Hivi kwanini serikali haikuwepo kwenye hukumu ya bae system???

babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
79
Jamani jana nilisikitika saana nilipokuwa nasikiliza Taarifa ya habari kupitia moja ya TV station hapa Bongo walipokuwa wakihojiana na mwandishi wa habari Ayoub Mzee toka Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Southwark Crown ya jijini London, Uingereza, kuhusiana na hukumu iloyokuwa ikiikabili BAE system juu ya kesi ya Rada waliyoiuzia TZ. Kilichonisikitisha ni kutokuwepo kwa kiongozi yeyote wa serikali kwa ajili ya kufuatilia nini kilichojili katika kesi hiyo. Si waziri wa mambo ya nje wala balozi wa TZ hapo UK hata afisa yeyote wa ubalozi hapo uk. Pamoja na BAE kutakiwa kulipa faini ya paundi 30,000. ambapo kati ya pesa hizo wanatakiwa wailipe mahakama jumla ya paundi laki saba kama gharama ya kuendesha kesi hiyo na pesa inayobaki ilipwe serikali ya Tanzania. Kinachoumiza katika hili ni kuwa ili pesa hii ilipwe kwa serikali ya TZ ni juu ya serikali ya TZ kufuatilia na kuomba ilipwe pesa hiyo. Sasa kama wangelikuwepo hapo mahakamani si ingelikuwa rahisi kwao kufungua kesi ili walipwe kama ilivyoamua mahakama??? Lakini mhhh wapi. Hofu yangu hapa ni kuwa hii pesa itaingia mifukoni kwa wajanja wachache haitoingia kwenye mfuko wa serikali
 
Kwani tz tuna serikali? we chukua chako mapema sepa, siku tukipata serikali tunaanza upya.
 
viongozi wenyewe karibu wote mafisadi..... ni wachache wanaweza kuwa na moral authority ya kwenda kusikiliza hukumu ya hiyo kesi....:embarrassed:
 
Back
Top Bottom