Mentor
JF-Expert Member
- Oct 14, 2008
- 20,328
- 23,890
1. Hivi kwa nini nafasi za uongozi Tanzania bado tunapeana kwa hisani?
.
kwa nini nafasi serious za kiutawala zisipewe kwa watu wenye taaluma za utawala au taaluma zifananazo na hi to! Au kama hana basi awe na 'distinguished performance' ya uongozi/utawala. Sitaji mifano.
.
2. Hivi kwa nini Tanzania sifa za kuwa mbunge zisibadilishwe kutokana na uhitaji wa nchi na mabadiliko tunayopitia?
.
Naamini wakati wanapitisha sheria kuwa 'sifa ya kuwa mbunge ni ujue kusoma na kuandika' hatukuwa na wasomi wengi. Ila sasa, sehemu yenye kutunga sheria, miongozo na kanuni za uendeshwaji nchi kutumika kama dawati la kupashana na taarabu sio sahihi.
Narejea maneno ya mh. Zitto, "...sasa uchaguzi umeisha, tujenge nchi..."
.
3. Hivi kwa nini bunge lisingekuwa linakaa wiki moja tu...au zaidi sana siku kumi tu. Kuna nini cha maana cha kukaa bunge wiki mbili tatu?
.
4. Hivi kwa nini na sisi Tanzania hatupitishi sheria ya kuzuia kelele?
.
kwa bahati mbaya nipo Moshi na siku mbili tatu nimekuwa nikiishi karibu na ilipo Rau pub. Ni sehemu ya wazi na wanapiga mziki jumatatu hadi jumatatu. Kwa kweli ni kero. Kama unataka kufanya hivyo jenga jengo lako weka sound proof piga mziki hadi mchana.
.
5. Hivi kwa nini vyuo vyote visipitishe dress code kwa wanafunzi wao?
.
mfano huu pia ni wa Moshi, MoCU (MUCCoBS au zamani Chuo cha Ushirika). Nilipita hapo nikawa najisemea kichwani, wadada wa Moshi ni wazuri...maana walikuw wamevaa vizuriii smart na ukimuona mzuri basi ni mzuri kweli na sio kwa sababu amevaa kimtego.
.
6. Hivi kwa nini ili kuwa lecturer usisomee hata Post graduate diploma ya ualimu?
.
kuwa na GPA ya 3.8 au zaidi sio kigezo cha kujua kufundisha. Kuwa mwalimu wa chuo hakukufanyi uwe tofauti na mwalimu wa shule ya msingi. Natamani hii iwe hivyo maana nimeona ni tatizo kwa walimu wengi hasa vijana wa siku hizi.
.
Lakini pia ngoja nitoe mfano wakati nikiwa polisi. Wakati kuruta wanapomaliza mafunzo, huwa kuna wanaochaguliwa kubaki chuoni ili wawe walimu. Kuchaguliwa huku kunaendana na uwezo na ubora wa wanafunzi hao walipokuwa chuoni. yaani, wale waliokuwa na uwezo mzuri wa kuongoza wenzao, wenye sauti nzuri za kuamrisha, wepesi wa kupokea maelekezo, wepesi kuelewa na wagumu kusahau.
.
Lakini pamoja na ubora wao huo, ni lazima waende kozi ya ukufunzi ya kati ya miezi mitatu hadi sita, ili kufundishwa jinsi ya kufundisha. Unaweza ukawa unajua sana lakini kama utashindwa kukimega unachokijua basi hufai kufundisha heri uende mkoani huko ukatumikie raia wengine.
.
Je, si zaidi sana kwa walimu hawa wa vyuo? natamani ningeandika zaidi juu ya hili....
Hivi kwa nini...?
#Tanzania