Papushikashi
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 10,702
- 12,774
Habari zenu waungwana na bila shaka weekend imeenda mujarabu
Niende moja kwa moja kwenye mada
Juzi kuna rafiki yangu wa siku nyingi tulikuwa tumepoteana kitambo na hatukuwa na mawasiliano, sasa nimeangaika nikawa nimepata mawasiliano yake. Basi nikampigia simu tukawa tunapiga story za hapa na pale, za maisha (kaajiriwa) sasa tukaingia kwenye suala hili la pensheni la asilimia 25...sasa nikawa namtania kwamba hajitahidi kuweka akiba maana akisubiri pensheni huko mbeleni hii sheria itawakamua....
Ghafla nikaona mtu kanikatia simu na baadae kidogo akanitumia sms kwamba eti haya mambo tusiyaongee kwenye simu maana eti serikali inarekodi mazungumzo kwahiyo tutajiweka kwenye matatizo......aisee nilipigwa na butwaa nikasema kweli tumefikia hatua ya kuogopa kiasi hiki mpaka tunashindwa kuongea mambo yanayotuhusu.....
Kweli tumefikia hatua ya kuogopa kiasi hiki?
Karibu kwa mjadala