Hivi kwanini Tanga hainyang'anywi hadhi ya kuwa Jiji? Ni sehemu ya ajabu sana

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
3,590
8,475
Hivi kwa nini Tanga ni Jiji, maana naona pilikapilika kama za majiji mengine hazipo kabisa, ni Mji ambao umepoa mithiri ya Tabora, baiskeli huku ndio nyingi kuliko magari.

Vijiwe vya vijana vipo kila mahala, huku maisha ni mepesi sana, yaani ukiwa na 500 unakula ugali na mboga za majani.

Ukienda kula wali samaki unapewa kibua mzima na wali eti elfu 2. Nyumba za majani zipo mpaka katikati ya mji, nyumba zenye vibaraza vikubwa zile za kizamani ndio zimejaa.

Nyumba za matofali ya tope zipo kila mahala. Nyumba za miti pia bado zipo.

Wale wanawake wazuri wa Kitanga wala huku siwaoni kabisa, hivi hii ndio Tanga niliyokuwa naisikia nikiwa Dar es Salaam. Au kuna Tanga nyingine wakuu? Tofauti na hii ya Forodhani, Chumbageni, 16, Donge, Majani Mapana, Gofu Chini n.k.

Sehemu za kula bata Tanga hazipo kabisa. Wanawake wa huku wanapenda wageni sana kuliko wenyeji sijui kwa nini?

Kiukweli Tanga ni sawa na Tabora tu, Wala Tanga haina hadhi ya kuwa Jiji.
 
Wenyewe Wanapambana Mkoa Yaani Jiji Ligawanywe
Kuwe Na Mkoa Wa Tanga, Na Wengine Waitwe Mkoa Wa Usambara.

Nakukumbusha Usishangae Tanga, Umefika Dodoma Lini Nalo Ni Jiji

Morogoro Yenye Hotels Nyingi Nzuri Inasubiri
Dodoma Ambayo Haiwezi Kupokea Wageni Wa Kimataifa
Ni Jiji
 
Wenyewe Wanapambana Mkoa Yaani Jiji Ligawanywe
Kuwe Na Mkoa Wa Tanga, Na Wengine Waitwe Mkoa Wa Usambara.

Nakukumbusha Usishangae Tanga, Umefika Dodoma Lini Nalo Ni Jiji

Morogoro Yenye Hotels Nyingi Nzuri Inasubiri
Dodoma Ambayo Haiwezi Kupokea Wageni Wa Kimataifa
Ni Jiji
Mkuu Dodoma nilifika mwezi wapili nilikaa siku 6. Dodoma haifai kuwa jiji lkn afadhari ya Dodoma kuliko Tanga. Lkn pote kwa ujumla hapafai kuwa jiji.
 
Back
Top Bottom