Habari wakuu,
Nimekaa nikajiuliza nikawaza nikaona kwa upande fulani sisi watu wa mafia kuna sehemu tumekosea maana huku hakuna maendeleo yoyote na hali inazidi kuwa mbaya hakuna usafiri wa uhakika ambao hata Serikali hauna mpango wa kutuletea usafiri wa uhakika.
Yaani tupo tupo tu kama hatutakiwi au tunajilazimisha au CCM ndio wanatufanya hivi maana hata kiongozi yeyote ukimuuliza kuhusu usafiri wa uhakika hawana majibu au mnataka tuangamie ndio mtupe pole bora uchaguzi ufike tutaongea kwa meno hata huo usafiri tunaotumia nauli wanapanga wenye boti ilimradi na sie tumo.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Wananchi wa Mafia hamuna akili..... Hamujielewi.
1.kimbau alikua mbunge miaka 30,sababu ya kutojitambua kwenu
2.Buji akaja kajipigia mahelaa miaka 15
3.Dau nae namuona hana dalili ya kuondoka.
Chagueni mbunge mzawa, Chagueni mbunge msomi, Chagueni upinzani....
Acheni uchawi vile vile..... Zikija boti classic munaziroga....
Kama kikwete alikaa madarakani miaka 10 mukashindwa kumtumia sahauni kabisa kuhusu maendeleo.
Mafia kuna mahoteli mengi na uvuvi..... Jiulizeni ushuru unaenda wapi?..... Madiwani wenu wameishia la saba vichwa box wamejaa usanii tu.
........ Viongozi wa serikali Mafia, wakuu wa wilaya na wakurugenzi hawawezi watetea, kwa nini?,..... Sababu wanalipwa per diem na tiketi za ndege ndefu sana..... Ambayo kama hizo nauli zingesema zinunue boti mungekua na Azam fast ferries kama 10 hivi.
Kikubwa jitambueni kama raia.
Pelekeni watoto shule achaneni kurithishana mashamba ya minazi, kupasa dagaa na kuchokoa kaa bwejuu na jibondo.
Sent using
Jamii Forums mobile app