Hivi makampuni makubwa kama Bakhresa Food Products na Bonite Bottlers wanawezaje kufanyia service magari yao?

AlphaMale

JF-Expert Member
Oct 26, 2019
613
1,402
Nlikua kwenye biashara ya usafirishaji (bodaboda) ila kilichonifelisha sio kodi, wala faini za barabarani, wala usumbufu wa madereva, kilichonifelisha ni service za Mara kwa Mara, yani hesabu ya miezi miwili inaliwa na service ya Siku moja, au kila wiki kitu flani kinaharibika kwenye pikipiki, mpaka inafika mahali mtu usipokiuza chombo cha moto, kinakufilisi hata kama una gereji yako binafsi, wanasema chombo kikitumika mda mrefu baada ya miaka 2 ndo kinaanza kusumbua service, ila kikiwa kipya ndo hakisumbui service, ila najiuliza

Bakhresa food product wana scania nyingi sana za zamani kidogo, INA maana magari yao hayapatagi breakdown za Mara kwa Mara? Magari ya bonite ya kusambazia soda ni ya zamani mno tena wanazo faw, howo, canter, na fuso kama 200 hivi, magari yao hayapati breakdown za Mara kwa Mara?

Kuna jirani hapa nae alinunua fuso anasema haijawahi kumwekea laki 2 ndani kisa service za Mara kwa mara, Mara hiki Mara kile, service zinakuwa nyingi mpaka inafika mahali MTU inabidi uuze gari au pikipiki hata kama ulikuwa huna shida wala mpango wa kuliuza.
 
Mkuu Mtu kama Bakhresa ameajili Transport Manager ambaye ana timu yake ya watu wa Mechanics hata Karakana ya kutengenezea magari ipo pale so kuna watu wanalipwa kazi yao ni kuagalia magari 24/7 tofauti na Wewe ambaye hauna utalaam na hauwezi kuajili.

Magari yao pia yana Ving’amuzi na Kwa hapa Dar Magari yao mengi hayaendi Petrol station zetu hizi yeye ana visima vyake vya kujazia kwenye Karakana.
 
Kwa uzoefu wangu, kampuni kubwa zote zina Meneja Usafiri halafu kuna Mkuu wa Madereva na Makenika mkuu na wana gereji maalumu ya kutengeza magari yao. Hawa kazi zao ni kufuatilia ubora wa gari kila siku. Gari mara nyingi zikipelekwa gereji hawalipi kila siku hadi wanapoletewa invoice kwa mwezi ndo wanalipa. So hao wanne kazi yao ni kuhakikisha ubora wa magari. Halafu siku hizi kampuno nyingi zina petrol station zao au wameingia mkata na petrol station wanazojaza mafuta kwa kadi maalumu, mfano Total.
 
Swali lako ni zuri sana na majibu utayapata

Kumiliki chombo cha moto unahitaji kwanza ujue chombo unacho miliki kinahitaji nini ili kiwe imara

Kwa watu wengi hujikuta katika umiliki wa vyombo vya moto kwa ushawishi wa kusikia vinalipa sana na hapo mtu hujikuta wakinunua vyombo vilivyo tumika na kuhitaji matengenezo makubwa kuliko hata thaman anayo uziwa

Hapa ndio mnunuzi huanza kuunga unga spea ili chombo chake kitembee hapa ndio hujikuta mauzo anayo pata kupitia chombo chake huishia kukikarabati tena na wakati mwingne huingia hata nje ya fedha chombo chake

Na kuna pia hawa mafundi wetu na madereva hushirikiana kuhujumu matajiri kwa kuwabambikia spea mbovu ili waendelee kupiga hela kwa tajiri

Ukija kwa watu wenye makapuni makubwa mara nyingi hawa huagiza spea zao toka kiwandani kinacho tengeneza hayo magari

Na huagiza spea za kutosha na hapo huuziwa bei rahisi kuliko unae enda dukani kufuta spea moja na pia huzingatia ubora wa spea husika

na kumbuka unapo nunua chombo cha moto jitahidi ununue kwa umakini usije kununua rangi ya nje na ndani ya injini na vipuri vingine vikawa vimeisha

Na kama bajeti inaruhusu bora ukapata km 0 hii itakupa faida zaidi na usumbufu haupo
 
Wewe ulipigwa na huyo dereva wako

Sent using Jamii Forums mobile app

Siamini sana, maana pikipiki nimeziuza kwa mkataba kwa mtu mwingine (tofauti na aliekua dereva wangu) hio ya mkataba, dereva mpaka amalize mkataba ni mziki, kwasababu ya service, mmoja wa dereva ameuza hadi kuku na simu alio nayo

Huyo niliemuuzia kwa mkataba hawez kunizungusha na kunichelewesha kunipa hela maana akifanya hivyo anajipiga risasi mwenyewe.

Just imagine mwezi mzima MTU anakuwa na uwezo wa kukuletea elf 60 tu, tena kipindi hiki cha mvua MTU anakuletea elf 30 kwa mwezi ya mkataba Danpol
 
Uchawi wa gari ni service na management .ukiweza yote hayo bila kuwa na mkono wa birika utaona faida ya vyombo vya usafiri
 
Wana garage zao,mafundi wanalipwa kea mwezi,Kunakuwa na team inatoongozwa na fundi mkuu,ambae yeye ndo anavuta mkwanja mkali,kwani hata kwenye manunuzi ya spare pia lazima ahusike
 
Kwa uzoefu wangu, kampuni kubwa zote zina Meneja Usafiri halafu kuna Mkuu wa Madereva na Makenika mkuu na wana gereji maalumu ya kutengeza magari yao. Hawa kazi zao ni kufuatilia ubora wa gari kila siku. Gari mara nyingi zikipelekwa gereji hawalipi kila siku hadi wanapoletewa invoice kwa mwezi ndo wanalipa. So hao wanne kazi yao ni kuhakikisha ubora wa magari. Halafu siku hizi kampuno nyingi zina petrol station zao au wameingia mkata na petrol station wanazojaza mafuta kwa kadi maalumu, mfano Total.
Ivi kampuni gani? ya mafuta ni nzuri haina uchakachuzi wa mafuta yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siamini sana, maana pikipiki nimeziuza kwa mkataba kwa mtu mwingine (tofauti na aliekua dereva wangu) hio ya mkataba, dereva mpaka amalize mkataba ni mziki, kwasababu ya service, mmoja wa dereva ameuza hadi kuku na simu alio nayo

Huyo niliemuuzia kwa mkataba hawez kunizungusha na kunichelewesha kunipa hela maana akifanya hivyo anajipiga risasi mwenyewe.

Just imagine mwezi mzima MTU anakuwa na uwezo wa kukuletea elf 60 tu, tena kipindi hiki cha mvua MTU anakuletea elf 30 kwa mwezi ya mkataba Danpol
Nimekaa na pikipiki mkuu , hakuna kitu ngumu kama pikipiki , na kwa wingi wake hapa mjini kama zingekua mbovu kama unavyodai ww kwa mafundi pikipiki ungekuta foleni ya pikipiki mamia kwa mamia , wewe ulipigwa na dereva wako.. piki piki ni jembe haswa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo makampuni makubwa hawasubiri gari iharibike ndio watafute pesa ya matengenezo....licha ya kumiliki garage zao....lakini pia kila mwaka wanatenga pesa mapema kutoka katika faida wanayopata na kuziweka katika account maalumu....kwa ajiri ya ununuzi wa spare na servise...na kuna kuwa na idara maaulumu chini ya wataalamu...ambayo pia wanahusika katika kufanya bajeti ya kiasi gani cha pesa kitahitajika kwa mwaka.
 
Back
Top Bottom