Uchaguzi 2020 Hivi mgombea wa CCM atafikisha hata 40% ya kura kweli?

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Nimeamini na huu ndio ukweli kwamba mgombea wa CCM atapoteza kiti chake siyo kwamba hajafanya kitu laahasha, shida kubwa ni mipangilio isyokua na mfumo ulionyooka. Ameshikilia kufanya mambo makubwa kwa wakati mmoja huku akiacha mambo madogo madogo yanayoigusa jamii. Hii kitu itamwangusha vibaya sana na walimshauri siyo wazoefu wa siasa za vyama vingi.

Unakimbilia kujenga mabarabara, mabwawa ya umeme, kununua mandege na kuhamisha mji kwenda Dodoma kwa wakati mmoja huku huduma zinazoingiza jamii moja kwa moja hutekelezi, watumishi wa umma umewaacha, ajira kiduchu kwa vijana,mikopo ya elimu ya juu shida tupu,huduma za afya bado ni tatizo, shida kwenye biashara mzunguko mgumu wa pesa mtaani, uhuru wa kujieleza ni shida. Haya yote yanachochea chuki, watu hawaangalii miundombinu hii wanataza maisha yao yanakwenda vipi.

Nataka niseme kwamba, kwa mwendo anaokimbia nao Tundu Lissu na hoja zake zenye mashiko na ngumu, ndiyo maana wananchi wengi wanakimbilia kwenye mikutano yake wakidhani kua huyu ndio mtu atakayewania shida zao badala ya yule anayetengeneza vitu kwa ajili ya mtaji wa kisiasa.

Kuna uwezekano CCM hata kura 40%% kisipate. Lissu anaweza kupewa 60% kama pumzi ya waliochoma. Swali ni je, Mgombea wa ccm anaweza kupata kura hata 40% kweli?
 
Nataka niseme kwamba, kwa mwendo anaokimbia nao Tundu Lissu na hoja zake zenye mashiko na ngumu, ndiyo maana wananchi wengi wanakimbilia kwenye mikutano yake wakidhani kua huyu ndio mtu atakayewania shida zao badala ya yule anayetengeneza vitu kwa ajili ya mtaji wa kisiasa.
Lowassa aliwajaza watu kuliko lissu, tunasubiri tu tarehe28 tukamfyeke huyo raia wa ubelgiji
 
Fanya utafiti bila mbwembwe za ushabiki wa hisia zako, jijengee kihoji watu bila kuonyesha mrengo wako (hakikisha hukosei ukaonekana), waulize ukiwa chumba Cha kupigia utampigia Nani kati ya Lisu na Magufuli, na kwa wale amba huwa wanasema sitaenda sitapiga kura, waulize ikiwa utaamua upige kura utampa nani?

Hutaacha kuona rangi!
 
Nimeamini na huu ndio ukweli kwamba mgombea wa CCM atapoteza kiti chake siyo kwamba hajafanya kitu laahasha, shida kubwa ni mipangilio isyokua na mfumo ulionyooka. Ameshikilia kufanya mambo makubwa kwa wakati mmoja huku akiacha mambo madogo madogo yanayoigusa jamii. Hii kitu itamwangusha vibaya sana na walimshauri siyo wazoefu wa siasa za vyama vingi...

Bwana yule akipata 40 Percent ashukuru Mungu. Hapo hujazungumzia pyu pyu pyu na kupotea kwa watu!!!
 
😂😂😂 Watu Banaa......

Ametiririka Weeeee... akaupuuza Ushawishi Mkubwa Wa CCM, Juu Ya Raia Wengi,Hususani Wanawake,Wazee na wale Waishio Wilayani Na Vijijini.

Je Ujenzi Huu Wa Miundo Mbinu Mfano lile BWAWA la Kufua Umeme Pale Rufiji,utaukosesha kura CCM?!!!

JIBU= Hapana

KWANINI?!!!

Kundi Kubwa La Watanzania Wenye Umri Wa Umakamo na Utuuzima na Wanawake Ambalo NDILO MTAJI USIODODA wa CCM,halijasahau MADHILA ya Kusuasua kwa Uzalishaji wa Umeme Nchini.

Kundi Hili,Linakumbuka kuwa,BUNGE la 8,9,10 Lilifululiza maneno Mazito ya kutaka TANESCO ivunjwe na hata kupewe TAASISI BINAFSI itakayozalisha Umeme.

Kwanini WABUNGE wanaojua KATIBA kufika kutaka tenda ya usambazaji Umeme ipewe SHIRIKA BINAFSI kinyume na KATIBA?!!!!

Hewaaa,Usiwasahau wale WAPIGA kura wa Uhakika wa CCM niliowataja hapo Juu,pamoja na WABUNGE hao,wote WALIKIRIHISHWA na yafuatayo:

#Nchi Kuwa Kiza
#Shughuli za Uzalishaji Mali Kuzorota
#Taifa kuingia Hasara zaidi ya dola milioni 200.
#Serikali Kuingia Gharama kubwa ya kuagiza Mafuta ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha Umeme.
#Net Group Solution halikuwa suluhisho Kuntu.
#Mzimu Wa Dowans toka 90s ya Mzee Mwinyi.
#Jinamizi la Escrow.
#Wapigaji Kuendewa vyema na BIASHARA ya MAJENERETA(na yalilipa kwani vipindi vya mgao wa umeme Kariakoo kulikuwa na kelele Kama KARAKANA)
#Wahujumu Wa Nchi Kutiririsha maji yatoke BWAWANI MTERA ili tuendelee na "nakama" yetu.

SHIDA YA UMEME Leo imepata msuluhishi wa VITENDO,mh.Magufuli....

Awamu ya 5 Imetujia na UTEKELEZAJI BORA wa Kujenga BWAWA la KUZALISHA UMEME wa Megawati 2200 pale RUFIJI.Hili Limewakuna Sana WALE NILIOWAORODHESHA hapo Juu na HAKIKA hawatoinyima KURA CCM.
Hakika Hawatoacha kumpa kura MAGUFULI.....
Kura Zao ni nyingi mno,Tena mno....OKOTEZAOKOTEZA katika Miji Mikubwa,halafu nenda Ukazizoe Wilayani na Vijijini(huko watu wameamka kwa umuhimu wa Umeme;REA).

Kwa Hiyo,sioni MAGUFULI Akianguka KATIKA Hili moja tu la UMEME.

Nitaendelea na mengine YATAKAYOMBEBA MGOMBEA URAIS WA CCM.

Jumbe Brown
Kijana Muuza Al Kasus
Tandale
 
Inakisiwa kwamba aweza pata kura halali asilimia 34 mpaka 36. Lakini, Tume ya uchaguzi itasema amepata asilimia 56, na hiyo ndo siri iliopo kwenye ule utafiti wa shirika flani kutoa repoti inayo onesha asilimia 56
 
Inakisiwa kwamba aweza pata kura halali asilimia 34 mpaka 36. Lakini, Tume ya uchaguzi itasema amepata asilimia 56, na hiyo ndo siri iliopo kwenye ule utafiti wa shirika flani kutoa repoti inayo onesha asilimia 56
Mkuu ni Shirika lipi Hilo?
 
Nimeamini na huu ndio ukweli kwamba mgombea wa CCM atapoteza kiti chake siyo kwamba hajafanya kitu laahasha, shida kubwa ni mipangilio isyokua na mfumo ulionyooka. Ameshikilia kufanya mambo makubwa kwa wakati mmoja huku akiacha mambo madogo madogo yanayoigusa jamii. Hii kitu itamwangusha vibaya sana na walimshauri siyo wazoefu wa siasa za vyama vingi.........
Labda kwa wizi
 
Nimeamini na huu ndio ukweli kwamba mgombea wa CCM atapoteza kiti chake siyo kwamba hajafanya kitu laahasha, shida kubwa ni mipangilio isyokua na mfumo ulionyooka. Ameshikilia kufanya mambo makubwa kwa wakati mmoja huku akiacha mambo madogo madogo yanayoigusa jamii. Hii kitu itamwangusha vibaya sana na walimshauri siyo wazoefu wa siasa za vyama vingi....
Hawezi kufikisha maana wananchi wamesha amua kuifuta ccm kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lowassa aliwajaza watu kuliko lissu,tunasubiri tu tarehe28 tukamfyeke huyo raia wa ubelgiji
Tunaongelea mgombea urais mwaka 2020 mzalendo wa kweli asiyo na makando kando, mbeba maono na matumaini ya watanzania mh Lissu.
photo%20266%2012-18-0.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom