Ukienda huko vijijini watanzania wanaishi maisha ya tabu na shida sana, wengi wanaishi kwenye nyumba za tembe huku huduma za kijamii kama barabara, maji na hospitali hakuna, akina mama huko wanatumia masaa mengi sana kutafuta maji na hutembea umbali mrefu kupeleka watoto wao kliniki na hospitalini.
Shule za kata nyingi zimekuwa sehemu ya kukuzia watoto na sio kuwapatia elimu, shule nyingi zina uhaba wa walimu, miundombinu mibovu ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia matokeo yake ni asilimia kubwa watoto hawa wanaosoma kwenye mazingira mabovu hufeli na hakuna juhudi zozote za kuwaendeleza.
Ukienda hospitalini dawa hakuna, yaani ukipeleka mgonjwa wako unaweza kufa kwa presha maana huduma ni mbovu watumishi wanafanya kazi kwa mazoea na kila dawa utaandikiwa ukanunue hata glovu za kuzalisha hakuna.
Ukosefu wa ajira ni janga kuu vijana wengi wamejazana mtaani bila kazi, wengi hushinda vijiweni wakibeti lakini serikali haifanyi juhudi zozote kukabiliana na suala hili, wao wanasema wajiajiri lakini hata mazingira ya kujiajiri sio rafiki ikiwemo ukosefu wa mitaji.
Watumishi ambao huwa ndio msaada mkubwa kwa ndugu zao wa vijijini wamebanwa wakabanika, hakuna nyongeza ya mishahara, hakuna kupanda madaraja wala uhamisho lakini vilevile wanahakikiwa kila siku tena wanaenda kwa gharama zao wenyewe na hakuna kurudishiwa. Vilevile kuna watumishi wa umma wamefukuzwa kazi bila kufuata taratibu hata wengine bila kusikilizwa na kuhojiwa na mamlaka za nidhamu zilizopo kwenye utumishi wao.
Uonevu kwa viongozi wa vyama vya kisiasa, ndani ya uongozi huu tumeshuhudia kamata kamata na uonevu wa wazi kabisa kwa viongozi vyama vya siasa na wengine kufungwa kwa hila za kisiasa.
Ukosefu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni janga lingine vijana wengi waliohitimu elimu zao wamenyimwa mikopo wapo mtaani wanazurura tu,
Nchi hii kwa sasa hakuna demokrasia, hakuna uhuru wa bunge (mtu mmoja anapanga bajeti) , ni mtu mmoja tu anaetakiwa kusikika, ni yeye tu anaetakiwa kuwa live na ni yeye tu anaepanga kila kitu ndani ya nchi hii.
Hivi kweli Watanzania wenzangu wameridhika na hali hii, tumekaa kimya kabisa haya yakifanyika, tutamlaumu nani huko mbeleni.