Hivi madereva wako katika muhimili wa ngapi kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi madereva wako katika muhimili wa ngapi kitaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by commonmwananchi, Jan 20, 2012.

 1. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,146
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Naomba kuuliza swali hili kutokana na yanayojili kila uchao hapa nchini kuhusiana na ajali za barabarani na unyeti wa kazi za madereva na umuhimu wa uwepo wao.kama zilivyo fani nyingine nchini na duniani kwa ujumla.
  Nasema hivyo kwa sababu katika taratibu zetu kimaisha mara nyingi unapoamka asubuhi na ili uweze kufika katika eneo lako la kazi iwe ni vitani,shuleni,hospitalini,mahakamani, bungeni au popote pale ni lazima utumie huduma ya usafiri na hata kama ni gari binafsi basi ni vema na inashauriwa kuwa na dereva mahsusi kwa usalama wako na wa chombo chako.

  Pia ni hivyo hivyo kwa usafirishaji wa bidhaa muhimu za mahitaji ya kibinadamu katika maisha ya kila siku na pia za kijeshi kwa ulinzi na usalama wa raia na mipaka ya nchi yetu.

  Hali inakuwa tofauti pale linapokuja suala la heshima,staha na masilahi kazini. Bila kusahau mazingira wanayofanyia kazi na madhila wanayokumbana nayo madereva katika utendaji wao wa kazi za kila siku
  Kwa waajili wengi nchini ni mazoea ya na kawaida sana kusikia lugha za NIPE FUNGUO ZANGU.
  au NAMTUMA DEREVA AKUFUATE DEAR UJE TUMALIZIE WEEK-END(hiyo ni mishale ya saa saba usiku) WEKA GARI LANGU HAPA AFU FUTIKA MBELE YA USO WANGU(pale ambapo ameendesha basi la abiria taratibu alafu akapitwa na lingine na akapata abiria wachache)

  Pale aambapo dereva kachelewa kuamka na kuwahi kazini kwa muda stahiki ile asubuhi kutokana na kumsubiri mheshimiwa akiwa kwenye maraha na nyumba ndogo usiku uliopita
  Basi usishangae kukuta dereva mwingine kishapewa funguo akiwa anaondoka na bosi na watampita bila hata salamu na huo ukawa ndio mwisho wa ajira kwa kauli ya (madereva mko wengi bwana.)

  Kwa baadhi ya waheshimiwa wabunge ambao ndio ilitarajiwa wawe watetezi na mfano bora kwa wananchi nao si mara moja tumesikia wakitia ndani mshahara wa dereva mahsusi wa mbunge unaotolewa na ofisi ya bunge.na badala yake kujiendesha wenyewe au kuchukuwa mtoto wa dada au akampa promo kaka wa nyumba ndogo asiye na uzoefu ili mradi tu lile fungu
  lisitumike lilikokusudiwa lote.

  MATOKEO!...Madereva walio wengi wenye sifa stahiki huachwa bila kazi na pia wale wenye sifa wanaokuwa kazini hujikuta wakifanya kazi kwa muda na mwendo mrefu bila kupumzika.jambo ambalo ukichanganya na maslahi madogo,ajira zisizo na uhakika kutokana na wengi wao kufanya KAZI bila mikataba ya kudumu huwafanya kuwa na MSONGO WA MAWAZO
  Hii ndio chanzo kikubwa cha ajali za mara kwa mara ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na rushwa kubwa iliyotapakaa nchi nzima barabarani tena mchana kweupe.

  HALI HII IKO SI KWA MADEREVA TU.BALI HATA KWA BAADHI YA MANAHODHA WA VYOMBO VYA MAJINI NA ANGANI VINGI VIKIMILIKWA NA WATU BINAFSI*JE MISIBA HII TUTAINYAMAZIA HADI LINI?
  Je hili si janga la kitaifa? Naomba tujadili wana JF labda tutakuja na solution ya nini kifanyike ili kuepukana na tatizo hili ambalo linamaliza nguvu kazi ya taifa na raslimali zetu kwa marudio ya
  Uchaguzi kila leo.
  Alamsiki
  .
   
Loading...