Hivi kweli Rais wetu huguswi na wabunge wa upinzani kutoka bungeni?

Nafikiri mkuu wa kaya ameridhika na hali ilivyo; hasa kwa sababu imesaidia budgets za wizara mbali mbali na ile budget kuu kupita kwa kishindo. Inawezekana kwa uelewa wake hii ni hali nzuri sana kisiasa. Hukuona jinsi ambavyo wabunge walio wengi, wakiwemo mawaziri wateule walivyomsifu sana NS na kumtaka akalie kiti kila wakati iki mambo yaendelee vizuri; ili zidumu fikra za mwenyekiti tarajali?

Hii ni awamu ya 5, na tutaona na kujifunza mengi; na kwa wengi wetu tutapata maumivu makali wakati utawala ukijinasibu kuudhibiti upinzani.

Ama kwa hakika hizi ni zama tofauti!
Wabunge wa ccm wanachoinjoi kwa ukawa kukaa nje ni kule kutobishiwa wanachosema wakati wa mijadala lakini si ati kwamba ukawa wangekuwapo miswada isingepita. Wamesusa simply because wanajua idadi yao kwa vyovyote haiwezi kubadilisha lolote bungeni unless ccm wawe upande wao but not the other way around. Hata hivyo acha tu ukawa waendelee kukaa nje ili wapate uzoefu kwa ajili ya kufikia maamuzi siku zijazo.
 
kama chama tawala kinakosea ni vigumu wakasema. lakini kama hawa wabunge wanaosusa ndio wenye makosa ni rahisi tu kusema
 
Tatizo binti anakiburi na kujiona anajua kuliko wengine.Nilimsikia Nsazugwanko akiomba kuwepo na marithiano,alijibiwa kama mtoto mdogo,na bado wabunge kama Lusinde wakamzomea,siyo rahisi ngoja tusubiri tuone kama kwenye CCM bado kuna wenye Hekima na Busara.
Ebu tufanye huko ccm hakuna mwenye hekima ama busara ya kuweza kusuruhisha haya mambo. Kwa nini basi tusitumie plan B kwa kuwahusisha wazee wengine wenye busara ili kutatua hili? Tunao wengi sana upande wa pili; Mzee Mtei, Marando, Kingunge, Prof. Safari, Prof. Baregu, Dr. Masha, Mzee Ndesamburo etc hawa wanaweza kuwa wa msaada zaidi kwa upinzani kuliko hata Rais.
 
Abdullah Makame wa FACEBOOK anasema




"Maoni Yangu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa na kiasi. Kiasi kikizidi kinakuwa kinachusha na kinaweza kikaleta madhara. Hata katika maisha ya ndoa Mume na Mke huweza wakapishana mawazo na wakawekeana misimamo ambayo hatimaye hupatikana suluhu.


Nionavyo mimi ni kwamba, muda wa MISIMAMO UMEPITA. Sasa wanaotoka (ambao pia ndio wanaosusia Mambo mbalimbali ikiwemo kupeana salamu) wafanye jitihada ya kuketi na wenzao wanaobakia kwa lengo la KUYAJADILI NA KUYAONGELEA MASUALA mbalimbali watakayoafikiana kuwa yapaswa kujadiliwa.


Huku kususa na kugoma hakutusaidii sisi Watanzania tuliowengi. Sana sana tunaona kwamba viongozi tuliowapigia kura kwa kuwategemea kuwa watatuongoza wameshindwa uongozi. Kwani miongoni mwa sifa za uongozi ni kujadiliana na kubadilishana mawazo; kushawishiana kwa hoja na sio kuwekeana mashinikizo yasiyo na tija kwa yeyote yule.


TUKUBALI KUKAA PAMOJA


TUJADILIANE


TUTHAMINIANE


HAKUNA CHOCHOTE KISICHOONGELEKA."


Leo siongei maana jamaa kamaliza kabisa huyu hii wataelewa wenye akili tu dah.................
 
Mleta mada huyo jamaa ameongea kwa upande mmoja wa kuwalaumu ukawa,
Wewe unasema wakae meza moja kwani hakuna kisichoongeleka,

Na unamaliza kwa kusema huyo jamaa wa fb kamaliza kila kitu.

HUELEWEKI.
 
Madikteta ndivyo walivyo, hujiona wao ndiyo wao na kujali maslahi yao kuliko yale ya nchi. Kule Bungeni jipu mbakaji demokrasi Bungeni Tulia baada ya kumaliza kazi yake ya kuwaadhibiti Wabunge wa UKAWA kuisarambatisha bajeti yao hewa, sasa anadai kachoka!!!! Sijui kwa lipi alilofanya. Ukweli ni kwamba kamaliza kazi yake maana bajeti imeshapitwa na hili Bunge haramu.
Haram ni ww mwenye fikra za kusogeza.
 
Wapinzani huwa siwaelewi hasa wanaidai Demokrasia ambayo ndani ya Vyama vyao haipo. SMH
 
Binafsi namwombea afya njema dr.Tulia ili aliongoze bunge kwa muda wote wa miaka 5 ili nione jeur ya hawa wasakatonge.
 
Kitendo cha wabunge wa Ukawa kutoka nje ya ukumbi wa bunge kilianza kama masikhara, wengi tukidhani kisingeenda zaidi ya wiki moja, lakini kadri siku zinavyoenda kinazidi kuchora picha mbaya na kuweka msitari wa mpaka wa uadui kati ya wabunge wa kambi ya CCM na Ukawa.

Inavyoonekana hali hii itaenda zaidi ya hapo, itasogea mpaka kwa wananchi kama ilivyo kule kisiwani Pemba.

Kinachonisikitisha ni kule kukaa kimya kwa viongozi wetu wastaafu, mzee Ali Hassan Mwinyi na Ben Mkapa na hata mheshimiwa Rais ambaye ndiye tuliyemkabidhi ubaba wa taifa hili na ulinzi na usalama wetu kwa kipindi cha miaka mitano tuliyo nayo. Yaani wako kimya kama kwamba kinachoendelea bungeni hakiwahusu na hawakioni kama ni kitendo kinacholichafua na kulitia aibu taifa letu kimataifa.

Nawaomba wazee wetu mjitokeze na mseme neno juu ya hiki kinachoendelea bungeni, hivi tunawatunza kwa kodi yetu ili mle tu na kuwa wageni wa heshima kwenye makongamano lakini msilisaidie taifa hata pale mnapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo? Mbona mwaka 1994 wakati wa utawala wa Mwinyi, mwalimu aliingilia kati tena kwa ukali alipoona wabunge wa kundi la G55 wa bunge la JMT linapigania kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika ndani muungano.

Wazee wetu jitutumueni mliokoe taifa hili bado mkingali hai lisiparaganyike mkiwa mnaangalia kama kwamba ni jambo lisilowahusu.

Mshauri kabisa afute na matokeo yote ya majimbo yaliyochukuliwa na upinzani aweke wa chama chake tukufu
 
Sidhani kama nia ni kumlaumu Rais, ninachosema ni kwamba mheshimiwa Rais kama kiongozi wa nchi anaweza kutoa maelekezo kwa nia nzuri tu ya jinsi ya kuumaliza mvutano uliopo baina ya wabunge wa Ukawa na naibu spika.
Mimi naamini juhudi zimefanyinyika lakini ni vyema tukawaekewa wapinzani kwa nia na malengo yao.mfano hakukuwa na sababu ya kususia hotuba ya rais alipozindua bunge sasa kwanini hawataki kufuata kanuni na taratibu za mbunge ambazo ziliwekwa na wabunge wenyewe.
 
Mimi Mwanakijiji nadhani unauelewa mkubwa sana kuhusu siasa na wanasiasa wa Tanzania.
Kumbuka kuwa hivi vyama vya siasa vinaelekea kwenye mabadiliko ya uongozi wa kisiasa.
Kwa hiyo mambo mengine yanafanywa kwa kuangalia kiongozi anayekuja anataka nini.
Haya yanafanywa kwa makusudi iwe ni kwa CCM au upinzani kila mmoja anamahali anapokosea. Lakini mwenye dhamana kubwa ya amani ya taifa hili ni Rais na serikali yake na chama chake kinachotawala.

Sasa hii staili wanayofanya CCM ndani na nje ya bunge ni kutaka kujikomba ili kila mmoja aonekane kuwa anaendana na awamu ya tano.
Yani watu hawataki tena kusimamia katiba bali wanasimamia mihemko yao kwa kujifanya wanamuunga mkono Rais. Leo hii hakuna mtendaji wa serikali anayesikiliza mtu na kubaini chanzo cha tatizo zaidi ya kutumia nguvu na mabavu hata kwa watu ambao sio majipu.

Mtu anatoa maoni yake anazuiliwa kwa nguvu kubwa kwa sababu gani?
Majipu ndiya yanayomaliza fedha za umma na sio watu wanaotoa maoni yao au kuongea kwa hisia kali. Hawa hawana madhara kwenye uchumi wetu na huduma bora.
Tunataka mapambano yaelekezwe kwa wakwepa kodi, wauza madawa, viongozi wa umma wenye kujichukulia tenda za umma kwa upendeleo, majambazi, magaidi, wenye vyeti feki na wala rushwa.
Hawa ndio wa kupambana nao kwa mikakati mikali. Lakini chaajabu vyombo vyote vya dola na bunge wameweka nguvu zote kupambana na wanasiasa wa upinzani.
Watu wanashinda kwenye mitandao kutafuta nani amemkashfu rais badala ya kuangalia wezi wa mabenki kwa njia za mitandao!!

Sasa hapo ndio kumsaidia rais kutumbua majipu?. Bunge linakaribia kuisha lakini hakuna mbunge hata mmoja wa CCM aliyefanya kama alivyofanya Makonda kwa kumtaja mtu hadharani kuwa ni jipu ili Rais achukue hatua ya kulitumbua hadharani.

Lakini wapinzani wakitaka kutaja majipu wanazuiliwa na kuambiwa wamekiuka kanuni mara sijui waziri amelalamika na kuzuia hoja hiyo na ndiye anayesikilizwa.

Sasa imekua kupambana na upinzani na kuwatukana wapinzani ndio kumsaidia rais tofauti na rais alivyotegemea asaidiwe na CCM na wabunge wake kutaja majipu.

Mfano wa rais kuwa na nafasi ya kuzuia hujuma zinazofanywa na bunge dhidi ya wapinzani ni ule uchaguzi wa mamea wa jiji la Dsm.
Kama sio Mh. Rais kukemea na kuonyesha kutokufurahishwa kwake na hujuma za CCM mpake leo meya wa jiji asingepatikana na huenda ungefanyika umafya wa kumpata na amani ya jiji ingekua kwenye hali tete.
Alitumia busara na kukataa dhulma kwenye kulazimisha ushindi kwa wale waliokua wanafikiri kuwa wanamuunga mkono kwa namna yoyote.

Tusilazimishe rais kuungwa mkono kwa namna yoyote kwani hata yeye mwenyewe hapendi hizo namna mbaya na za kinafiki za kumuunga mkono.

Mkuu ! Mimi naona umetoa hoja nzuri sana ! Lakini kuna sehemu kama kidogo una ji contradicts!

Ni ndefu lkn mi nitagusia mle tu ambako nimeona kuna utamu wa hoja na pengine negatively au positively , kuta rainforce nakosimamia mimi !

Kwa mfano ! Nitarudi
 
HAGUSWI ! ila nawasihi saana wasiombe usaidizi kwa ISS maana jamaa wanatumia Mabomu sio Risasi .
 
Matusi ya nguoni wanayowatukana Wabunge wa UKAWA kila wanapotoka Bungeni. Hata Bunge la katiba pia wajumbe baadhi wa CCM walirusha matusi ya makubwa ya nguoni hakuna aliyetia neno.

Hebu toa mfano kosa la mbunge wa ccm
 
RAIS JPM AGUZWE KWA LIPI AACHE KUWANGAIKIA WANANCHI NA TAIFA KWA UJUMLA HALAFU WANAJITOKEZA WATU WANAOTAKA AKWAME KWAJILI YA KUTETEA VYAMA VYAO NA SI WANANCHI KISINGIZIO KWA NAIBU SPIKA KUTOKA KWAO WALA HAKUSIANI NA MASLAHI YA WANANCHI,ILA VINAHUSIANA NA MASLAI YA VYAMA VYO.NASHUKURU JPM KESHA LIONA HILO.
Unapaswa kuwa muelewa ndugu, kitendo cha wabunge wa ccm kuwa wengi bungen hakimaanishi kuwa kila wanachokifanya na kuamua ni sahihi,
Kitendo cha naibu kujaribu kunyamazisha upinzani pindi unapoikosoa serikari au kuleta miongozo inayogusa maisha ya wananchi siyo sahihi na kinapaswa kupingwa na watu wote wennye uelewa,
Binafsi naona kama Raisi anakosea kupuuzia hili suala kwasababu wabunge wa upinzan pia ni sehemu yake kama kiongozi mkuu, kiberiti ni kidogo sana lakin moto wake huwa ni mkubwa sana,
Kitendo hiki kinaonekana kidogo sana lakin impact zake ni kubwa sana, hasa kiusalama na kiuchumi,
 
Back
Top Bottom