Yaani mara ya kwanza kumtumia demu msg ya kumtaka kimahusiano basi kama dakika 3 hivi msg ikaingia kwenye simu yangu basi kwa ule mshtuko niliopata sikuifungua muda huo kwanza niliendelea kufanya kazi zangu huku kijasho kinanitoka hapo nawazia jibu lipi limerudishwa nikamaliza kazi yangu nikaoga.
Basi nikaenda sehemu nikaagiza kinywaji ile naanza kunywa nikatoa simu mfukoni nisome jibu la msg yangu nakuta simu imezima chaji.
Hivi kuna mahusiano gani ya msg na mshtuko wa mapigo ya moyo kuongezeka?