Hivi, kwa nini wanatudhalilisha namna hii?

bigmash

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
416
421
Leo nimekutana na kesi inayomhusu mchina mmoja kamtukana mtanzania kwa kumuita nyani, kesi ipo police ila sijui nini kilijiri kwenye hiyo kesi. Ninachotaka kujadili hapa ni kwamba imekuwa ni kawaida sana kwa hawa watu weupe yaani wazungu, waarabu, wachina na wengineo wanaojiona bora kwa sababu ya weupe wao kututukana sisi waafrika kwa kutuita nyani kwa sababu tu ya ngozi yetu nyeusi.
Tumeshuhudia mpaka watu maarufu wakiwemo wanamichezo mbalimbali katika ligi kubwa za ulaya na hata zile za FIFA wanandinga weusi wakirushiwa ndizi kwa kufananishwa na nyani. Kwa kweli ubaguzi huu hauwezi kwisha kwani upo kwenye damu zao hawa wenzetu.
Hapa sisi ngozi nyeusi ni lazima tutafute suluhisho juu ya suala na tuache kulalamika kuwa tunabaguliwa na kudharauliwa.
Hivi kwa nini na sisi tusiwaite manguruwe? Maana kama sisi wanatuita nyani na wao tuwaite nguruwe maana wamefanana ngozi zao na nguruwe, wakitutupia ndizi sisi tuwatupie pumba au mabunzi. Tuache kabisa kulalamika sasa hivi ila na sisi tujibu mapigo maana tumechoka, labda njia hii itasaidia kuliko kulalamika. Kumbukeni hii imekaa kiasili zaidi kwani hata mtu akiitwa jina la utani ambalo halipendi basi watu ndio huzidi kuliita, dawa yake ni kutafuta jina baya litakalo mkera anayekutania na wewe umuite jina hilo baya. Lakini tukiendelea kulalamika kwamba kila siku tunatukanwa, hawa jamaa hawataacha kutuita nyani. Kuanzia leo na sisi tuwaite pigs (manguruwe) labda watabadilika.
Nawasilisha.
 
Kumuita mtu Nguruwe anayekuzidi kila kitu in all walks of life, wala jina halitashika! Sijui tufanyeje? Umasikini wetu! Wewe hapo unaangalia upenyo wa kwenda "Majuu"
 
Wanajua mnafikiri kwa matumbo yenu!
Njaa/shida ni kitu mbaya sana.
 
Au na sisi tuwaite nguruwe au! Maana wamefanana sana rangi.
 
Tatizo ni sisi watu weusi wenyewe kutokujikubali, na tunaona kama ngozi nyeupe ndio yenyewe, kujidharau Sisi wenyewe, kutojiamini. Kiasi Kwamba hata mzungu au mchina anachukua advantage hapo yakutuona sisi ni watu wa chini na wao ni zaidi yetu
 
Kama waafrika baadhi wakiacha kujichubua ngozi zao ziwe kama za hao wazungu au wachina. Basi watatuheshimu
 
Unajua kwanini wakawa wanaita watu weusi ndani? Kwasababu nyani kazi yake kula tu na akimuona mwenye shamba anamfanyia fujo. Sasa angalia viongozi wetu wanavyowafanyia fujo wananchi, halafu angalia mtu mweusi zaidi ya kula kavumbua nini zaidi hapa duniani? Mchina huyu huyu alikuwa taabani kimaisha baada ya kupewa uhuru angalia alipo na sisi waafrika tulipo. Yeye anajitegemea sisi tunamuomba mchina na wote tulikuwa taabani nchi zetu.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Wapo sahihi kabisa kutuita nyani!....Kama tv zinazimwa,kodi zetu zinatumika kununua wapinzani,rais anafanya ukanda kwa kutengeneza viwanja vya ndege kwake bila kuangalia sababu za kiuchumi,watu wanauawa bila sababu,watu wanapotea,uhuru wa kujieleza unaminywa e.t.c halafu tunakaa tu kimya je sisi tutakuwa ni binadamu kweli??....Huoni kwamba tofauti yetu na wanyama ni ndogo sana???....Mtu akituita manyani atakuwa ametuonea kweli??....mtu akituita makima atakuwa amekosea???
 
Kumuita mtu Nguruwe anayekuzidi kila kitu in all walks of life, wala jina halitashika! Sijui tufanyeje? Umasikini wetu! Wewe hapo unaangalia upenyo wa kwenda "Majuu"
Tuwaite tu mkuu, labda watabadilika kuliko kukata tamaa.
 
Wapo sahihi kabisa kutuita nyani!....Kama tv zinazimwa,kodi zetu zinatumika kununua wapinzani,rais anafanya ukanda kwa kutengeneza viwanja vya ndege kwake bila kuangalia sababu za kiuchumi,watu wanauawa bila sababu,watu wanapotea,uhuru wa kujieleza unaminywa e.t.c halafu tunakaa tu kimya je sisi tutakuwa ni binadamu kweli??....Huoni kwamba tofauti yetu na wanyama ni ndogo sana???....Mtu akituita manyani atakuwa ametuonea kweli??....mtu akituita makima atakuwa amekosea???
Hiyo sasa siasa kumbuika hata aliyekuwa rais wa marekani Barack Obama naye alibaguliwa japo anatoka nchi iliyoendelea, aliitwa bastard son (mtoto wa mwanahamu) kwa sababu tu ni mweusi.
 
Tunavyo 'omba omba' na kufanya vitu vya kipuuzi lazima watudhalilishe. Kwa mfano tuko tayari kurudia uchaguzi kwa mabiioni kadhaa (cash) wakati huo huo tunashindwa kujenga vituo vya afya, kuboresha elimu n.k. Kwahiyo jamaa wakiangalia vipaumbele vyetu wanaona kabisa sisi sio binadamu wa kawaida na mwisho wa siku wanatufananisha hata na sokwe.
 
Kwanza anza kujikubali kwanza!!

Mwenzio mpaka akuite nyani kajikubali na kujiamini.

Punguzeni ndoto za kukimbilia urahisi wa maisha ughaibuni na mjivunie uafrika wenu kwanza!

Tukifika hapo ata tukiwaita manyumbu itawauma!!
 
Back
Top Bottom