Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
HIVI NI KWELI WATANZANIA WANAJUA NINI MAANA YA UHURU WA KUJIELEZA? (FREEDOM OF EXPRESSION )
Tunapo zungumzia juu ya uhuru wa kujieleza tunakua tunamaanisha nini? Hili ndio jambo la kwanza kujiuliza kwa kila Mtanzania kabla ya kuanza kudai uhuru huo wa kujieleza. Ni lazima ujue kua unahitaji nini ili uweke nguvu yako katika kukipata kile ambacho ni haki yako. Mfano unapo jitambua kua unahitaji kupata elimu Ndio ambapo huchukua hatua ya kwenda kuipata elimu unayo ihitaji
Hili nijambo muhimu Sana kujua kua unahitaji nini? Turudi kwenye hoja yetu ya msingi juu ya Uhuru wa kujieleza (freedom of expression).
Tunapo sema uhuru wa kujieleza tunakua tuna maanisha nini? Uhuru wa kujieleza ni haki ya mtu kutoa maoni na mawazo yake juu yakile ambacho anaona kinafaa, maoni haya yanaweza kua katika maandishi, hotuba ama sanaa. Lakini maoni hayo yanapaswa yasiwe yenye kuzuru ama kuzaririsha wengine.(Right to express one's ideas and opinions freely through speech, writing, and other forms of communication but without deliberately causing harm to others'character and/or reputation by false or misleading statements.)hii ndio maana ya uhuru wa kujieleza.
Ukitizama katiba ya Tanzania katika sura ya kwanza 18-(1) inasema bila ya kuathiri sheria za nchi kila mtu anao uhuru wa kua na maoni .Katika kutoa maoni yako kama ilivyo tafsiri yenyewe ya utoaji wa maoni inataka mtoa maoni atoe maoni bila kuathiri haki na utu wa wengine. Katika kulitambua hili katiba ikaweka pia kifungu kinacho mtaka mtoa maoni kuzingatia hayo. Ukisoma kifingu cha 12-(2) cha katiba kinasema.. Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuheshimiwa utu wake. Bado katiba ikaona haitoshi kusema hivyo tu. Bado ikaenda mbali zaidi ikitaka watu wote watambue kua wapo sawa.. Ukisoma kifungu cha 13-(1) cha katiba kinasema, watu wote ni sawa mbele ya sheria. Hii Ndio misingi ya mtu kupata haki yake, yaani akizingatia na kutambua haki na utu wa wengine..
Ukisoma American declaration of independence iliyo wekwa Mwaka 1776 mwezi wa Saba tarehe 4 inasema "We hold these truths to be self-evident, that all men are created equal , that they are endowed by their Creator with certain unalienable Rights, that among these are Life, Liberty and the pursuit of Happiness" .
American declaration of independence imetambua haki na utu wa kila mmoja bila kubagua namna na jinsi alivyo. Na hata tukienda mbali zaidi Katika sheria za umoja wa mataifa. Haki ya kutoa maoni inatambuliwa Katika kifungu cha 19 katika azimio la Kimataifa juu ya haki za binadamu (universal declaration of human rights), pia ukipitia sheria ya kimataifa juu ya haki za binadamu (international human rights law) kifingu cha 19,utaona kua ni kwa namna gani haki ya kila mmoja imezingatiwa..
KINACHO NI SHANGAZA MIMI...
ukisoma huko kote niliko jaribu kuelezea kutokana na maandiko na machapisho niliyo pitia, sijaona mahala pakiwa pameandikwa kua uhuru wa kujieleza unajumuisha kutukana, kejeli na zarau. Hakuna mahala pamesema hivyo.
Watanzania leo tumegeuza uhuru na haki ya kujieleza kua ni uhuru wa kutukana,kukashifu,kuzarau na kuzaririsha wengine. Ndugu zako hakuna haki ya namna hio wala uhuru wa namna hio. Na kama Taifa lolote likiruhusu uhuru wa namna hii basi litakua nitaifa la vichaa na taifa ambalo halikuwi kutokea duniani.
Mungu mwenyewe ametupa uhuru wa kufanya jambo lolote hapa chini ya jua lakini kaweka mipaka na adhabu pia siku ya kiama kwa yule atakaeenda kinyume na matakwa yake. Ndio maana kuna vitabu vitakatifu vinavyoeleza misingi ya kuenenda kama Mungu atakavyo. Vivyo hivyo hata mamlaka za kidunia zimeweka vitabu hivyo (katiba na Sheria) .
MAONI YANGU
kabla ya kudai kile ambacho unakitaka na kilicho kua ni haki yako, lazima ujue na utizame misingi ya namna ya upatikanaji wake. Lakini Kama tutaendelea na mfumo wa matusi kwa madai kua ni uhuru wa kujieleza basi wengi wetu watakabiliwa na mkondo wa sheria. Kuto kujua sheria sio sababu ya wewe kufanya makosa...
c&p.