Hivi kwanini mpaka sasa "Chama cha Walimu Tanzania (CWT)" kinashindwa kujiendesha chenyewe kwa mtaji waliopata kutoka kwa Walimu.

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) chini ya uongozi wako kimepoteza umaarufu, uelekeo, maono, dira kama chama cha wafanyakazi kwasababu zifuatazo

Kimsingi Chama Cha Walimu siyo taasisi ya kujifurahisha, ni taasisi ya HARAKATI za kumkomboa Mwalimu wa Tanzania kwa maendeleo ya Mwalimu

Lakini ukichungulia uelekeo wa sasa naona chama hiki ni shirika la fedha.

Chama hakina kumbukumbu za Walimu Hakijui wako wapi, wanafanya nini, wanafanyiwa nini au wanastahili kufanyiwa nini na chama pamoja na mwajiri. Chama hakijui ni Mwalimu yupi kaajiriwa lini na analipwa vipi na ni lini wanapaswa kupandishwa vyeo/madaraja, kubadilishiwa miundo na kulipwa stahiki zao kwa wakati.

MY TAKE!

Kiujmla chama kina hazina kubwa ya fedha nadhani kisimame chenyewe, kujiendelea kwa kufanya jambo lingine ili kuwalipa wafanyakazi wake walikuwepo.

Pili kama ni ngumu basi kiwe kinawapa walimu asimilia kidogo katika wakati wanastaafu, sio zile bati 20 tu. Yani mwalimu anastaafu umekata hela yake yakutosha unampatia mabati 20 jamani hiki sio chama ni kundi la kifisadi.

Maana faida ya hiki chama mpaka sasa sijaona.

Mr mkiki
 
Wezi wakubwa hao, walikuwa na mtaji mkubwa Bil 20 wakaamua kuanzisha bank yao na kuuza hisa kwa waalimu, mwaka 2015 JPM akawaambia waikopeshe serikali kwaliji ya kampeni na zitarudi

Baadae hazijarudi na Mwenyekiti wa CWT Taifa akanywea mpaka leo ni kupigwa tu ahadi hewa, hakuna cha benki wala Mwalimu yeyote aliyenunua hisa CWT.

Kujenga heshima kwa CWT ni waanzishe bodi yao ya ualimu, iwe Professional Course yenye board then pamoja na CERTIFICATE waalimu wapewe LICENCE pia na wawe na board ya kuwatetea serikalini kama walivyo wahasibu, Wahandisi, Madaktari n.k

Bila hivyo CWT na Waalimu wake watadharauliwa tu na serikali siku zote
 
CWT Ni kibaka Kama vibaka wengine, mana wanachukua pesa bila ya lidhaaa ya mwenyewe! Naamini hakuna mwalimu anayetaka kukatwa hiyo 2%
 
CHAKAMWATA kilikuja na utaratibu mzuri wa makato ya 1% kwa kila mwanachama, na pia kumrejeshea mfanyakazi 50%ya michango yake yote atakapostaafu , lakini walipigwa vita kila kona. Mpaka viongozi wengine mikoani na wilayani walishirikiana na CWT kuwatisha walimu na kuhakikisha chama hicho hakifanyi kazi kwenye mikoa yao. CWT ni pilipili chungu kwa walimu.
 
Wote wapigaji tu, hakuna wakumtetea mwalimu hapo ila wanaangalia fursa.
 
Wezi wakubwa hao, walikuwa na mtaji mkubwa Bil 20 wakaamua kuanzisha bank yao na kuuza hisa kwa waalimu, mwaka 2015 JPM akawaambia waikopeshe serikali kwaliji ya kampeni na zitarudi

Baadae hazijarudi na Mwenyekiti wa CWT Taifa akanywea mpaka leo ni kupigwa tu ahadi hewa, hakuna cha benki wala Mwalimu yeyote aliyenunua hisa CWT.

Kujenga heshima kwa CWT ni waanzishe bodi yao ya ualimu, iwe Professional Course yenye board then pamoja na CERTIFICATE waalimu wapewe LICENCE pia na wawe na board ya kuwatetea serikalini kama walivyo wahasibu, Wahandisi, Madaktari n.k

Bila hivyo CWT na Waalimu wake watadharauliwa tu na serikali siku zote
Aisee
 
Back
Top Bottom