Hivi mke wangu anajiandaa kuachana na mimi au?

Mtu mwenye mpenzi halaf akatafta mpenz mwengine maana yake hampendi huyu alonae,sabab kama angekuwa anampenda mwengne angemtafuta wa nin? Najivika kiatu cha mkeo, amegundua kubwa ni kuwaandalia future watoto na si kulazimisha lisilokuwepo.
 
Ulikosea lakini unastahili msamaha.., hapo inabidi umrudishe mwenzio kwenye hali ya kawaida kama kweli anataka kukengeuka, embu tenga kama wiki tatu za kuwa naye karibu sanaaaaaaa..

, mwonyeshe mapenzi ya hali ya juu.., mtoe out, ongea naye kuhusu mipango ya maisha, malezi mazur ya watoto, jaribu kumpeleka kufikiria miaka 40 mbele...,

then SIKU moja utakayoona yupo kwenye mood nzur na ana furaha MWULIZE KUHUSU HALI yake, mwelezee madhara yake, vip na wewe ukaanza kufanya hivyo,

vipi mipango ya miaka 40 mbele? HALAFU mpe muda wa kuamua.., kama ataendelea means hatakaa akuelewe.., so nawewe unaanza kukaa kiupande upande....!
 
Bob Marley aliwahi kusema kitu kimoja.."the greatest problem that mankind face is failing to keep issues where they are"

sasa lets try to keep issues where they are
tatizo letu hapa sio usaliti aliowahi kuufanya jamaa..maana aliomba msamaha akasamehewa..na its been a long long time..so hata kama mwanamke angekuwa na roho ngumu vipi angeshasamehe..after all jamaa tangu hapo hajawahi kumpaexcuse ya kumhisia vibaya tena.

Ni kweli jamaa alikosea kmsaliti mkewe but right now that is immaterial..the issue tuliyonayo mkononi ni usiri wa mke wake katika kufanya mambo ambayo 100% yanahusiana na finance...mimi ningeelewa iwapo katika maisha yao labda jamaa ana matumizi mabaya ya fedha, au mke wake aliwahi kumtrust na some amount jamaa akaisquander au something like that..lakini no..ugomvi uliowahi kutokea ni wa kimapenzi sio wa kipesa

Inawezekana tatizo la jamaa ni kuwa tangu mwanzono mwa maisha yao ya ndoa hawakuweka ule mpango tunaoita common pool...kwamba mwisho wa mwezi yeye na mkewe wanatakiwa wacontribute kiasi fulani katika mfuko wa pamoja wa kuendeleza mambo ya familia..inavyoonekana kwa upande wa mke ni chako chetu, changu changu

sasa basi, suala la mke anajiandaa kuishi peke yake sidhani kama lina uzito mkubwa ila ninachoona hapa ni kuwa jamaa aestablish evidence kuwa ingawa wote ni wafanyakazi, bado mke hachangii chochote katika family development financially ili litakapotokea la kutokea habari ya "tulichuma wote" isiwepo

Pia nadhani hata mheshimiwa mwenyewe anaweza akafollow suit..aache kumshirikisha mkewe katika baadhi ya mambo na mke abaki kusikia tu...akielewa hiyo kitu na akachukulia poa basi uwe ndo mtindo wa maisha..none among them will be the loser!!!
 
Yule mzinifu mwenzio si bado anakupenda uhamie kwake kabisa?

Hii usithubutu. Fanya hivi kama upo serious maana anaweza kuondoka kweli nawe ulikuwa unatania. Ogopa sana mwanamke ambaye hana tabia ya kufunga vitu na kuondoka.

Kama umekaa na mwanamke zaidi ya miaka 10 na hata mara moja hajawahi kufungasha vitu na kuondoka alafu akarudi usimtanie habari ya talaka. Ukisema kitu jua neno halirudi nyuma utatamani kulifuta haitawezekana.
Ila kama kweli upo tayari kwa lolote waweza mwambia.
 
Hapo kuna matatizo mawili makubwa.
1. Kakosa uaminifu kwako kabisa, kwamba kama uliweza kutembea na rafiki yake tena hapohapo nyumbani na yeye akiwepo umemuumiza sanaaa hiyo elewa. Na maumivu ya hili hayaishi haraka ila yataisha tu endapo utaonyesha upendo wa hali ya juu kwake.na kuonyesha kujutia sana kosa lako na kuonyesha mazingira yaliyosababishwa na huyo rafiki yake wewe kutenda kosa.

Mchukue mpeleke kwa wazee wa dini au watu wa saikolojia wanaohusiana na maswala ya ndoa na kumpa canselling. Onyesha wazi kutambua makosa yako bila kificho na kukiri kurorudia tena.

2. Umesema umejenga guesthouse kijijini kwenu na msismamizi ni mamako je mlikubaliana hili au ulikubaliana na mamako?
Mapato ya hii guest house yeye anayajua? Je.huko kijijini wanajua kwamba hiyo guest house ni mali yako na familia yako au ni mali ya nduguzo? Wanatambua hilo?

Kwanini uliamua kwenda kujenga guest house kijijini kwenu na si mahali mnapoishi nyinyi wakati huo? Je ulimweleza sababu za kufanya hivyo na akaridhika?
 
Binafsi namchukukia mtu anaezini na rafiki wa mke wake au mme wake ...... Tena wote mnaozini nje ya ndoa dawa yenu ipo . waangalie sura zao
 
Kwani huyo jamaa amefanya "mortal sin"?japo sehemu ya maelezo yako haisemi kwamba ulikiri makosa kwa dhati nae kukusamehe.Ushauri wangu jamani kama tuwaheshimu wasaidizi wetu hasa kwa maana ike halisi ya mke ni msaidizi.
 
Mkuu nashangaa sana, hivi kwa hesabu zako unadhani bado upo kwenye ndoa. Hakuna kitu kibaya kwenye ndoa kama mke kumfumania mume, hata iweje hakusamehe katu. Nina asilimia zote hata yeye ana mtu ama mchepuko wake na ndo huyo anaempa idea za biashara na kumsimamia mambo ya license na nyaraka nyengine muhimu. Ushauri... mtoe out kupata dinner na baada ya chakula mwambie umeamua kumpa talaka just as a joke uone ata react vipi. Utapata jibu

Kuna vya kutania siyo hivyo

Na huo ni utani wa kiboifrendi.
 
Hehehehehehehrhehehhehehehehehe!
Nacheka kama mazuri!
Pole mwayego!
Ahahahahahahahaha!
 
Nampa hongera huyo mwanamke kwakujiandaa kw lolote lile akil yake hijalala.
 
Kama alikusamehe kwa dhati ya moyo na unakiri unampenda jaribu kuokoa ndoa hiyo alafu ukiona haijakaa sawa chepuka tena
 
Kwa kweli mwanaume sio ndugu.
Na muomba ushauri kaleta hapa kwa vile tu mkewe ana uwezo wa kujifanyia yake yakaenda.
Mke angekua kapuku hoehae anategemea kila kitu kwa mume basi yule rafiki angekua nyumba ndogo.
Yani hapo mke sio kwamba anajiandaa kuachana nawe ile umempa tahadhari kua wewe sio wa kuaminika hivyo ameamua ajiandae kwa lolote litakalotokea. HAKUAMINI TENA
Anakupenda ila anaishi nawe kwa kujihami.
Nimempendaje!!!?
 
hufai kabisa ww mwanaume una mwanamke mwenye kujituma lakini huna akili
anajiandaa kukuacha huyo nampa hongera sana amefanya maamuzi mazuri sana
 
Back
Top Bottom