Hivi madaktari na pharmacists wa Tanzania huwa wanasomea nini?

my name is my name

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
2,017
2,384
Madaktari, pharmacists na hawa watu wa laboratories wa Tanzania huwa wanasomea nini chuoni? Ikitokea magonjwa ya ajabu au ya kulipuka hata hawasikiki utadhani haiwahusu wao vile.

Wanasubiria nchi za ulaya wahangaike walete dawa wao kazi yao kuandika dose tu kwa wagonjwa. Hawajawahi kugundua dawa yoyote wapo wapo tu. Wao wanajua kutoa mimba tu kuua viumbe visivokuwa na hatia ikija kitu serious wanakaa kimya kama hawapo.

Na watu wa laboratories kazi yao kupima mkojo tu na damu hawana jingine wanajua.

Hebu tumieni elimu mliopata hata kidogo ili tujue kweli mlisomea. Sio Ku kremisha dalili za magonjwa na dawa zake na kuandika lisiti tu.
 
Kuna NIMR, Kuna Chuo cha Utafiti wa masuala ya Afya huko Ifakara nk mimi binafsi ktk hojja yako natamani hata wafutwe kazi yaaani ndio wamedhihirisha wanapokea Mishahara ya Kodi yetu pasipo manufaa.

Yaaani wale wa Mitishamba/Tiba asili wako bizze kuliko hawa wasomi wetu wa Utafiti wa magonjwa. Mungu ibariki Tanzania naamini sote tutavuka Salama, RIP kaka Mbitta daima tutakukumbuka hasa Wana Simba SC.
 
Kuna NIMR, Kuna Chuo cha Utafiti wa masuala ya Afya huko Ifakara nk mimi binafsi ktk hojja yako natamani hata wafutwe kazi yaaani ndio wamedhihirisha wanapokea Mishahara ya Kodi yetu pasipo manufaa.
Yaaani wale wa Mitishamba/Tiba asili wako bizze kuliko hawa wasomi wetu wa Utafiti wa magonjwa. Mungu ibariki Tanzania naamini sote tutavuka Salama, RIP kaka Mbitta daima tutakukumbuka hasa Wana Simba SC.
Kumbe kuna chuo hadi cha utafiti 🙄 sasa huwa wanatafiti nini huko kama wanashindwa hata kugundua dawa ya tumbo la kuharisha.
 
Tatizo kubwa mfumo wetu WA elimu na ukosefu wa vifaa vya kufundishia na umasikini tulionao Kama nchi sasa kama nchi nzima maabara ya kuangalia ugonjwa wa corona ipo moja tuu unategemea nini sasa.

hii vyote husababusha madaktari na wafamacia wetu kutokuwa na uwezo wa kuwa wagunduzi wa madawa mpya. Vilevile utafiti inahitaji uwekezaji wa pesa za kutosha sasa nchi zetu pesa haiwekwi kwenye utafiti Bali imewekwa kubwa kwenye siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gharama za kutafiti dawa moja tu ya ugonjwa mkali inafika trilioni moja bila hata ubishi. Hapo una kila facilities zinazohitajika kama mahabara, mashine na mitambo.

Gharama za kuwa na hizo facilities ni trilioni kadhaa nyingine.
Ongeza operating costs na muda wa kusubiri dawa ipatikane. Imagine Pfizer, kampuni ya madawa ambayo kwa mwaka inaingiza fedha kuliko Tanzania nzima. Kampuni hii imeshindwa kupata dawa ya HIV kwa miaka yote hii mpaka sasa.

Wewe ambaye nchi yako haiwezi tengeneza hata bakuli za kutia mchuzi ndo unataka tuwe na uwekezaji kwenye madawa. Si tutakufa njaa.
 
Tatizo kubwa mfumo wetu WA elimu na ukosefu wa vifaa vya kufundishia na umasikini tulionao Kama nchi sasa kama nchi nzima maabara ya kuangalia ugonjwa wa corona ipo moja tuu unategemea nini sasa.hii vyote husababusha madaktari na wafamacia wetu kutokuwa na uwezo wa kuwa wagunduzi wa madawa mpya. Vilevile utafiti inahitaji uwekezaji wa pesa za kutosha sasa nchi zetu pesa haiwekwi kwenye utafiti Bali imewekwa kubwa kwenye siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfumo wa Elimu wa Tanzania umejikita kwenye kusoma tafiti za wenzetu na kufundsha vilivyo kitabuni..haya mambo start from their making..walete nn wakat wamesoma vilivyomo Elimu yetu ilenge tafiti zaidi jamani hauwezi kuwa nao hao Kama mfumo haundai jamani

Sent using Jamii Forums mobile app

Sidhani kama mfumo wa elimu una tatizo. Watanzania sio watendaji hata wakipewa kila kitu hakuna kitakachofanyika, zitazuka blah blah nyingine tu
 
Back
Top Bottom