Hivi kwanini hivi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kwanini hivi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Aug 9, 2010.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Habarini wakuu!
  Kama mnakumbuka kuna thread moja niliweka " KILA NIKIAMKA" wengi walinipa ushauri wa kuoa haraka kutokana na sababu mbalimbali walizonipa! Nilichukua ushauri wao nami nikaa na GF wangu kipenzi nikamuelezea juu ya mawazo na maamuzi niliyofikia naye akakubaliana nami! GF wangu ni wa kiislam na mimi ni wa christian! Alipeleka mawazo yake kwa wazee ila upande wao hawakuwa tayari kutokana na tofauti za itikadi zetu za kuabudu! ila walipenda mie niingie uislam na tufunge ndoa msikitini na nifuate mafundisho yao! Sasa bado sijafanya maamuzi yeyote juu ya hili ila nina swali " Kumekuwa na hii kitu, Mdada wa kikristo akitaka kuolewa na muislam huwa hamna vipingamizi saaaana na wala hakuna milolongo ya mambo yanayopelekea kutofunga ndoa , ila mdada wa kiislam akitaka kuolewa na mkristo basi panatokea mapingamizi makubwa kiasi kwamba wengine hutofautina na wazazi na pengine hupelekea kufunga ndoa za kiserikali na kukaa pamoja" Hii ni kwa nini inakuwa hivi???? Wadau naomba tujadili kwa kina hasa?!!!
   
 2. M

  Mgalatia JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 28, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa maoni yangu ni kuwa hili jambo hutokea tu pale wazazi wanapokuwa na imani sana na dini yao na wanaipractice sana. Kama mdada mkristu haijui vema dini yake na wazazi hali kadhalika (wakristu wa majina) hawataona ni issue binti yao kwenda kuolewa na muisilamu.Ila kama wazazi ni wakristu kweli binti anaenda kule ambako hakuna ubatizo wakikubali ni kama vile wanaruhusu mtoto wao kwenda upotevuni maana wanaona kuwa mwisho wa safari binti yao hatafika mbinguni hivyo wangependa binti yao aolewe na mtu wa imani yao. Hali kadhalika mwisilamu wa jina lakini ha practice uisilamu hataona ni issue binti yao kwenda kuolewa na mkristu. Ila kama wazazi ni waisilamu haswa hawatakubali binti yao aolewe na mtu wanayemuona kama amepotea,hajamwagiwa maji. Ni suala la imani tofauti tu. Ndio maana binadamu tunaagizwa ili kulinda imani na amani tuoane watu wa dini na dhehebu moja.
  :smile-big:
   
 3. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  suala la dini ni imani ya mtu sipendi kuongelea hayo mambo kwa sana ila nakushauri ufunge ndoa ya kiserikali halafu baada ya muda mkishasimama kwenye maisha yenu mnaweza kuamua kuchagua dini moja ya kufuata.
   
 4. malisak

  malisak JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 16, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  Ukitaka lako wala usimsikilize mtu angalia mapenzi yako kwake hilo ndio la msingi haiendi dini kuishi na mke ila ni nyie kama mmeridhiana sawa ila vipingamizi vikizidi viheshimuni au kuweni wapagani
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Vimeshazidi na Nimezoea kuabudu Upagani siwezi mmmmh:confused2:
   
 6. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,074
  Trophy Points: 280
  pole kaka ukiona vipi mmimbishe tu wenyewe watakuwa wapole
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwa njia hii nitafanikiwa kweli halafu sikupenda iwe hivi
   
 8. chloe.obrain

  chloe.obrain JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sure!! kama kweli mnapendana then wazazi wanaleta longolongo za dini fanyeni kama hapo kwenye red.
   
 9. F

  Fanta Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nadhani inategemea na msimamo wa wazazi. wengine kama hivo wanasimamia wanachoamini. it has nothing to do with mdada ni mkristo au mwislam. mwisho wa siku idhini ya wazazi kwenye ndoa za dini tofauti inategemea sana na misimamo yao ya dini.

  lakini imezoeleka pia kuwa mara nyingi msichana akiwa anaolewa na mtu wa dini tofauti yeye ndo hubadili dini na kuwa mfuasi wa dini ya mume wake. (ni mazoe tu)

  wakati nikosoma hii post nimejiuliza 'hivi idhini ya wazazi ni lazima ili watoto wao wafunge ndoa? (kwa dini yangu ni muhimu vinginevyo sahau kuoa/kuolewa ndoa ya kidini
   
 10. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  kaaaazi kwelikweli
   
Loading...