Hivi kwanini ukihoji mambo fulani juu ya Dr. Slaa na Mbowe unaonekana msaliti?

Tsakhodegha

Member
Mar 16, 2013
27
13
Wanajavi natanguliza samahani kwa watakao kwazika kwa namna moja au nyingine na hili....binafsi nikiwa kijana mpenda mabadiliko ktk nchini yangu hii napata shida sana na ni muda sasa kwanini mtu ukijaribu kuhoji kwa nia njema kabisa na kwa mantiki jambo lolote juu ya chadema kwa ujumla wake unaonekana mpinga ukombozi, msaliti, kibaraka wa ccm na mengine ya aina hiyo.

Hivi ni kweli kwamba vijana tulio wengi tuna mapenzi ya kufa na kuzikana na vyama vyetu vya siasa kuliko nchi yetu? Hivi haya mapenzi mazito kwa vyama vyetu vya siasa yametufanya tuache kutumia mantiki katika kuhoji mambo badala yake hisia?

Niwaombe vijana wenzangu kwa mwendo huu hatutafika embu tuweke maslahi mapana ya nchi yetu mbele then vyama vyetu vya siasa.....na huu utamaduni wa kuogopa kukosoa jambo kisa nitaonekana msaliti, natumika haujengi vyama vyetu bali unavibomoa.....daima tusimamie hoja za msingi regardless zimetoka upande gani.......nimalizie kwa kusema dr.slaa na mbowe ni binadamu wala si malaika hivo panapotakiwa kukosolewa wakosolewe na wakosoaji wasionekane matarishi......

Ni mawazo tu.
 
wala c dhambi,na wala vijana hawako ivo,vijana wanapenda sana sera zao na si kuwapenda wao,jiulize swali hili.ni wanasiasa wangapi waliopo hapa tz lakini mbona hawapendwi?jibu ni dhamira walonayo hao wanasiasa,sasa cc vjana tunawaona sio tu kwa maskio na macho lahasha bali hata kwenye midahalo wapo juu sana rejea mdahalo wa mbowe na wasira utapata majibu.kwaheri gamba.
 
mimi niko tayari kupigana vita ya aina yoyote kuona ccm inaenda jehanam.. Niko tayari kufa kuhakikisha cdm inaongoza nchii hii... hata kama sitakuwepo wajukuu wangu watafurahia life!
 
Ccm inatakiwa ipigwa vita kuanzia nchi kavu, angani.. mpaka majini..mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya, kata kwa kata, kitongoji kwa kitongoji, kijiji kwa kijiji,mtaa kwa mtaa, nyumba hadi nyumba, uvungu hadi darini.. Ni vita tuu.. haya makamanda kazi kwenu.. Ondoeni uovu.. leteni baraka.. Ondoeni giza leteni nuru, ondoeni shetani leteni Mungu.. Kazi kwenu MAKAMANDA WOTE WA NCHI KAVU ANGANI HADI MAJINI..
 
GOOD ARGUEMENT; hii ni mojawapo ya sababu zinazonifanya nisitishe kuchangia mambo yanayohusu CHADEMA jamvini ingawa ni MWANACHAMA. Washabiki wamekuwa wengi na hawachukui hata sekunde ku "reason" mambo, zaidi ya matusi na kejeri hata kwa mambo ya muhimu yenye malengo ya kujenga chama.

Naamini kuna wanachama wengi sana nikiwemo mimi ambao tumeanza kuhoji uamuzi wetu wa kuendelea kuwa MEMBER OF THE PARTY. Na ni kwa nia njema inayoambatana na mranganisho wa mategemeo Vis Matokeo. Washabiki ni watu hatari sana Mh Mrema ni shahidi.Chadema ilianza na wanachama, tena wenye malengo yanayofanana na wenye mwelekeo wa kiukombozi na ikafanikiwa sana.Leo chama kinakumbatia washabiki kuliko wanachama na kimewapa baadhi uongozi.Hii ni kwa sababu wanachama hu-hoji utendaji wa viongozi na mwelekeo wa chama, lakini Washabiki husifia na kupamba kila lisemwalo au litendwalo na viongozi.
WANACHAMA tunaliona hili mkuu, na LINATUSIKITISHA
 
kwan unataka tukazane kumshambulia mbowe au slaa na tuache wanaotunyonya.

unanishawishi vp nishambulie chadema na niwaache wanaoleta mgao wa umeme?
wenye hela uswis, ufisadi wa kutisha na mengine.
ebu niambie uhusiano wa kufer kwa kidato cha 4 na mbowe au slaa, ni waz kwamba huwez kusema chochote hapo
sasa sisi kama wananchi tunawaona nyinyi mnaojitokeza kukwamisha ustawi wa chadema mnatumika coz kwa mtu timamu lazima atashambulia ccm coz wana uhusiano wa moja kwa moja na maisha duni hapa tanzania
ebu tuambien nyinyi sasa mnaotaka kushamburia watetez hawa mmefurahishwa nn na ccm
 
Wanajavi natanguliza samahani kwa watakao kwazika kwa namna moja au nyingine na hili....binafsi nikiwa kijana mpenda mabadiliko ktk nchini yangu hii napata shida sana na ni muda sasa kwanini mtu ukijaribu kuhoji kwa nia njema kabisa na kwa mantiki jambo lolote juu ya chadema kwa ujumla wake unaonekana mpinga ukombozi, msaliti, kibaraka wa ccm na mengine ya aina hiyo.

Hivi ni kweli kwamba vijana tulio wengi tuna mapenzi ya kufa na kuzikana na vyama vyetu vya siasa kuliko nchi yetu? Hivi haya mapenzi mazito kwa vyama vyetu vya siasa yametufanya tuache kutumia mantiki katika kuhoji mambo badala yake hisia?

Niwaombe vijana wenzangu kwa mwendo huu hatutafika embu tuweke maslahi mapana ya nchi yetu mbele then vyama vyetu vya siasa.....na huu utamaduni wa kuogopa kukosoa jambo kisa nitaonekana msaliti, natumika haujengi vyama vyetu bali unavibomoa.....daima tusimamie hoja za msingi regardless zimetoka upande gani.......nimalizie kwa kusema dr.slaa na mbowe ni binadamu wala si malaika hivo panapotakiwa kukosolewa wakosolewe na wakosoaji wasionekane matarishi......

Ni mawazo tu.

Mnajitahidi kweli kujiunga humu ili tu kukamilisha misheni yenu ya kuitokomeza CHADEMA ndani ya mwaka huu wa 2013 kama alivyoaihidi yule binadamu wa kale!
Mtahangaika sana lakini naamini hamtafanikiwa...NIAMINI!
 
jibu la swali lako ni rahisi sana,chadema kinaendeshwa na falsafa ya ''people's power''na wanachama ndio waamuzi,kumkosoa mbowe au slaa ni usaliti wananchi wote wapenda mabadiliko kwa sababu mbowe na slaa wanasilisha mawazo ya wananchi hao,chadema siyo kama kile chama chenye falsafa ya ''zidumu fikra za mwenyekiti wa..''
 
Hivi mtu anakuja hapa jamvini na kusema yeye ni Chadema halafu analeta hoja kama hizi hapa chini, unafikiri kwanini wafuasi wa chadema wasikuite msaliti(Na Mwisho wa siku anarudi CCM kwa mbwembwe), kwa mfano

1/Slaa kachukua mke wa mtu!!

2/Slaa katumwa na kanisa katoliki!!

3/Slaa alimtaka kimapenzi
Secretary wake.

4/Slaa anamiliki kadi ya CCM iliyolipiwa mpaka 2016.

5/Slaa ni pandikizi la CCM!!

6/Slaa iliiba fedha za kanisa katoliki wakati wa ziara ya papa!!

7/Mbowe sio mwanasiasa bali ni DJ na mchezesha Disco tu!!

8/Mbowe anaendesha chama kikabila!!

9/Mbowe elimu yake ni darasa la saba!!

10/Mbowe na Slaa ndio wanaongoza mipango ya mauaji dhidi ya raia!!

*Embu kaa kufikiri tu hizo hoja hapo juu zilivyo za kijinga, halafu tathmini na kufikiri kama mtu anayeleta hoja hizo kama atakuwa ameonewa kama ataitwa Msaliti na wanaChadema
 
Tuko pamoja mkuu...binafsi naikubali sana cdm bt kwa namna tunavyokwenda naona kuna kila sababu ya kujitafakari kama tupo kwenye njia sahihi au tumeanza kuhama na kuelekea porini...
 
Hawa ni zaidi ya mitume hawana makosa ni marufuku kuwakosoa wala kuhoji.

Ukiwahoji tu unaitwa masalia au umetumwa.

Subiri matusi kutoka kwa wafuasi wao.
 
Njaa mbaya sana
Unajua makamanda siku hizi nasikia wanashinda kwenye show room za magari wanauliza yatakuwa bei gani ifikapo 2015 kwani wana uhakika wa ulaji
 
nenda kahoji mambo ya dhaifu mbona mengi tu! au umesahau mambo ya ze unono? magamba mna shida nyie kili kukicha ni kubadili ID zenu. masalia wakubwa nyie.
 
Hivi mtu anakuja hapa jamvini na kusema yeye ni Chadema halafu analeta hoja kama hizi hapa chini, unafikiri kwanini wafuasi wa chadema wasikuite msaliti(Na Mwisho wa siku anarudi CCM kwa mbwembwe), kwa mfano

1/Slaa kachukua mke wa mtu!!

2/Slaa katumwa na kanisa katoliki!!

3/Slaa alimtaka kimapenzi
Secretary wake.

4/Slaa anamiliki kadi ya CCM iliyolipiwa mpaka 2016.

5/Slaa ni pandikizi la CCM!!

6/Slaa iliiba fedha za kanisa katoliki wakati wa ziara ya papa!!

7/Mbowe sio mwanasiasa bali ni DJ na mchezesha Disco tu!!

8/Mbowe anaendesha chama kikabila!!

9/Mbowe elimu yake ni darasa la saba!!

10/Mbowe na Slaa ndio wanaongoza mipango ya mauaji dhidi ya raia!!

*Embu kaa kufikiri tu hizo hoja hapo juu zilivyo za kijinga, halafu tathmini na kufikiri kama mtu anayeleta hoja hizo kama atakuwa ameonewa kama ataitwa Msaliti na wanaChadema
Kwani kuna uongo hapo,yani watu kusema ukweli imekua ni kosa?
Ukiona mtu anatoka povu juu ya hizo tuhuma basi ujue ni katika wale wa kitengo cha mapambano ya JF
 
Hivi mtu anakuja hapa jamvini na kusema yeye ni Chadema halafu analeta hoja kama hizi hapa chini, unafikiri kwanini wafuasi wa chadema wasikuite msaliti(Na Mwisho wa siku anarudi CCM kwa mbwembwe), kwa mfano

1/Slaa kachukua mke wa mtu!!

2/Slaa katumwa na kanisa katoliki!!

3/Slaa alimtaka kimapenzi
Secretary wake.

4/Slaa anamiliki kadi ya CCM iliyolipiwa mpaka 2016.

5/Slaa ni pandikizi la CCM!!

6/Slaa iliiba fedha za kanisa katoliki wakati wa ziara ya papa!!

7/Mbowe sio mwanasiasa bali ni DJ na mchezesha Disco tu!!

8/Mbowe anaendesha chama kikabila!!

9/Mbowe elimu yake ni darasa la saba!!

10/Mbowe na Slaa ndio wanaongoza mipango ya mauaji dhidi ya raia!!

*Embu kaa kufikiri tu hizo hoja hapo juu zilivyo za kijinga, halafu tathmini na kufikiri kama mtu anayeleta hoja hizo kama atakuwa ameonewa kama ataitwa Msaliti na wanaChadema

Namba moja hata mtoto wa darasa la kwanza anajua ni kweli labda wewe great thinker tu ndio unjifanya hujui!jambo hilo liko wazi na huyo mama bado kamng'ang'ania tu

ushabiki wa kijinga@work
 
Mie naangalia siasa ya Tanzania sioni mbele.... Sioni mbele kwasababu most of politicians wanaongelea matatizo ya chama, kupigana vijembe, kufanyiana fitina etc
Sidhani Kama kuna Mtu anaipenda nchi hii miongoni mwao ( politicians) leave alone the mess ambayo chama ya wala kimeshafanya ambapo honestly sioni Kama wana dalili ya ku resolve wapo busy na ku attack chadema
Ila sishangai Africa haitokea kukawa na Democracy kwasababu kila Mtu anajali Tumbo lake na hatuangalii mbele
Tunatengeneza bureaucracy makusudi
 
GOOD ARGUEMENT; hii ni mojawapo ya sababu zinazonifanya nisitishe kuchangia mambo yanayohusu CHADEMA jamvini ingawa ni MWANACHAMA. Washabiki wamekuwa wengi na hawachukui hata sekunde ku "reason" mambo, zaidi ya matusi na kejeri hata kwa mambo ya muhimu yenye malengo ya kujenga chama.

Naamini kuna wanachama wengi sana nikiwemo mimi ambao tumeanza kuhoji uamuzi wetu wa kuendelea kuwa MEMBER OF THE PARTY. Na ni kwa nia njema inayoambatana na mranganisho wa mategemeo Vis Matokeo. Washabiki ni watu hatari sana Mh Mrema ni shahidi.Chadema ilianza na wanachama, tena wenye malengo yanayofanana na wenye mwelekeo wa kiukombozi na ikafanikiwa sana.Leo chama kinakumbatia washabiki kuliko wanachama na kimewapa baadhi uongozi.Hii ni kwa sababu wanachama hu-hoji utendaji wa viongozi na mwelekeo wa chama, lakini Washabiki husifia na kupamba kila lisemwalo au litendwalo na viongozi.
WANACHAMA tunaliona hili mkuu, na LINATUSIKITISHA

hongera mkuu,umemaliza kila kitu mkuu,ila naomba niongezee kuwa jambo hili linatufedhehesha sana sie tulioanza safari na cdm,tena hata wazee waliopo nje ya uongozi wanashangaa sana hali hii na hawaamini kama cdm hii ya leo bado ina nia ile ile ya wakati ule wa kuleta mapinduzi ya kweli. INAFEDHEHESHA SANA
 
Back
Top Bottom