Hivi kwanini mtu akija huku Dar anapenda lafudhi ya kiswahili chetu?

Zombie S2KIZZY

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
823
1,613
Hivi kwanini mtu akija huku Dar anapenda lafudhi ya kiswahili chetu?

Yaani unakuta mtu anaiga kabisa ule uongeaji sijui na yeye aonekane kazaliwa huku?

Sasa kibaya zaidi anavyoongea ni hovyo yaan unaona anajilazimisha na anakosea, hii kitu siipendi kichizi. Ndugu zetu mnaotoka mikoani acheni kulazimisha lafudhi ,kama lafudhi yako ni ya kisukuma, kikurya, kichaga, kimasai nk.

Wewe ongea sisi tunawaelewa na hatuwacheki maana mjini msingi pesa sio lafudhi, mbona wanangu wa ngarenaro wanaongea kwa lafudhi Yao alafu shega tu.

Huu mtazamo tu,

Sorry kwa niliowakera🙏

Screenshot_20231009-095139_1.jpg
 
Hivi kwanini mtu akija huku dar
aanapenda lafudhi ya kiswahili chetu ?
Yaan unakuta mtu anaiga kabisa ule uongeaji sijui na yeye aonekane kazaliwa huku ?
Sasa kibaya zaidi anavyoongea ni hovyo yaan unaona anajilazimisha na anakosea ,
hii kitu siipendi kichizi .
Ndugu zetu mnaotoka mikoani acheni kulazimisha lafudhi ,kama lafudhi yako ni ya kisukuma,kikurya,kichaga,kimasai nk,
Wewe ongea sisi tunawaelewa na hatuwacheki maana mjini msingi pesa sio lafudhi.
Sorry kwa niliowakera🙏
View attachment 2780113
Sasa wewe kinachokuudhi nini?

Kwani akiiga humuelewi?
 
Hivi kwanini mtu akija huku dar
aanapenda lafudhi ya kiswahili chetu ?
Yaan unakuta mtu anaiga kabisa ule uongeaji sijui na yeye aonekane kazaliwa huku ?
Sasa kibaya zaidi anavyoongea ni hovyo yaan unaona anajilazimisha na anakosea ,
hii kitu siipendi kichizi .
Ndugu zetu mnaotoka mikoani acheni kulazimisha lafudhi ,kama lafudhi yako ni ya kisukuma,kikurya,kichaga,kimasai nk,
Wewe ongea sisi tunawaelewa na hatuwacheki maana mjini msingi pesa sio lafudhi.
Sorry kwa niliowakera🙏
Hongera kwa kuzaliwa Dar
 
Unamaanisha hii lafudhi mbovu ya Dar wasioweza kutofautisha matumizi ya R na L.
Chakura, dalasa, karamu, kalatasi nk.

Tofautisha 'slang' na lafudhi. Nahisi unamaanisha ile misemo ya ovyo ya kuigana ambayo huwa ina trend kwa muda na kupotea kama 'maokoto' kwa sasa.

Itakuwa ni mpumbavu huyo wa kuiga lafudhi mbovu kabisa ya watu wa dar.

Pwani yenye lafudhi nzuri ni Zanzibar na Tanga tu, na Tanga ni wadigo pekee.
 
U
Unamaanisha hii lafudhi mbovu ya dar wasioweza kutofautisha matumizi ya R na L.

Chakura
Dalasa.

Itakuwa ni mpumbavu huyo wa kuiga lafudhi mbovu kabisa ya watu wa dar.

Pwani unayoongelea wewe yenye lafudhi nzuri ni Zanzibar na Tanga tu, na Tanga ni wadigo pekee.
Unaongelea Mara au Dar?.....ukiona mtu anaongea hivyo ujue katika mkoani
 
Hivi kwanini mtu akija huku dar
aanapenda lafudhi ya kiswahili chetu ?
Yaan unakuta mtu anaiga kabisa ule uongeaji sijui na yeye aonekane kazaliwa huku ?
Sasa kibaya zaidi anavyoongea ni hovyo yaan unaona anajilazimisha na anakosea ,
hii kitu siipendi kichizi .
Ndugu zetu mnaotoka mikoani acheni kulazimisha lafudhi ,kama lafudhi yako ni ya kisukuma,kikurya,kichaga,kimasai nk,
Wewe ongea sisi tunawaelewa na hatuwacheki maana mjini msingi pesa sio lafudhi,
Mbn wanangu wa ngarenaro wanaongea kwa lafudhi Yao alafu shega tu.
Huu mtazamo tu,
Sorry kwa niliowakera🙏
View attachment 2780113
Hongera kuongea kidaslam na kuzaliwa daslam
 
Unamaanisha hii lafudhi mbovu ya dar wasioweza kutofautisha matumizi ya R na L.
Chakura, dalasa, karamu, kalatasi nk.

Tofautisha 'slang' na lafudhi. Nahisi unamaanisha ile misemo ya ovyo ya kuigana ambayo huwa ina trend kwa muda na kupotea kama 'maokoto' kwa sasa.

Itakuwa ni mpumbavu huyo wa kuiga lafudhi mbovu kabisa ya watu wa dar.

Pwani yenye lafudhi nzuri ni Zanzibar na Tanga tu, na Tanga ni wadigo pekee.
Hao uliowaongelea ndio aliokua anawasema mtoa mada sasa, wanaharibu halafu asiyejua anahisi ni wa town kumbe mluga luga wa mkoani.
 
Asilimia 90 ya hapa dar ni wa kutoka mkoa sasa unaanzaje kuiga??, Ingekuwa hivyo mbona rahisi tu maana kila siku wanasikika kwenye radio na runinga na wangeweza kuiga

Nachofahamu watu aina yoyote wakitoka mahali waliko na kwenda mjini zaidi huwa na desturi ya kuboresha matamshi yao hasa katika lugha ya kiswahili

Maana kuna baadhi ya mikoa na sehemu hupenda zaidi kuzungumza kilugha kwa hiyo akifika katika mji wowote mkubwa ambako matumizi ya kiswahili ni mengi lazima ataboresha uzungumzaji wake ikiwemo kutamka maneno kwa usahihi haijalishi Dar tu,

hata mtu akitoka Katavi akifika Mbeya mjini atazungumza kama watu wa huko sababu ya kuongea nao
 
Unamaanisha hii lafudhi mbovu ya dar wasioweza kutofautisha matumizi ya R na L.
Chakura, dalasa, karamu, kalatasi nk.

Tofautisha 'slang' na lafudhi. Nahisi unamaanisha ile misemo ya ovyo ya kuigana ambayo huwa ina trend kwa muda na kupotea kama 'maokoto' kwa sasa.

Itakuwa ni mpumbavu huyo wa kuiga lafudhi mbovu kabisa ya watu wa dar.

Pwani yenye lafudhi nzuri ni Zanzibar na Tanga tu, na Tanga ni wadigo pekee.
Nikiongea na mtu hata kama nilikuwa namuheshimu kiasi gani akiingiza hili neno wala simzingatii tena.

Nitaacha aongee anavyoweza tukiagana yote nayasahau.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom