Hivi mke wangu anajiandaa kuachana na mimi au?

Hivi mke wangu anajiandaa kuachana na mimi au?

jean paul

New Member
Joined
Apr 26, 2015
Posts
1
Reaction score
4
Kwanza naomba mnikaribishe mimi ni mgeni humu

Husika na kichwa cha habari, nimekua nikijiuliza hili swali kwa kipindi kirefu sana bila majibu. Mimi na mke wangu tulifunga ndoa ya Kanisani miaka kumi iliyopita, tuna watoto watatu, sisi sote ni wafanyakazi na sote ni masters holders.

Miaka saba iliyopita mke wangu alinifumania na rafiki yake kipenzi. Huyo rafiki alikua anaishi mkoani mara nyingi akija Dar es salaam alikua akifikia kwetu, so akawa amekuja kwa mambo yake.Jumapili moja wife na familia walienda kanisani akabaki rafiki na mimi, baadae nikaenda bar kupata supu, then nikazimua bia kadhaa hadi mchana nikaenda home nilale kidogo nitoke tena.

Nilipofika home nikafungua geti dogo, nilipaki Gari nje. Nikasikia kilio cha mahaba sebuleni naingia hivi namkuta shemeji akiwa na top tu chini hana chochote akijihudumia kwa mkono huku alilia kwa sauti kubwa, nilishindwa kujizuia nikaanza kuvua nguo kama nafukuzwa nikamrukia kochini na akanipokea kwa mikono miwili.

Ikawa ndo mchezo wetu, kumbe housegirl aliunyaka mchezo mzima na kumshtua wife na wakatuwekea mtego ambapo tulinasa, nilikua nimeamka usiku wa nane nikaenda kwa shemeji tukiwa katikati wife akaingia na kutuma na kumtimua rafiki usiku huo huo.Nikamwangukia na kuomba msamaha na nikasamehewa.Miaka michache tangu fumanizi hilo wife akaanzisha tabia ya usiri na kutonishirikisha mambo yake hasa ya maendeleo

(1) Tukio la kwanza:-
Alijenga nyumba sehemu flani hapa Dar es salaam bila mimi kujua, fundi wake alinipa hizo taarifa accidentally
Nilipom confront akakiri na kukosa majibu ya maana.

(2)Tukio la pili:-
Akafungua duka la nguo kimya kimya nikabaini kupitia intelligence info nilizopata akaruka sio duka lake
Ila baadae nilithibitisha ni la kwake.

(3)Tukio la tatu.
Alinunua shamba bagamoyo worth 10 million niligundua baada ya yy kudhulumiwa kumbe Dalali alimtapeli shamba halikua lake.Kesi ikaenda polisi hatimaye mahakamani ikafika pahala ikashindikana kuficha nikagundua, nikaingilia kati kumsaidia mke wangu akarudishiwa pesa zake tukafuta kesi

(4)Tukio la nne
Alinunua Gari 35 million dream car yake, tangu anadunduliza hizo hela akawa anatuma Japan kwa binamu yake kidogo kidogo lakin kimya kimya hadi likafika, nikastukia tu siku amekuja nalo home badala ya kufurahi kwa kweli nilihuzunika

Gari hilo ilibaki kidogo tu liibiwe nikaingilia kati halikuibiwa ilikuaje? Ni hivi:-
Kumbe kijana aliemfanyia clearance bandarini wife hakumlipa yule kijana wakatofautiana
Janki alitaka 1.5 million wife akadai ni laki tano dogo akagomea hela akasema utaona

Baada ya mwezi hilo Gari likaibiwa kibo complex tegeta wife alilia kama mtoto mwanaume nikaingia kazini. Nikatenga kama 1 million kwa polisi, kwa kutumia technolojia ya mawasiliano na kwa ku mtrack yule dogo na mawasiliana yake hatimaye gari ikapatikana dogo yupo nyuma ya nondo hadi leo.

Hata hivyo wife hajaacha hii tabia, hivi sasa ana biashara ya kukopesha watu kwa riba anaifanya kwa siri kubwa ila mimi naijua nimeamua kumuacha tu aendelee maana nimeshachoka.Wadau huyu mtu ana mpango gani na ndoa hii? Au ndo anajiandaa kuishi kivyake baadae? Nimefañya kosa gani lisilokua na msamaha? Kama lipo naomba mnisaidie majibu ya haya maswali.

Kwa upande wangu, biashara zote nazofanya mbali na kazi yangu anazijua.Hata nyumba nilizojenga nimempeleka kote. Nina guest kijijini kwetu ambayo mama yangu mzazi anaisimamia pia Mke wangu anaijua ingawa ningeweza kumficha na asingejua nipo njia panda najiuliza huyu mtu ni Wa kufa na kuzikana kweli?
Je safari yetu ya maisha ni moja kweli?

WanaJf sincerely naomba kwa moyo wenu wa dhati mnisaidie mawazo.

NB: Sijazini tena tangu nizini na Rafiki yake miaka saba iliyopita nae sijawahi kumshika wala kumshuku kwa uzinzi.

Karibuni kwa mawazo
 
asante kwa kunijuza hayo ya mashamba ya mamilion ya hela tukirud kwenye mada je ulishawah kukaa nae chini mkaulizana inakuaje anafanya sir??? ni ngumu kukushaur had nimskie na mkeo
 
Kama anakupenda we wasiwasi wa nini? Yeye kufanya hivo si mjinga lazima kuna kitu unakifanya kwa siri kashakushtukia ndo anajihami mapema usimuone kanyamaza kwanza ulivo mcheat ingawa alikusamehe ya kuongea ndo mana ana Fanya yake kisiri sioni tatizo mwanaume unaye lala na rafiki yake . Pia ukute hupendi kuona mkeo akifanya maendeleo mana wanaume wengi huwa hampendi ungekua uko Sawa usingemhofia cha msingi kaa naye chini umuulize kwa Upendo, ana lengo gani kukuficha, na we we uache kudate na wanawake nje ya ndoa.
 
asante kwa kunijuza hayo ya mashamba ya mamilion ya hela tukirud kwenye mada je ulishawah kukaa nae chini mkaulizana inakuaje anafanya sir??? ni ngumu kukushaur had nimskie na mkeo

Hivi huwa ni lazima wakae chini!!!
 
Ulimficha kuwa unazini na rafiki yake hadi alipokufumania. Ajabu iko wapi anavyokuficha mambo yake ya maendeleo na wewe uwe unafumania hivyo hivyo. Nadhani hata adhabu anayokupa ndogo sana sababu mwisho wa siku mali zake na za kwako ni za watoto wenu, hivyo vumilia tu, kuwa mpole
 
Hicho ndio anachokufanyia mkeo....
 

Attachments

  • 1430145300657.jpg
    1430145300657.jpg
    16.5 KB · Views: 2,262
seek a proffesional counsellor everything will be sotted out and you wanna live a happy alife again.
 
Leo jioni sijui nakula mini ntakuwa na wazo la kuchangia jamani, njaa inaharibu Hadi akili eti
 
Nikuulize Mkuu , ivi ingekua wewe ndio umemfumania kama alivyokufumania wewe Ivi leo hii mgekua pamoja au ingebaki story tuu? Nirahisi kusema kosa Gani lisilo samehewa lakini umekaa ukafikiri umemumiza kiyasi gani?
 
ni vema ukakaanae ukamueleza yote kwa uwazi , usikie atakupa jibu gani , ila nadhani uaminifu wake kwako haupo tena , anaishi na wewe kama mwanaume wa kawaida tuu na si mume kwake.
 
Khaa!! Ulifanya ujinga mkubwa. Kama unatamaa ya Malizake nawe mtafute best wako sana amgonge yaishe
 
Kikubwa hapa utalipia maumivu yote wanaume waliyowahi kuwasababishia wanawake wote watakaopita humu. Brace yourself bro.
 
Mkuu, FYI baadhi ya wanawake hujenga chuki under-ground......................... halafu hutokezea kule upande wa pili !! Itakubidi uweke kikao na wazee wahusika ili makubaliano ya kudumu kwenye amani yawepo !!
 
Alichokifanya na anachokifanya ni sawa kabisa.
Umethubutu kulala na rafiki yake inaonyesha wewe hufai kabisa,ndio maana hakushirikishi kwenye mambo yake.
 
Unapokua unakunywa fanta ukaamua kuondoka na kuanza kutumia pepsi inamaana kunakitu kipo kwenye pepsi cha ziada.mdada anafanya yake....kama ni ndoa wewe ulipokua unagonoka hukuijua? Welldone dada
 
Back
Top Bottom