona namna ambavyo.uandikishaji huo ulivyodorora sana hata katika siku 3 za nyongeza za uandikishaji huo,ambapo makarani walikuwa wakiuchapa usingizi, katika vituo vya uandikishaji wakiwasubiri hao wananchi wa kuwaandikisha

Tulishuhudia wakuu wa wilaya wakihamasisha kwa kuongea na vipaza Sauti, viwamja vitupu kabisa katika maeneo mbalimbali ya hii hilo

Tunamuomba Rais Magufuli auchunguze mkoa huo kwa kuwa tunaamini kabisa, takwimu tulizopewa na Mheshimiwa Jafo ni za kupika za wazi kabisa na tunaamini pia walioandikishwa, ili kuweza kuvunja rekodi, ni wale wasiostshili kujiandikisha, kama vile watoto wa shule za msingi za mkoa huo, ambao ni dhahiri hawajafika umri wa kujiandikiisha,, ambao ni miaka 18

Ikumbukwe pia zoezi hilo "lilisusiwa" na wakazi wake wengi sana, kwa kile ambacho wakazi hao wamekieleza kuwa zoezi zima la upigaji kura hapa nchini Tanzania hivi sasa kuwa kama kichekesho!

Kwa kuwa wanajua kuwa watawala wetu "wanalazimisha" ushindi wa kishindo kwa chama cha CCM, hata katika maeneo yale ambayo hawakushinda kabisa!

Tuendelee kuwasihi watawala wetu kuwa wasiwageuze watanzania wote kuwa ni wajinga na wapumbavu ambao hawajui kinachoendelea nchini kwetu hivi sasa,

Ni muhimu sana kuwa kura inayopigwa na mwananchi kwenye sanduku la kura iheshimiwe na kusiwe na uchakachuaji wa kura hizo hata kidogo, ili kuepuka nchi isiingie kwenye machafuko

Kwa kupewa uhakikisho huo pekee, ndiyo kutaweza kuwarejeshea Imani ya kujiandikisha na hatimaye kuwapigia kura wale viongozi watakaowaona wanafaa katika maeneo husika
 
Futuhiiiii ndio ni FUTUHI.
Wasipoliheshimu sanduku la kura, na kuamini kuwa wananchi ndiyo wanaowachagua viongozi wao wanaowataka na wala siyo watawala "kulazimisha" matokeo kwa kuonyesha kuwa CCM wameshinda kwa kishindo, hakika watasababisha machafuko nchini.
 
CCM wana masikio na macho lakini sidhani kama wanaliona sanduku la kura na kama wanaliona basi hawaelewi ni dubwashana gani
 
Kwa jinsi nilivyoona na kufatilia sijui hata kama walifikisha 30% ya wapiga kura waliojiandikisha.
Ndiyo uone namna watawala wetu wanavyotuona wananchi wake tulivyo wajinga na wapumbavu, tusioweza kupambanua na kuujua ukweli
 
Kuna muujiza gani ambao mkoa wa Dar ulitumia hadi kuandikisha wananchi zaidi ya asilimia 108 ya watu waliotakiwa kujiandikisha, katika uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba mwaka huu??

Tukumbuke pia tulipewa taarifa na Waziri wa Tamisemi, kabla zoezi hilo halijaongezewa muda wa siku 3 wa kujiandikisha, kuwa mkoa huo katika siku 10 walizopewa za awali kujiandikisha, wenyewe ndiyo ulishika mkia, kwa kuandikisha wakazi wake asilimia 8 pekee!

Sasa ninachojiuliza mkoa huo ulitumia miujiza gani kuandikisha wananchi wake zaidi ya asilimia 108, kwa siku 3 pekee zilizoongezwa kwa uandikishaji??

Tumeona namna ambavyo.uandikishaji huo ulivyodorora sana hata katika siku 3 za nyongeza za uandikishaji huo,ambapo makarani walikuwa wakiuchapa usingizi, katika vituo vya uandikishaji wakiwasubiri hao wananchi wa kuwaandikisha

Tulishuhudia wakuu wa wilaya wakihamasisha kwa kuongea na vipaza Sauti, viwamja vitupu kabisa katika maeneo mbalimbali ya hii hilo

Tunamuomba Rais Magufuli auchungize mkoa huo kwa kuwa tunaamini kabisa, takwimu tulizopewa na Mheshimiwa Jafo ni za kupika za wazi kabisa na tunasmini pia walioandikishwa ili kuweza kuvunja rekodi, ni wale wasiostshili kujiandikisha, kama vile watoto wa shule za msingi za mkoa huo, ambao ni dhahiri hawajafika umri wa kujiandikiisha,, ambao ni miaka 18

Ikumbukwe pia zoezi hilo "lilisusiwa" na wakazi wake wengi sana, kwa kile ambacho wakazi hao wamekieleza kuwa zoezi zima la upigaji kura hapa nchini Tanzania hivi sasa kuwa kama kichekesho!

Kwa kuwa wanajua kuwa watawala wetu "wanalazimisha" ushindi wa kishindo kwa chama cha CCM, hata katika maeneo yale ambayo hawakushinda kabisa!

Tuendelee kiwasihi watawala wetu kuwa wasiwageuze watanzania wote kuwa ni wajinga na wapumbavu ambao hawajui kinachoendelea nchini kwetu hivi sasa,

Ni muhimu sana kuwa kura inayopigwa na mwananchi kwenye sanduku la kura iheshimiwe na kusiwe na uchakachuaji wa kura hizo hata kidogo

Kwa kupewa uhakikisho huo pekee, ndiyo kutaweza kuwarejeshea Imani ya kujiandikisha na hatimaye kuwapigia kura wale viongozi watakaowaona wanafaa katika maeneo husika
Akili za Bashite aonekane kafanya kazi nzuri sana.
 
CCM wana masikio na macho lakini sidhani kama wanaliona sanduku la kura na kama wanaliona basi hawaelewi ni dubwashana gani
Lazima tuwaambie ukweli hawa CCM kuwa huko wanakotupeleka siko kabisa, kwa vile ukitembea mitaani utawasikia maelfu kwa maelfu, wakikiri wazi kabisa kuwa hawajaona sababu ya kupoteza muda wao kujiandikisha, sasa unajiuliza hao wananchi zaidi ya asilimia 108, aliyotutangazia Waziri Jafo, ni za kupika??
 
Idadi hii ni muhimu sana kwa CCM kuweza kujitangazia ushindi mkubwa wa kishindo, kumbuka uchaguzi wanaandaa wenyewe, wanasimamia wenyewe, wanahesabu zao wenyewe na wanatangaza wenyewe chini ya maelekezo na ulinzi mkali.
 
Akili za Bashite anazijua mwenyewe. Kazoea kulisha matango pori
Inashangaza kuona Rais akiendelea kumkumbatia, wakati vitendo anavyovifanya kila mtu anaviona kuwa anavunja sheria
 
Back
Top Bottom