Hivi Magufuli majipu Board ya mikopo huyaoni?

fieldmashal

Member
Nov 22, 2015
78
3
Jamani wahanga wenzangu continuing students tuliokosa mikopo, kwanza nashukuru kurejea tena kwenye jukwaa hili la elimu baada ya kuzuiliwa kidogo kutumia hili jukwaa, hizi zote ni jitihada zangu za kupigania haki yetu ya msingi, nilishikwa na hasira nikaandika matusi kwa wahusika wa loan board, ndipo uongozi wa jukwaa ukanifungia huduma.

Sasa nimerudi tena fieldmashal ndani ya jukwaa, nitapambana hadi nihakikishe jpm ameyaona na kuyatumbua majipu haya, yanayojiita mafanyakazi ya bodi ya mikopo elimu ya juu, kumbe hakuna yanachokifanya zaidi ya kunyanyasa na kutesa wanafunzi vyuoni.

Nilisikitika siku moja ITV mpuuzi mmoja alipo litangazia taita la Tz kwamba wanafunzi wote vyuo vikuu wamepata mikopo, nilitamani nipasuwe scrini niingie ili tumalizane naye, hivo ilikuwa vigumu sana kesho yake nilipopiga simu kwa mjomba kuomba hela ya chakula hapa chuoni, Kwani mjomba alisema niache usela wakati ITV imetangaza wanafunzi wote wamepata mikopo, niliumia sana, na maneno ya mjomba "usela"

Hivyo nawaomba wahanga wote na wale wote watakaogusha na hili tutengeneze modarity nzuri ili tuweze kupambana nalo, tukumbuke kuwa ipo siku na sisi tutahitajika kusomesha watoto wetu, wakikuta hii hali watasema sisi tulikuwa viraza wa kufikiri kwanini hatukuiona hii halii.?

NB: My pain, your pain, together we can, unity is power.

Let us struggle as intellectuals team work organization.
 
kwa kifup bodi wametuchonganisha sana na wazaz,yani siku hizi hawatuamini kabisa........kwanza ni tushinikize yule jamii atengue kauli yake au aitolee ufafanuz wa kina katka vyombo vya habar,pili naamin rais wetu huwa anaangalia taarifa ya habar,siku moja tu organize na waandish wa habar tutoe yetu ya moyon ili tuuanike uongo wa bodi ya mikopo,na pia ningeomba TAHLISO watoe tamko ili wazaz na wafadhil wetu warudshe iman kwetu
 
Bodi haiko sawa. Hata wafuatiliaji kutoka vyuo wameishia kula hela yetu wakidai ni yakukomboa mikopo na watoto hawapewi mikopo. Kwa kuwa awamu wameamua kuwa wafuatiliaji ni kwenda tu huko maofisini na vielelezo vyetu.
 
Pamoja sana, huyo mtu aliyetangazia umma kuwa ...WOTE WAMEPATA MKOPO.." binafsi kanichonganisha siyo tu kwa wadeni wangu bali hata wanachuo wenzangu waliokuwa wananitoa japo msosi. Sasa hali imekuwa mbaya zaidi hadi nimeonba kupewa CERTIFICATE ili nirudi tu kijiijini.
 
Pamoja sana, huyo mtu aliyetangazia umma kuwa ...WOTE WAMEPATA MKOPO.." binafsi kanichonganisha siyo tu kwa wadeni wangu bali hata wanachuo wenzangu waliokuwa wananitoa japo msosi. Sasa hali imekuwa mbaya zaidi hadi nimeonba kupewa CERTIFICATE ili nirudi tu kijiijini.

Jaman hiki kitu ni janga la sote wahanga mi naomba wahanga wote vyuo vikuu tz tuwe na kauli moja ambayo itatufanya tupate haki yetu ya msingi.
 
Sasa si muandamane kwenda loan board ,,kwani huku wanawasikia

JIPU LA BODI YA MIKOPO LIMEWASHINDA NINYI LAKINI NAWAHAKIKISHIA KUWA SISI WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TUTALITUMBUA NA KULIKAMUA WENYEWE.

na SHITINDI VENANCE

Hii bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu inapaswa kubadilishwa jina na kuwa bodi ya pensheni kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutokana na ukweli kuwa bodi hii imeshindwa kabisa kutekeleza majukumu yake mpaka pale panapokuwa na mashinikizo mazito kutoka kwa wanafunzi.

Hali hii inathibitishwa na ukweli kwamba mpaka sasa ninapoandika waraka huu bado kunawanafunzi ambao ni wanufaika wa mikopo lakini mpaka sasa hawajapewa fedha zao pasipokuwa na sababu za msingi za kufanya hivyo.

Chakisikitisha zaidi na kinachoonesha kukosa huruma kwa watu hawa ni kuwa mapaka sasa kuna baadhi ya walemavu, watoto yatima na wale wenye mzazi mmoja ambao kwa misingi ya vipaumbele ndio watu ambao wanakipaumbele zaidi chakupata mikopo lakini hawajapata mikopo mpaka sasa na wengine wanazungushwa kama pia kila uchao.

Lakini pia tunayo idadi kubwa ya wanafunzi ambao mpaka sasa hawajui hatima yao ya mikopo kwani majina yao hayajatolewa mpaka kufikia kipindi hiki ambacho vyuo vingi vimeshaanza kufanya mitihani ya awali ya majaribio kitu kinachowafanya wanafunzi hawa kukosa haki zao za kufanya mitihani kutokana na ukweli kwamba bado hawajasajiliwa katika vyuo husika na kiutaratibu tuu ni kuwa huwezi kufanya mtihani bila kujisajili na usajili haufanyiki bila kulipa ada na ada hailipwi bila kujua unapewa mkopo asilimia ngapi.

kwa hali hii watoto wa mafukara tumeonekana kushindwa kujikim na kulipa ada ya chuo hivyo wengi wetu wameshaanza kurudi majumbani kwao kwenda kuuendeleza umasikini uliokithili katika familia zao na kuachana na elimu ya juu ambayo huenda ingeweza kupunguza kama si kumaliza mnyororo wa umasikini katika familia hizi.

yote haya yanatokea kutokana tuu na utendaji mmbovu wa bodi ya mikopo kwani watendaji wa bodi hii wamekuwa wakitumia muda mwingi zaidi kujiandaa na mashindano ya soka na hata kushiriki mashindano hayo zaidi ya kutekeleza majukumu yao jambo ambalo linapelekea wanafunzi kushindwa kupata mikopo na hata wanaopata basi hawapati pesa hizo kwa wakati muafaka.

Pamoja na uzembe huu lakini pia wafanyakazi wa bodi hii ndio wafanyakazi wenye rugha mbovu na zakukatisha tamaa kuliko taasisis yoyote nchini na hata wameweza kukiuka kwa makusudi kauli iliyotolewa na naibu waziri wa wizara ya Elimu Eng siku ya tarehe 14/12/2015 kwani aliwataka kutatia matatizo ya wanafunzi nchini ndani ya masaa 24 lakini mpaka ninapoandaa waraka huu hakuna kilichofanyika .

Kwakuliona na kulitambua hili wanafunzi wa vyuo vikuu wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya mikopo SHITINDI VENANCE tuliungana na kwenda kuhoji utekelezaji wa kauli hii Bodi ya mikopo mnamo tarehe 16/12/2015 lakini baada ya kukosa majibu tulifika mpaka ofisi za Wizara ya Elimu na kupeleka hoja zetu zote lakini pia tulishapeleka malalamiko yetu kwa Ofisi ya Waziri mkuu kwa maandishi mnamo tarehe 13/12/2015 na mpaka sasa hatuja pata majibu yoyote,

Kinachoonekana hapa ni kuwa jipu la bodi ya mkopo limekosa mkamuaji maana Naibu waziri limeshamshinda hivyo kama wanafunzi wa vyuo vikuu nchini hatuwezi kukaa tunalialia tuu tukingoja aliyeshiba kuja kutupa chakula.

Mpaka sasa tumebakiwa na wiki tatu tuu za kuanza kudai boom la pili kwa mwaka huu wa masomo na kwa dalili zinavyoonesha kuwa pesa hizi zitacheleweshwa sana kwani mpaka sasa hakuna maandalizi yoyote yanayoendelea katika kuhakikisha wanafunzi wanazipata pesa hizi kwa wakati kama ilivyo kawaida ya bodi hii kuchelewesha pesa za kujikimu mara kwa mara

MAAMUZI MAGUMU
NAOMBA WANAFUNZI WA VYUO VYOTE NCHINI WALIO NA WASIO NA MKOPO MJIANDAE KWA KUFANYA MASHINIKIZO MAKUBWA YASIYO NA KIKOMO NCHI NZIMA MPAKA PALE SERIKALI ITAKAPOAMUA KUITAZAMA UPYA BODI YA MKOPO NA KUUFUMUA MFUMO WAKE MBOVU.
UTARATIBU WA MASHINIKIZO HAYO UTATOLEWA NA KAMATI YA MAWAZIRI WA MIKOPO YA ELIMU YA JUU NCHINI HIVI KARIBUNI.

KUUTUMA WARAKA HUU KWA WANAFUNZI WENGINE NI MCHANGO MUHIMU KATIKA HARAKATI HIZI. SHARE

SHITINDI VENANCE
0759704444
MWENYEKITI WA KAMATI YA MAWAZIRI WA MIKOPO YAELIM YA JUU TAIFA.
 
Back
Top Bottom