Hivi kwanini wanawake hamtosheki?

Hivi kwanini wanawake hamtosheki?

Lakini umemuangalia nje vizuri?huwenda kaenda kumalizia kufua
 
Kwa kuwa asha ondoka mwenyewe sina mengi ya kukushauri, endelea na maisha tafuta mke mwingine oa.
Usipo fuata huu ushauri utakuwa Bashite sasa
 
Mi nahic cjui kaenda kwa Hugo baby wake inauma
Honestly hilo ndilo jibu lililobaki . .kama wazazi wake hawajui alipo basi atakuwa kwa huyo baby mwingine

Ni ukweli mchungu,unauma ila hakuna namna zaidi ya kukubali hali halisi na kupambana tu

Cha kufanya sasa hivi kusanya kila kilicho chake peleka kwao ili asipate sababu ya kurudi kwako

Pole sana ngosha wa kule Mwanza
 
Wanabodi,

Yamenikuta mwanaume mwenzenu, yaani shemeji yenu aliyonifanyia sitakaa nisahau, Juzi niliamua kujipumzisha nyumbani sasa nikiwa busy kuangalia movie simu ya wife ikaita maana alikua ameiacha chaji wala mimi sikujua kama kaiacha chaji kutokana na mimi kutopenda kufatilia simu ya wife sikutaka kujua ni nani anapiga.

Huyo mtu aliendelea kupiga sasa mototo wangu mdogo anamazoea simu ikiita hua anaichomoa chaji na kumpelekea mwenye simu dah mwanangu akaichomoa ile simu kutoka nayo nje ampelekee mama yake.

Bahati mbaya mtoto akajikwaa akaanguka na simu mimi ikabidi niwahi kuangalia kama ameumia na nikajua hata simu itakua imeshavunja kioo si unayajua ma simu ya tach, dah dogo alikua poa na simu ilikua poa ila wakati nikiwa naiangalia simu kama hajapata damage ndo SMS ikaingia, mimi nikaona niicheki ndo nakutana na ujumbe baby mbona hupokei simu, yaani roho ilinidunda ghafla mapigo ya moyo yalibadilika maana sikutarajia kuona kitu kama hicho kwenye simu ya wife.

Nikajikaza kisabuni nikamjibu nilikua busy baby unasemaje? Jamaa akajibu yaani nimekumbuka mambo uliyonipa, sikutaka hata kuendelea nae nikaona nimwite wife maana alikua nje anafua nikamwonesha zile sms alicho kifanya ni kuondoka kusiko julikana mpaka sasa sijui aliko, hata ndugu zake nimewataarifu hawajamuona.

Jamani naombeni ushauri wenu maana sijielewi nifanye nini.
Kwahiyo hilo jambo nalo unaona ni la kushauriwa??haya basi mwambie akusamehe kwa kuwa umesoma msg zake.
 
Ngoja nukushauri. Tatizo ni huyo mtoto siku nyingine akibeba simu mwambie asianguke anguke kwani ana kifafa?
 
Back
Top Bottom