Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Tumemsikia wenyewe siku ya jana kwenye kongamano la uchumi, lililofanyika chuo kikuu cha Dar, Rais Magufuli akieleza kuwa hawezi kutenga fungu la pesa kwa ajili ya kuwapa posho wajumbe kwa ajili ya kuandaa Katiba mpya!
Akaendelea kueleza Mheshimiwa Rais kuwa ni heri pesa hiyo aipeleke kujenga reli ya Standard gauge........
Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa kuhusu msimamo huo wa Rais. Je tunavyotumia mabilioni ya pesa katika kurudia uchaguzi, kwa wagombea wanaotoka upinzani, wakigombea kwa nafasi zile zile walizokuwa nazo awali, je hayo ndiyo matumizi mazuri ya pesa zetu??
Vile vile nimjulishe Mheshimiwa Rais kuwa kilio cha Katiba mpya ni cha mamilioni ya watanzania, na wanaoipinga hii Katiba mpya ya Tume ya Warioba ni watu wachache sana walioko kwenye ngazi ya utawala
Hivi ngoja nimuulize swali jingine Mheshimiwa Rais, hivi hii pesa ya kuandaa Katiba mpya inatoka mifukoni mwake??
Kwa kuwa kwa namna alivyoongelea kuwa yeye hawezi toa pesa za kuwalipa posho "bure" kwa wajumbe wa Bunge la Katiba, utadhani pesa hiyo inatoka mifukoni mwake!
Nimuulize swali jingine, hivi haoni jinsi Taifa linavyopoteza mabilioni ya shilingi katika kurudia chaguzi ndogo kutokana na CCM "kuwanunua" wabunge hao wa upinzani??
Hivi tukilinganisha matumizi ya kurudia chaguzi ndogo na Taifa kupata Katiba mpya, hivi ni matumizi gani ambayo kiuhalisia ni ya hovyo kabisa??
Kwa kuwa kwa namna alivyoongelea Jana, ni kama pesa hiyo anavyoionea uchungu kama inatoka mifukoni mwake na hazitoki kwenye hazina ya Taifa!
Nipende tu kumfahamisha Mheshimiwa Rais kuwa ametoa mawazo yake binafsi na ya wenzake wachache wa CCM, lakini atambue kuwa mamilioni ya watanzania bado wanaililia Katiba mpya, kwa kuwa wanajua kuwa Katiba iliyopo sasa ni kama ya mfumo wa chama kimoja cha CCM na imempa madaraka makubwa mno Rais, na ndicho wananchi wanachoona umuhimu wa kupata Katiba mpya
Kwa hiyo niwashauri wananchi, tusikatishwe tamaa na kauli ya Mheshimiwa Rais na tuendelee kuidai kwa nguvu zote ili nchi yetu iweze kupata Katiba mpya ambayo ndiyo itakayotupa dira nzuri na ustawi wa nchi yetu na ndiyo itafaa katika kipindi cha sasa cha mfumo wa vyama vingi
Mungu ibariki Tanzania