....X-Paster kweli USA watu hawapewi msaada ovyo ovyo, ila ninachoweza kusema baadhi ya wamarekani ni wavivu, hawataki kufanya kazi na watu nguvu wanazo........kuna wengine kazi wanachagua. Wengine walishaingia kwenye bad credit na crimes nyingi haswa madawa mtu kama huyo hawezi pata msaada serikalini. Ndio mwisho wanaishia kuwa homeless.
Hivi uliwahi kujiuliza kwa nini immigrants wengi huko marekani huwezi kuwakuta wakihangaika kama wazawa wa hapo USA? Kwa sababu kwanza immigrants wanachapa kazi kisawa sawa na hawachagui kazi. Sasa hao wamarekani waliochoka na kuwa homeless wamejitakiwa wenyewe. Wengine wakifanya kazi haswa hao weusi, baada ya kupata paycheck hata kazini haendi.
.....USA ni land of opportunity, kama mtu umetulia na kuchapa kazi na kutojiingiza kwenye crimes utafurahia mema ya nchi. Hata kama bahati mbaya umepoteza kazi, na huna crimes yoyote utalipiwa bills zako zote za muhimu kama nyumba, umeme na maji. Utapewa food stamps na serikali watakupa minutes chache kwenye simu.
Vile vile ukistaafu kuna kitu kinaitwa social security benefits, hii utaipata kila mwezi hadi hapo utakapoondoka duniani. Hao homeless wanajitakia wenyewe, naweza sema wavivu na hii ni kawaida kwa viumbe sisi binadamu hatufanani. Nchi hata iwe na utajiri lakini lazima utakuta kuna wavivu/kilaza.
Na hao wanaohangaika na watoto hapo wanatakiwa kwenda shelter za serikali au za makanisa, zipo kila mji, sema ukienda huko hakuna sigara wala beer na ni marufuku kukaa shelter kama unakunywa au kuvuta, utafukuzwa.......hivyo wanaona bora kuomba omba kupata pesa ya sigara na pombe badala ya kwenda shelter.
[h=3][/h]