Zee Korofi
JF-Expert Member
- Oct 5, 2021
- 1,612
- 1,410
Yaani Wabongo amsha amsha kwenye issues za msingi hawana kabisa, kisiasa ni kondoo ambao wanapelekeshwa kwa kila kitu. Sioni Wabongo mfano wa miamba ya akina Aristotle na Plato, mifano ya akina Lincoln, mifano ya watu wagumu waliowahi kufanya makubwa duniani.
Wengi ni hodari kwenye upuuzi usio na tija, na ubishani wa kijinga. Kila kitu ubishi ubishi tu, huku muda unakwenda na kazi haifanyiki, maendeleo zero, vijana wamekalia kubishana mitandaoni tu, kutoa hoja nyiiingi kana kwamba zitatekelezeka in real life, mwisho zero.
Yaani mtu anajifia ndani au kwenye hospitali ndogo kulinganisha na magonjwa anayoumwa. Bila msaada wowote kutoka kwa ndugu na marafiki. Michango ya maana hamna, ila akifariki anazikwa kwa gharama, ndugu wazito mno wanakuja. Wengine kutoka hata nje ya Afrika, wenye pesa kede kede.
Watu watakula, watasaza, watazika. Ila ukiumwa utaambulia "pole" tu ya mdomo, wachache watakuuguza mpaka utakapokata roho, hawa Mara nyingi ni mama yako na baba yako. Ukifa mpaka mjomba wako wa SA atatuma ndege ikupeleke kijijini, na baba yako mdogo pale MOI atatoa milioni 10 kwa ajili ya chakula na kutengeneza ukumbi wa msiba.
Binamu yako wa USA atakuja na kutoa 20000000 kwa ajili ya rambi rambi kwa wazazi wako na kuwajengea pa kujisitiri
Mara baada ya kutafakari haya usiku mmoja huku machozi yakinilenga lenga, niliamua kwa dhati kutochangia TENA sherehe yoyote au ndoa. Niliapa kuchangia matibabu tu badala ya sherehe na harusi. Sijui kama nipo au sipo sahihi, ila ni miaka 8 sasa sitoi mchango wa harusi au sherehe yoyote, pia hata harusi yangu sitoomba mchango wa yeyote.
Kifupi tunapigiana chapuo na kuhimizana kwenye vitu vya kipuuzi au vyenye kuleta maumivu. Ni rahisi mtu kukushawishi uingie kwenye ndoa kisa yeye anaumia kwenye ndoa ila ana-fake ili na wewe uingie uteseke.
Ni hatari na upumbavu!