Hivi kuna wakati mgumu maishani kama ambao chanzo chako cha kipato kimedorora na huoni njia nyingine ya kujikimu ?

Hivi kuna wakati mgumu maishani kama ambao chanzo chako cha kipato kimedorora na huoni njia nyingine ya kujikimu ?

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
935
Reaction score
3,014
Kuna wakati mwingine maisha huingia giza, ni pale ambapo shughuli yako kuu inadidimia, kipato kinapungua, na haionekani njia nyingine ya kujikimu.

Hali hizi husababishwa na mtu kuzoea kitu flani muda mrefu ila ghafla mambo yanabadilika, Ushindani na ubunifu unazidi sokoni, kitu anachofanya kimepitwa na wakati, wateja kuhama, n.k.
  • Mchuuzi sokoni aliyekuwa na wateja wengi kila siku, sasa anahangaika kupata hata wateja watatu,
  • Mwanamuziki aliyekuwa na hits pamoja na shows kibao, sasa hapati show hata kijijini.
  • Dereva wa boda boda aliyekuwa akipata mizunguko mingi, sasa anakaa masaa bila mteja.
  • Mama ntilie ambaye chakula chake kilikuwa kikuu kwa wengi, sasa sufuria zinarudi zikiwa bado zimejaa.
  • Dereva wa teksi aliyekuwa akipata kipato kizuri, sasa anazunguka sana bila safari.
  • Mwanasoka aliyekuwa akicheza timu kubwa mshahara mzuri, sasa hana timu kabisa.
Huwa ni vigumu kukubali mabadiliko ya hali hasa kwa wale waliowahi kuonja maisha mazuri na kudhani yatadumu milele. Wengi wao hujikuta wakitumia pesa bila mpango, wakitumia kupita kiasi kwa dhana kuwa “kesho ipo tu.” Mara hali inapoanguka, huzidiwa na mshtuko na ni rahisi kwa kundi hili kuamini ushirikina
 
Kaza
img_4_1746950417468.jpg
 
Ukiwa na roho ndogo unaweza kusema ni ulozi au mikosi
😂😂Sio roho ndogo, amini kwamba watanzania 7 kati ya 10 huamini wamechezewa, wanajisahau sana zile nyakati nzuri za mavuno na faida kubwa kufanya vya maana wakidhani kwamba hali nzuri haitabadilika, kila wakiamka itakuwepo, mambo yakibadilika ni rahisi kuamini wamerogwa na ndio mwanzo wa kuporomoka zaidi
 
Hiyo hali ni ya kwanza kukupata wewe pekee duniani? Kama ni marudio basi nyanyuka kung'uta vumbi kisha songa mbele.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Niliwahi pitia kipindi kigumu nikiwa. Hom.before chuo baada yapo mi ni mbele tuu nipo na high despline...
 
Ukiwa home unasubiri chuo bado hujaanza hata kujitegemea, hayo ni mazoezi mepesi tu
Hv unajua skua hom nilikua nakaa sehmu flan hv temporary...

Nikakata tamaa ya kusoma nikawa nafanya kazi za saidia fundi

Mara nikawa fundi bomba.
Sijakaa vzr nikawa fundi kuchomelea..

Mkuu katika welding nilikua sana nipo upande wa ku grand na kupiga puti..

Kuna siku nusu mashine inikate, baati mbaya tu ikaenda kwengine.

Achana na hayo kuna siku chuma kikaingia kwa jicho kila nikilalamika wakawa wanasema niweke big g ndo kinatoka.

Nilikua nafanya kazi napata pesa ya nauli tu 5k kuna siku nilikosa kabisa nikatembea kwa mguu kutoka keko to mbande mkuu hiyo rout unaijua au unaiskia tu..
 
Niamini mimi, bado haujapitia magumu mkuu 😎
Mkuu kwanza kula ilikua ishu ukizingatia faza yupo nyanda za juu kusini alafu mama yupo kusini huko...

Hvyo nikawa dar natanga tanga tu hapo nikapata sehem ya kujishikiza an nafundisha nursery mkuu mshara ni 5ok kwa mwezi....

Hapo nikawa nalala humo humo class yaan kwa mkeka huku najifunika shuka na net..

Mkuu ile time sina smart nipo mm na kiswaswadi naskiliza story kwa redio tuu.
Unakuta hauli unavizia chakula cha madogo an asbh watt wanakunywa uji na mi hapo hapo napiga kwa watoto vitumbua mandazi na kazarika..
 
Wakuu mi nafatilia sana nyuzi za namna kama hii humu jf hvyo huwa najifunza mengi na wala sikurupuki kufanya kitu kama sijaja.huku..

Hii nazani ndo.inafanya mpaka sasa nipp hapa graph angu inapanda day after day na ata kama ikishuka basi ni kwa mipango ya mungu ambako tunasema Afya kubadilika au kupata ajali ukiacha hvo alhamdullilah tutaitana matajiri tuu hvo hvo kinafiki
 
Back
Top Bottom