Hivi kuwepo karantini lazima utoe hela?

Hivi kuwepo karantini lazima utoe hela?

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
17,029
Reaction score
23,695
Ndugu yangu ambaye ni mtanzania Kama Mimi Jana alienda kupima Corona pale hospital ya TMJ Mikocheni baada ya kuhisi kama ana ugonjwa wa Corona. Baada ya kupimwa akataka aondoke akaambiwa abaki mpaka kesho ndiyo atapewa majibu so akapelekwa karantini ikabidi akae hapo mpaka kesho.

Kesho ilivyofika akapewa majibu ni negative ila akaambiwa hawezi kuondoka mpaka alipe gharama ambayo ni laki 3.5 ya kuwepo pale baadae akapunguziwa mpaka laki 2 ndugu yangu akashangaa kwasababu yeye alizani ni bure na alienda pale kwa lengo la kupima tu na hao ndio waliomlazimisha alale hapo karantini na hawakumwambia kama hizo gharama zitakuwepo.

Ndugu zangu hili suala limekaaje? Mwenye kujua atujuze please
 
Mbona wana majumba Mengi sana ,mengine yamekoswa wapangaji, mengine wanauziana kwa Bei cheee? Hivi majumba yao ya shirika yanakazi gani?

Yaan mtanzania Mimi, uniweke karantini , Unilipishe Pesa yote hiii?

Aki ya mama kuondoka naondoka bila kulipa, alafu ndo tuone matumizi ya nguvu yalivo.
 
Back
Top Bottom