Rudisheni fedha zetu, CDM, haiwahusu!.
[h=2]
Serikali ya CCM na matumizi ya wataalam[/h]Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu matukio mbali mbali yanayojitokeza katika Tanzania chini ya seriakli ya ccm na kubaini kwamba, serikali hii haipo kwa ajili ya kuboresha maisha ya Watanzania. Kwa sababu hiyo hiyo ccm haina uelewa, nia wala lengo la kutumia raslimali zilizopo zenye maslahi ya taifa katika kuleta maendeleo ya taifa zikiwemo raslimali watu.
Hili limethibitika katika maeneo mengi yakiwemo yafuatayo:-
1. Kuwapoteza Wanasiasa kwa kila anayeonyesha nguvu kubwa ya kupinga misimamo ya kifisadi ya serikali ya ccm, bila kujali uwezo, taaluma na umuhimu wa watu hao katika maendeleo ya jamii na taifa.
2. Kuongeza madaraja ya ufaulu wa elimu ili kupunguza alama za ushindi bila kuboresha kiwango cha elimu, kwa ajili ya kuficha aibu ya serikali pasipo kujali madhara ya elimu duni kwa taifa.
3. Wajumbe wa BMK, kujigeuza researchers na wasanifu wa maoni ya wananchi, na watengenezaji wa rasimu ya katiba na serikali kuridhia usanii huo huku ikifahamu kwamba hilo halikuwa jukumu la BMK, na 90% ya wabunge wa ccm hawana uwezo wa kufanya kazi hiyo kitaalamu na zaidi ya yote ni kwamba walijifanya wawakilishi wa maoni ya wananchi kuhusu katiba wakati hawakukusanya maoni hayo kwa asilimia 100. Hii ni zaidi ya dharau na umbumbumbu juu ya umuhimu na thamani ya elimu na utaalamu katika fani.
4. Raisi kutozingatia ushauri wa kitaalamu katika maamuzi na matamshi yake.
5. Raisi kuteua mawaziri na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri kwa misingi binafsi bila kujali elimu na uwezo wa wateuliwa hao.
6. Ccm kuunda katiba ya nchi, inayokataza elimu kuwa kigezo cha sifa za wagombea ubunge bila kujali kwamba wabunge hao ndio wanakazi kubwa ya kutunga sheria na kutoa miongozo ya nchi.
7. Ccm kulazimisha kwamba mawaziri watokane na wabunge, wakati wabunge hawahitaji kuwa na kiwango maalumu cha elimu, na hivyo kuwa na mawaziri wasio na viwango maalumu vya elimu.
8. Ccm kulazimisha teuzi zote zifanywe na raisi pasipo kuwa na mwongozo wala chombo chochote cha kuchuja na kupima wateuliwa wa nyadhifa hizo kwa kuzingatia, elimu, uwezo na sifa zinginezo za wao kushika nyadhifa husika.
9. Kuruhusu muendelezo wa ujenzi holela katika miji bila kujali ramani za maeneo husika, huku serikali ikitumia fedha nyingi kugharimia mipango miji ambayo ina wataalamu waliosoma kwa kodi zetu.
10. Seriakli kutokupima na kuhifadhi maeneo kwa matumizi sahihi ili kutoa mwongozo wakati watu wanapohitaji kufanya matumizi ya ardhi, na badala yake, watu wanatumia ardhi kiholela bila mwongozo, wala kufuata ramani za miji kisha wataalamu kwenda kupima kule watu wameshajijengea kiholela na kuwamilikisha kishaghala bagala. Na hivyo kuwa na miji isiyo na mipangilio as is if hakuna wataalamu wala ramani za mipango ya ardhi inayojulikana mapema.
11. Katika mwendelezo huo, serikali kutumia gharama kubwa mara kwa mara kwenye mazoezi ya bomoa bomoa wakati kuna wataalamu na idara zilizotakiwa kuhakikisha matumizi sahihi ya ardhi kwa kufuata mipango na ramani sahihi. Ikiwa ni pamoja na usimamizi wa compliance badala ya kuruhusu matumizi yasiyo sahihi na baadaye kuliingiza taifa na wananchi kwenye mitafaruku na matumizi ya raslimali yasiyo na mashiko.
12. Kutokuwa na usanifu wa majengo yanayojengwa kwenye shule, polisi, hospital yanayojengwa na wananchi kwa amri ya serikali. Na hivyo kuwa na majengo yasiyo na viwango vya ubora na mwonekano katika maeneo mbali mbali ya serikali.
13. Kutokutumia wahandisi katika kusanifu na kusimamia ujenzi wa shule, hospital, vituo vya polisi, maabara na miundo mbinu mbai mbali inayojengwa na wananchi kwa amri ya serikali, na hivyo kuwa na miundombinu duni inayohatarisha usalama wa maisha ya watumiaji. Mfn. Juzi juzi kuna jamaa kahojiwa ITV kuhusu ubora wa maabara za vodafasta zinazojengwa na wananchi kwa fimbo migongoni, akasema "tunajifunza kwa makosa. Tulikosea majengo ya madarasa ya shule za kata, lakini sasa kwenye hzi maabara tunaboresha zaidi". Mnapojenga vitu kwa gharama kubwa kwa kubahatisha, wataalamu wako wapi?
14. Serikali ya ccm kumiliki na kutoa amri kwa jeshi la polisi kuua raia kinyume na maadili ya taaluma ya polisi, na hivyo kuondoa thamani wala umuhimu wa kuwa na taaluma ndani ya jeshi la polisi.
15. Matumizi mabaya ya fedha za uma bila kujali mipango ya bujeti na hivyo kuwa na budget crisis mara kwa mara na kupelekea seriakli kuingia kwenye madeni yasiyoelezeka na hata kuanza kunyang'anya fedha za wananchi ili kutekeleza miradi ya serikali. Hali inayoodoa maana ya kuwa na mipango ya usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na matumizi ya fedha serikalini.
16. Serikali kutowatumia na wataaluma waliobobea wa fani zote ambao iko nao, wala haiwajengei mazingira sahihi yak u maximize ufanisi wao wa kazi na badala yake kuwa frustrate na kuwafanya wawe underutilized, wakimbilie nchi za nje, na wengine wawe misused. Tuna uhaba wa wahandisi lakini serikali ya ccm inadeliberate kuwatumia wahandisi wachache tulionao kwa masuala ya kisiasa. Mfano Engineer Ndikilo kumfanya mkuu wa mkoa.
Kwa mtindo huu, wa uendeshaji nchi wa seriakli ya ccm, inatupeleka katika mwelekeo sahihi wa kimaendeleo? Ninachelea kusema tulipo na tunapoelekea ambapo karibu tunafika ni mahala penye giza ambapo mambo mengi yanaamuliwa bila utaalamu na huku elimu ikishuka kwa kasi ya kutisha.
Pasipo jitihada sahihi, serikali itarihia hata itikadi za kukataza watu kusoma kama "book haramu", kwa sababu seriakli yenyewe haioni umuhimu wala thamani ya elimu.
Ninaomba tujadili hali hii na mwelekeo wa taifa letu.