Hivi masikio yamewakosea nini?

mjambaji

Senior Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
174
Reaction score
98
Jamani naomba mnisaidie kujibu hili swali,

Hivi kwa nini watu hupenda kusifia sehemu mbalimbali za kichwa cha binadamu kama vile; macho, pua, mdomo n.k. lakini sio masikio?

Mara nyingi utasikia watu wakisema...ana macho mazuri, mdomo mzuri, pua nzuri n.k... lakini ni vigumu kusikia mtu akisema flani ana masikio mazuri. Najaribu kujiuliza ina maana hakuna masikio mazuri? Na kama yapo mbona hatuyasifii?
 
Mimi masikio yangu kama mabawa ya mbuni. Hivi ni nani atayapenda? Labda mimi mwenyewe.

Hata hivyo binadamu huwa tuna kawaida ya kusifu vionekanavyo kwa urahisi zaidi kama vile sehemu za uso, kifua, mapaja, mgongo na usisahau protruded makalio mkuu😀😀:thumbup::thumbup:
 

Du! Umenifurahisha eti kama mabawa ya mbuni. Si ajabu ukapata mtu akayapenda hivyohivyo yalivyo.
 
Mbona magoti, viwiko, na visigino pamoja na ugoko havisifiwi kwa uzuri wake?
 

Hata k husifiwa
 
Ah! Ni ya ajabu!!! Alafu umri wako utakuwa under 25!!!
Kwani uajabu wa ID yangu ni upi? Halafu be careful unaweza ukakuta mi ni babu yako kimiaka. So usiwe na haraka ya kudhani niko under 25.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…