Hivi kweli nyie mipango miji mnawezaje kuachia watu wanajenga hovyo namna hii (ona picha) tena karibu kabisa na mijini..??! Em' fanyeni mbomoe hivyo vibanda haraka sana mjenge grid roads nzuri ziendane na hiyo BRT road hapo kati. Pitisha bulldozer hapo na hakuna kumpa mtu fidia hapo watatutia hasara tu.., kama jitu lilikuwa na ujasiri wa kujenga kiholela basi liwe na ujasiri wa kuvunjiwa na kuhamshwa kihololela!
Inaboa kweli.., hivi kwanini mtu usiwahi kufanya planning then uuze viwanja ili ufidie gharama ya hiyo planning.., hapa msiseme hakuna fedha ya kufanya hiyo planning.., hiki ni kitu ambacho ni self paying..