Hivi kwanini CHADEMA wanaharibu vipaji vya vijana?

Hivi kwanini CHADEMA wanaharibu vipaji vya vijana?

Mpangawangu

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
887
Reaction score
965
Chadema ni Mtambo wa kuua vipaji.
Wapo wazazi wengi huzaa watoto na kuwakataa,
Watoto waliokataliwa huishi maisha ya dhiki,kufadhiliwa na wapita njia,majirani nk

Mtoto akipata mafanikio ukubwani,baba anajitokeza....

Tabia hizi zipo Chadema,Wanasiasa wenye vipaji huzamishwa majini ili wasihatarishe utawala wa Mfalme.

Hutukanwa kila aina ya matusi Duniani,lkn wanapohamia vyama vingine na kupata mafanikio kisiasa ,Malaghai ya Chadema huanza kujileta na kujifanya yanatoa ushirikiano.

Mwaka 2009,Kafulila alishinda uchaguzi wa Bavicha,Slaa na Mbowe wakatengua matokeo baada ya mtoto wao Mpendwa heche kushindwa vibaya.

Kafulila akaambiwa ameshinda kwa rushwa kwa msaada wa Zitto Kabwe.

Kafulila akaitwa sisimizi na kutishiwa maisha,kafulila akaambiwa hata atambikie kamwe hata pata tiketi ya chadema.

Leo Kapewa tuzo ya HR,Baba mlaghai kajitokeza kujinufaisha na mafanikio ya Mtoto aliekataliwa na kuitwa sisimizi.

Huu ni ulaghai uliochupa mipaka.

Chadema ni mtambo wa kuua vipaji.
Cc.Ben Saanane,Zitto Kabwe,David Kafulila,Mtela Mwampamba,Juluana Shonza ,Habib Mchange.
 
Back
Top Bottom