Hivi kweli Rais wetu huguswi na wabunge wa upinzani kutoka bungeni?

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Kitendo cha wabunge wa Ukawa kutoka nje ya ukumbi wa bunge kilianza kama masikhara, wengi tukidhani kisingeenda zaidi ya wiki moja, lakini kadri siku zinavyoenda kinazidi kuchora picha mbaya na kuweka msitari wa mpaka wa uadui kati ya wabunge wa kambi ya CCM na Ukawa.

Inavyoonekana hali hii itaenda zaidi ya hapo, itasogea mpaka kwa wananchi kama ilivyo kule kisiwani Pemba.

Kinachonisikitisha ni kule kukaa kimya kwa viongozi wetu wastaafu, mzee Ali Hassan Mwinyi na Ben Mkapa na hata mheshimiwa Rais ambaye ndiye tuliyemkabidhi ubaba wa taifa hili na ulinzi na usalama wetu kwa kipindi cha miaka mitano tuliyo nayo. Yaani wako kimya kama kwamba kinachoendelea bungeni hakiwahusu na hawakioni kama ni kitendo kinacholichafua na kulitia aibu taifa letu kimataifa.

Nawaomba wazee wetu mjitokeze na mseme neno juu ya hiki kinachoendelea bungeni, hivi tunawatunza kwa kodi yetu ili mle tu na kuwa wageni wa heshima kwenye makongamano lakini msilisaidie taifa hata pale mnapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo? Mbona mwaka 1994 wakati wa utawala wa Mwinyi, mwalimu aliingilia kati tena kwa ukali alipoona wabunge wa kundi la G55 wa bunge la JMT linapigania kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika ndani muungano.

Wazee wetu jitutumueni mliokoe taifa hili bado mkingali hai lisiparaganyike mkiwa mnaangalia kama kwamba ni jambo lisilowahusu.
 
Huu sio utawala wa siasa za Maigizo na kukaribishana juisi Ikulu.... upinzani ubadili aina ya siasa zake la sivyo tutakuwa tunawasikia wakati wa bunge tu.

Wakijenga hoja watasikika na wananchi tutawaelewa lakini wakiamua kutafuta umaarufu na kugonga headline hawafiki popote .

Sioni dalili kwa Mbowe na Magufuli wakigongeana glasi za juisi Ikulu kwa siku za karibuni.

Tuache kuishi kwa mazoea.!
 
Hili wala halitakiwi kuingiliwa na Mh Rais,
Bunge lina wazee wenye busara ukitoa unazi wa kishabiki wa wabunhe wa Ccm. Pia kuna kamati ya maadili lakini bado ndio ule unazi umetawala hii kamati.
Pia kuna Mh Waziri Mkuu kama kiongozi wa shughuli za serikali bungeni lakini nae sijui anawaza nini. Mimi naamini pamoja na ipole wake Mh. Pinda hii hali haingefika hapa. Alikuwa mstaarabu na alijua umuhimu wa iwakilishi wa upinzani kwenye bunge la vyama bingi. Sijui inamshinda nini Mh Kassim Majaliwa Waziri mkuu na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Maana hii issue ni ndogo sana kama ustarabu utatumika.
 
Huu sio utawala wa siasa za Maigizo na kukaribishana juisi Ikulu.... upinzani ubadili aina ya siasa zake la sivyo tutakuwa tunawasikia wakati wa bunge tu.

Wakijenga hoja watasikika na wananchi tutawaelewa lakini wakiamua kutafuta umaarufu na kugonga headline hawafiki popote .

Sioni dalili kwa Mbowe na Magufuli wakigongeana glasi za juisi Ikulu kwa siku za karibuni.

Tuache kuishi kwa mazoea.!
Kaka umeongea ukweli...ukweli mtupu. Siasa za kutengeneza matukio ili utengeneze headline kwenye magazeti zimepitwa na wakati.
 
hao wanaotoka hawajielewi! na naombea raisi magufuli aendelee kuwapotezea tuu
Hapana, kama wanaotoka nje hawajielewi wasitufanye nasi tuonekane hatujielewi.
Tuwe waungwana kuliko wao kwa kutazama kinachowakera tukifanyie kazi.

Kama kweli Dk Tulia Ackson ni tatizo, kwa nini tukubali mtu mmoja alipasue bunge. Watanzania tuache ushabiki unaoweza kutugharimu mbeleni.
 
Madikteta ndivyo walivyo, hujiona wao ndiyo wao na kujali maslahi yao kuliko yale ya nchi. Kule Bungeni jipu mbakaji demokrasi Bungeni Tulia baada ya kumaliza kazi yake ya kuwaadhibiti Wabunge wa UKAWA kuisarambatisha bajeti yao hewa, sasa anadai kachoka!!!! Sijui kwa lipi alilofanya. Ukweli ni kwamba kamaliza kazi yake maana bajeti imeshapitwa na hili Bunge haramu.

Kitendo cha wabunge wa Ukawa kutoka nje ya ukumbi wa bunge kilianza kama masikhara wengi tukidhani kisingeenda zaidi ya wiki moja, lakini kadri siku zinavyoenda kinazidi kuchora picha mbaya na kuweka msitari wa mpaka wa uadui kati ya wabunge wa kambi ya CCM na Ukawa.

Inavyoonekana hali hii itaenda zaidi ya hapo, itasogea mpaka kwa wananchi kama ilivyo kule kisiwani Pemba.

Kinachonisikitisha ni kule kukaa kimya kwa viongozi wetu wastaafu, mzee Ali Hassan Mwinyi na Ben Mkapa na hata mheshimiwa Rais ambaye ndiye tuliyemkabidhi ubaba wa taifa hili na ulinzi na usalama wetu kwa kipindi cha miaka mitano tuliyo nayo. Yaani wako kimya kama kwamba kinachoendelea bungeni hakiwahusu na hawakioni kama ni kitendo kinacholichafua na kulitia aibu taifa letu kimataifa.

Nawaomba wazee wetu mjitokeze na mseme neno juu ya hiki kinachoendelea bungeni, hivi tunawatunza kwa kodi yetu ili mle tu na kuwa wageni wa heshima kwenye makongamano lakini msilisaidie taifa hata pale mnapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo. Mbona mwaka 1994 mwalimu aliingilia kati alipoona wabunge wa kundi la G55 wa bunge la JMT linapigania kuanzisha serikali ya Tanganyika ndani muungano.

Wazee wetu jitutumueni mliokoe taifa hili bado mkingali hai lisiparaganyike mkiwa mnaangalia kama kwamba ni jambo lisilowahusu.
 
Seriously..kwani wana ugomvi na Rais..wao wanahitaji juomba kukaa chini na Spika..waelewane. Tunataka kumlaumu Rais kwa mambo ya kumtafutia lawama tu.
Sidhani kama nia ni kumlaumu Rais, ninachosema ni kwamba mheshimiwa Rais kama kiongozi wa nchi anaweza kutoa maelekezo kwa nia nzuri tu ya jinsi ya kuumaliza mvutano uliopo baina ya wabunge wa Ukawa na naibu spika.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo la upungufu wa elimu kwa wengi wa wawakilishi wetu, na Rais analiona hilo na ndio maana haingilii kati! Watu walizoea kuishi bila kufuata sheria na kanuni za nchi ktk katiba yetu inayolalamikiwa, sasa sheria zikizingatiwa na kutekelezwa inaonekana kama udikteta, wenye elemu ya hapa na pale kama yangu hapa, tunatafuta vifungu vinavyotubeba ili tukosoe utendaji! Uhuru bila mipaka ni uendawazimu! Rais anasema serikali yake, hii ni kwa kuwa popote akiharibu musimamia kwa maslahi ya taifa kwa kipindi chote cha utawala wake, yeye ndie wa kubeba lawama! Utamtoaje kwenye mihimili yote? Yeye serikali kwa maana ya taasisi ya rais, ni yake, mahama ni yake na bunge ni lake! Mambo yakiharibika kwenye utawala wake, kila mtu atamlaumu rais!
 
Kitendo cha wabunge wa Ukawa kutoka nje ya ukumbi wa bunge kilianza kama masikhara, wengi tukidhani kisingeenda zaidi ya wiki moja, lakini kadri siku zinavyoenda kinazidi kuchora picha mbaya na kuweka msitari wa mpaka wa uadui kati ya wabunge wa kambi ya CCM na Ukawa.

Inavyoonekana hali hii itaenda zaidi ya hapo, itasogea mpaka kwa wananchi kama ilivyo kule kisiwani Pemba.

Kinachonisikitisha ni kule kukaa kimya kwa viongozi wetu wastaafu, mzee Ali Hassan Mwinyi na Ben Mkapa na hata mheshimiwa Rais ambaye ndiye tuliyemkabidhi ubaba wa taifa hili na ulinzi na usalama wetu kwa kipindi cha miaka mitano tuliyo nayo. Yaani wako kimya kama kwamba kinachoendelea bungeni hakiwahusu na hawakioni kama ni kitendo kinacholichafua na kulitia aibu taifa letu kimataifa.

Nawaomba wazee wetu mjitokeze na mseme neno juu ya hiki kinachoendelea bungeni, hivi tunawatunza kwa kodi yetu ili mle tu na kuwa wageni wa heshima kwenye makongamano lakini msilisaidie taifa hata pale mnapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo? Mbona mwaka 1994 wakati wa utawala wa Mwinyi, mwalimu aliingilia kati tena kwa ukali alipoona wabunge wa kundi la G55 wa bunge la JMT linapigania kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika ndani muungano.

Wazee wetu jitutumueni mliokoe taifa hili bado mkingali hai lisiparaganyike mkiwa mnaangalia kama kwamba ni jambo lisilowahusu.
RAIS JPM AGUZWE KWA LIPI AACHE KUWANGAIKIA WANANCHI NA TAIFA KWA UJUMLA HALAFU WANAJITOKEZA WATU WANAOTAKA AKWAME KWAJILI YA KUTETEA VYAMA VYAO NA SI WANANCHI KISINGIZIO KWA NAIBU SPIKA KUTOKA KWAO WALA HAKUSIANI NA MASLAHI YA WANANCHI,ILA VINAHUSIANA NA MASLAI YA VYAMA VYO.NASHUKURU JPM KESHA LIONA HILO.
 
Hapana, kama wanaotoka nje hawajielewi wasitufanye nasi tuonekane hatujielewi.
Tuwe waungwana kuliko wao kwa kutazama kinachowakera tukifanyie kazi.

Kama kweli Dk Tulia Ackson ni tatizo, kwa nini tukubali mtu mmoja alipasue bunge. Watanzania tuache ushabiki unaoweza kutugharimu mbeleni.
tatizo hoja zao hazina maana, Dr.tulia ni mchapakazi na anapenda kufuata kanuni na taratibi kitu ambacho viongozi qa chadema hawafuati!! by the way mm ni shabiki wa lowassa, natamani awe mwenyekiti chadema, mbowe anatupoteza!
 
Kumbe na wewe ni wale wale?
 
Wazo lako zuri sana lakini unadhani yupo mwenye kuliona kwa jinsi wewe ulivyoliona? Tumwombe Roho Mtakatifu atusaidie ktk hili otherwise tulie tu
 
Back
Top Bottom